Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Na Matibabu Yake

Watu walio na matatizo katika uhusiano wao wa kimapenzi watapata kuwa ni vigumu kwao kuwa katika hali ya kutamani kufanya mapenzi.
Sio jambo geni kwa wanandoa kushuhudia punguko katika hamu yao ya kufanya mapenzi. Ni jambo linalo fanyika mara kwa mara. Ila linapo zidi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako litatuliwe.
Vyanzo vya kifizikia vya hamu ya chini ya kufanya mapenzi
- Kufilisika kimawazo
- Kuwa na shaka
- Matatizo ya uhusiano
- Kufilisika kimawazo
Kulingana na Healthline.com, kufilisika kimawazo kunaweza fanyika kufuatia kuto kuwa sawa kwa kemikali kwenye ubongo wa mtu. Kwa sababu hamu ya ngono ina dhibitiwa na kemikali kwenye akili, kufilisika kimawzo kunaweza kuwa na athari hasi kwa kemikali hizi na kusababisha utendaji kazi wa kingono usio dhabiti. Pia, mtu aliye filisika kimawazo hana hamu ya kufanya mambo ya kumfurahisha, ikiwemo tendo la ndoa.
2. Kuwa na shaka
Kuwa na shaka nyingi na kukosa hamu ya tendo la ndoa huandamana. Hii ni kwa sababu kuwa na shaka huathiri furaha ya mtu na pia matamanio ya kufanya mapenzi.
3. Matatizo ya uhusiano
Watu walio na matatizo katika uhusiano wao wa kimapenzi watapata kuwa ni vigumu kwao kuwa katika hali ya kutamani kufanya mapenzi. Ikiwa kuna kutoka nje kunako husika ama kumdhulumu mchumba wako, kukosa kuaminiana kunaweza kuwa na athari hasi kwa uhusiano wenu.
Matibabu ya hamu ya chini ya kufanya mapenzi
Kuchechemua hamu yako ya kufanya mapenzi kuna wezekana unapo chukua wakati kuangazia chanzo cha tatizo hilo.
Hivi ndivyo unavyo weza kurekebisha tatizo hilo
- Furahia tendo kabla kufanya mapenzi
Hakikisha unachukua muda kumbusu na kumpapasa mwenzi wako na wakufanyie hivyo pia. Huku kuta kubalisha mwili wako kuwa tayari kwa tendo la ndoa.
- Kubadili mambo chumbani cha kulala
Kubadili mambo chumbani cha kulala ni muhimu ikiwa unaona kuwa ngono yenu inakosa ladha. Huenda ikawa vigumu kutoka kwa mambo mliyo yazoea hapo awali, lakini ni muhimu kufanya mabadiliko ikiwa ungependa hali yenu ibadilike.
- Zungumza kuhusu ngono
Kuzungumza kuhusu jambo hilo linaweza saidia sana katika kuongeza hamu yako ya kufanya. Zungumza na mchumba wako kuhusu uwoga wako, unayo tarajia na mabadiliko ambayo ungependa kuona.
- Fanya mazoezi
Mazoezi hayana faida kwa mwili wako tu, mbali yana saidia kukuweka katika hali ya kutamani kufanya mapenzi. Mwili wako unaachilia endorphins ambazo ni homoni za furaha, unapo fanya mazoezi.
- Zungumza na daktari wako
Ikiwa unachukua dawa zinazo athiri libido yako, unapaswa kumjulisha daktari wako. Huenda kukawa na uwezekano wa kuzibadilisha ili utumie dawa zisizo athiri hamu yako ya ngono.
Vyanzo: Cosmopolitan
Soma Pia: Wanandoa Wanapaswa Kufanya Ngono Mara Ngapi Kwa Wiki?