Nyege ama ashiki ni hamu ya mtu ya kufanya ngono. Ashiki ya chini ni pale ambapo mtu anakosa hamu ya vitendo vyovyote vinavyohusiana na ngono huku hamu ya juu ya ngono ni ongezeko katika hamu ya kujihusisha katika vitendo vya ngono.
Vyanzo vya hamu ya juu ya kufanya ngono

Mazoezi. Kulingana na utafiti, watu wanaofanya mazoezi ya kifizikia huwa na hamu za juu za ngono.
Testosterone. Utafiti unahusisha viwango vya juu vya juu vya testosterone katika wanaume na kuwa na hamu ya juu ya ngono.
Matumizi ya dawa. Kuna baadhi ya dawa kama cocaine zinazosababisha ongezeko katika hamu ya tendo la ndoa.
Vyanzo vya hamu ya chini ya ngono
Afya ya kiakili
Kulingana na utafiti, wanaume na wanawake walio na matatizo ya kiakili, kusombwa na mawazo, mawazo mengi ama kufilisika kimawazo (depression) huwa na nafasi zaidi ya kuwa na maisha hafifu ya kingono. Na kusababisha punguko katika hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Magonjwa sugu
Hali sugu za kiafya kama kisukari na ugonjwa wa moyo zinaweza kuathiri maisha ya kingono na kupunguza hamu ya kujihusisha katika kitendo kile.
Umri
Hamu ya kufanya mapenzi hubadilika kadri umri unavyoongezeka. Kulingana na utafiti, ashiki hushuka watu wanapotimiza miaka 60.
Ujauzito
Hamu ya ngono katika wanawake wajawazito hubadilika katika kila muhula. Kuna baadhi ya wanawake wanaokosa hamu ya kufanya mapenzi kabisa wanapokuwa na mimba.
Dawa za matibabu
Baadhi ya dawa zinaweza kuathiri hamu ya kufanya mapenzi. Kama vile mbinu za uzazi wa mpango wa kike kama sindano ama implant. Dawa za kupunguza mawazo mengi na chemotherapy.
Jinsi ya kuongeza hamu ya kufanya mapenzi

Lala muda zaidi
Utafiti ulibaini kuwa kulala kwa muda mrefu kwa wanawake kulisababisha hamu ya juu ya kufanya mapenzi.
Kufanya mazoezi
Kufanya mazoezi na yoga kumethibitishwa kusaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.
Kutumia aphrodisiacs
Vitu kama strawberries, chocolate na yohimbine ni aphrodisiacs zinazosaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.
Hamu ya kufanya ngono hutofautiana kati ya kila mtu. Kuna sababu tofauti zinazosababisha kukosa hamu ya ngono ama ongezeko lake. Sababu kama umri, homoni, hali ya afya, kufanya mazoezi na dawa za matibabu. Njia za kuongeza hamu ya tendo la ndoa ni kama vile kufanya mazoezi, kulala vya kutosha na kuzungumza na mtaalum. Iwapo una shaka kuhusu maisha yako ya kingono, ni vyema kuwasiliana na mtaalum.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vidokezo Vya Kingono: Mambo Ya Kutofanya Chumbani Cha Kulala!