Ni kawaida mtu kuhisi kuwa hana hamu ya mapenzi baadhi ya wakati. Ila, ni jambo la kutia wasiwasi hamu ya kufanya mapenzi inapoisha. Kukosa hamu ya kufanya mapenzi huwa na athari kwa uhusiano wako wa kimapenzi. Kwa hivyo ni vyema kwa wanandoa kutatua suala la hamu ya chini ya mapenzi mapema iwezekanavyo.
Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikawafanya wanandoa kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Sababu zinazo wafanya wanandoa kukosa hamu ya ngono

Mawazo tele
Mambo mbalimbali yanayo fanyika maishani huenda yaka yasomba mawazo ya mtu na kumaliza nishati yake. Baada ya siku kuisha, hatakuwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Kufikisha umri wa ugumba
Mabadiliko mengi hufanyika mwilini mwa mwanamke anapotimiza umri wake wa ugumba. Kupunguka ama kuisha kwa vichocheo vya estrogen, testosterone na progesterone humfanya mwanamke kukosa hamu ya ngono. Ni vigumu kuwa tayari kwa tendo la ndoa hili linapofanyika.
Ujauzito
Mimba huwa tofauti kwa kila mwanamke. Kuna baadhi ya wanawake ambao hamu ya kufanya tendo la ndoa huisha wanapokuwa na mimba. Mabadiliko katika viwango vya homoni mwilini wakati wa mimba huathiri hili. Na mwanamke hana uwezo wa kubadili jambo hili.
Kupanga uzazi
Mbinu za kupanga uzazi hasa zilizo na vichocheo kama implant, tembe, IUD yenye homoni, huathiri viwango vya vichocheo mwilini. Mwanamke ako katika hatari ya kukosa hamu ya kufanya ngono anapokuwa akitumia mojawapo ya njia hizi kupanga uzazi.

Matibabu
Kuna baadhi ya dawa ambazo huwa na kukosa hamu ya kufanya mapenzi kama athari hasi baada ya matumizi. Ni kawaida kwa nambari kubwa ya madawa hasa za shinikizo la damu.
Matatizo kwenye ndoa
Watu walio na matatizo kwenye ndoa zao huipata ikiwa vigumu kujihusisha katika tendo la ndoa. Ikiwa mchumba ametoka nje ya ndoa, anamchapa ama kutomlinda mwenzake ipasavyo, imani kwenye ndoa hudidimia na inakuwa vigumu kwa wapenzi hawa kuaminiana. Jambo linalo athiri hamu ya kufanya mapenzi.
Kufilisika kimawazo
Kutokuwa sawa kwa kemikali akilini mwa mtu husababisha hali ya kufilisika kimawazo. Hamu ya chini ya mapenzi huathiriwa na kemikali akilini, kufilisika kimawazo huenda kukaathiri viwango vya kemikali hizi na kuathiri hamu na utendaji wa tendo la ndoa. Ni vyema kwa mtu anaye sombwa na mawazo kupata matibabu mapema iwezekanavyo.
Soma Pia: Kufanya Mapenzi Katika Mimba Ni Salama Kwa Mtoto? Maswali Kuhusu Ngono Katika Mimba