Mabadiliko katika hamu ya kufanya mapenzi na kuwa na hamu ya juu ya ngono mara kwa mara ni jambo la kawaida. Ikiwa afya yako iko sawa na hamu ya kufanya mapenzi haiathiri maisha yako ya kawaida, hakuna tatizo.
Hamu ya kufanya mapenzi huwa tofauti kwa kila mtu. Hakuna kiwango fulani kinachotumika kuhesabu usawa wa hamu ya ngono.
Hamu ya juu ya ngono sio chanzo cha shaka iwapo haiathiri maisha yako ya kawaida, kazi yako, kuathiri afya yako ya kiakili ama kuathiri uhusiano wako wa kimapenzi.
Vyanzo

Hamu ya ngono huathiriwa na sababu kama vile:
- Viwango vya nishati
- Hali ya afya kimwili
- Hali ya afya ya kiakili
- Umri
- Hali ya uhusiano wa kimapenzi
- Hali ya muingiliano wa kijamii
- Matumizi ya dawa za matibabu
- Matumizi ya pombe
- Matumizi ya dawa za kulevya
Afya ya kiakili
Kusombwa na mawazo kunaweza kuathiri hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kuwa na mawazo mengi hupunguza hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya watu hufanya mapenzi ili kupunguza mawazo.
Umri na homoni
Mabadiliko ya homoni mwilini huchangia pakubwa katika hamu ya kufanya mapenzi. Kwa vijana, homoni huwa juu na kuwafanya kuwa na hamu iliyoongezeka ya kufanya mapenzi. Huku kwa watu wazee, homoni huwa chache na kupunguza hamu ya kufanya mapenzi.

Afya ya kifizikia na viwango vya nishati
Watu walio na afya bora ya kifizikia, wanaofanya mazoezi mara kwa mara na wako fit huwa na hamu zaidi ya kufanya tendo la ndoa. Na hata wanapofanya kitendo hiki, wanakifurahia zaidi.
Uhusiano
Kulingana na utafiti, wachumba walio katika uhusiano bora na wenye furaha huwa na hamu zaidi ya tendo la ndoa. Huku wachumba walio na vita na vurugu katika mahusiano yao huwa na hamu ya chini ya tendo la ndoa. Ili kuboresha maisha yako ya kingono, ni muhimu kwao kusuluhisha matatizo waliyo nayo.
Matumizi ya dawa za kulevya
Utumiaji wa dawa za kulevya, sigara na pombe huenda uka ongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa muda mfupi. Ila matumizi ya vitu hivi kwa muda mrefu ama kila mara ili kupata hamu ya kufanya mapenzi kuna athari hasi kwa afya.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Haya Yanafanyika Baada Ya Kufanya Ngono Kila Siku Kwa Mwaka Mzima