Ishara Na Dalili Za Hamu Kubwa Ya Ngono (Kupenda Tendo La Ndoa Zaidi)

Ishara Na Dalili Za Hamu Kubwa Ya Ngono (Kupenda Tendo La Ndoa Zaidi)

Dawa ni mojawapo ya tiba ambazo zime dhihirishwa kuwasaidia watu wanao tatizika na uraibu wa matendo ya kingono.

Huenda ukawa umesikia kuhusu hamu kubwa ya ngono ama uraibu wa tendo la ndoa. Lakini huenda ukashangaa kujua kuwa kuna mjadala ikiwa ni kweli kuwa ni uraibu. Na cha kufurahisha zaidi, sio kuhusu ngono tu. Waraibu wa ngono sio watu wanao kuwa na hamu ya kufanya mapenzi kwa sana. Badala yake, wana matatizo yanayo wasumbua. Ishara za uraibu wa ngono ni kama vile mawazo mengi, kuwa na wasiwasi, kukwazwa kimawazo na kuaibika ndizo zinazo waingiza katika tabia hatari za kingono.

Hamu kubwa ya ngono ni nini?

hamu kubwa ya ngono

Tendo la ndoa sio tatizo kwa watu wengi, lakini ni tatizo kwa baadhi ya watu. Hamu kubwa ya ngono ni kauli inayo eleza baadhi ya watu wanapo kuwa na vitendo vya kingono zaidi ya udhibiti wao. Walakini, hakuna utambuzi wa ugonjwa huu rasmi.

Hii ni hamu ya kufanya matendo ya kingono ili kutatua ama kuhisi njia sawa na waraibu wa vileo.

Baadhi ya ishara maarufu za hamu kubwa ya ngono

 • Kujifurahisha kingono zaidi
 • Kuwa na uhusiano zaidi ya mmoja na wachumba wengi wa kingono
 • Kutumia picha na video za watu wakiwa uchi
 • Kufanya ngono isiyo salama
 • Kufanya ngono kupitia kwa mitandao
 • Kufanya umalaya

Baadhi ya tabia za mraibu wa tendo la ndoa ni kama vile:

 • Kushindwa kudhibiti hamu ya kufanya tendo la ndoa na kuheshimu mipaka ya wengine wanao husika katika kitendo hicho
 • Kuto jihusisha na watu wasio mtosheleza katika tendo la ndoa
 • Hamu zaidi ya kuwavutia wengine, kuwa katika mapenzi, kuanza uhusiano mpya wa kimapenzi na kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja
 • Hisia za kuaibika
 • Kujihusisha katika vitendo vya kingono kwa muda zaidi na inavyo kusudiwa
 • Majaribio mengi ya kukoma, kuwacha ama kupunguza
 • Kutumia wakati mwingi akitafuta ngono, akiwa kwa kitendo ama kupona kutokana na kipindi cha ngono

hamu kubwa ya ngono

Matibabu

Mashirika ya kujisaidia (self-help), kama vile Sexaholics Anonymous, Sexual Compulsives Anonymous, wana programu za kumsaidia mraibu kudhibiti hali yake.

Wanandoa kushauriwa. Huku kuna manufaa mengi kwa mraibu na mchumba wake. Kuna saidia kuboresha mazungumzo yako, kuaminiana na kuwa na matendo yenye afya ya kingono kati ya wachumba.

Matibabu ya tabia za kiakili yana mbinu zinazo msaidia mraibu kubadili tabia zao. Na atapata maarifa ya kumsaidia kuto rejelea tabia hatari za kingono.

Dawa ni mojawapo ya tiba ambazo zime dhihirishwa kuwasaidia watu wanao tatizika na uraibu wa matendo ya kingono. Ni muhimu sana kwa waraibu kuhakikisha kuwa wana kundi la wanafamilia na marafiki zao wanao wasaidia katika safari yao ya uponaji. Kufanya hivi kuna ongeza nafasi zao kupona kwa kasi kuokana na uraibu huo.

Kumbukumbu: Medical News Today

Soma Pia:Wanandoa Wanapaswa Kufanya Ngono Mara Ngapi Kwa Wiki?

Written by

Risper Nyakio