Jioni ya Jumanne, Rita Dominic, mwigizaji mashuhuri aliyeshinda tuzo nyingi kwa kuwa nyota wa sinema za Nollywood, alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Fidelis Anosike. Harusi ya Rita Dominic iliyokuwa ya kufana imekuwa vinywani vya watu kwa muda sasa ilifanyika katika Aboh, Mbaise, Imo state, katika uwanja wa babake Rita, marehemu Eze Marcellenus J. O Waturuocha. Aliyekuwa kiongozi cha jamii.
Picha: Rita Dominic Instagram
Kutokana na harusi hii ilivyokuwa, bila shaka mwanadada huyu anatoka kwa familia ya kifahari. Katika picha na video zilizoibuka za siku hii kuu kwao, baadhi ya waigizaji mashuhuri wa sinema za Afrosinema walijumuika na wanandoa kusherehekea siku hii. Miongoni mwao ni kama vile Ini Edo, Uche Jomo, Chidi Mokeme, Lily Afegbai na kadhalika.
Picha: Ini Edo Instagram
Rita Dominic alifunga pingu za maisha na Fidelis Anosike ambaye ni mwenyekiti, mkurugenzi wa bodi ya Kundi la Folio na mwenye Daily Times Nigeria. Ambayo ni mojawapo ya magazeti ya kwanza huko Nigeria.
Picha: Reeldeel22 Instagram
Wawili hawa walitangaza kuwa katika uchumba tarehe 5 mwezi wa Aprili baada ya kuweka urafiki wao siri kwa muda.
Picha: Instagram
Rita Dominic ni mtu mashuhuri Nigeria, anafahamika kwa talanta yake ya kuigiza. Ni mojawapo ya waigizaji walioanzisha Nollywood na ameigiza katika sinema nyingi katika Afrika kote. Licha ya kuwa na miaka arobaini na sita, angali anapendeza kwa kweli.
Huku wafuasi, jamaa na marafiki wakiendelea kumpongeza kwa hatua hii ya maisha, kulikuwa na maswali kwanini rafiki yake na mwigizaji mwenza Genevive Nnaji hakujumuika na wengine katika harusi ya rita dominic.
Soma Pia: Hongera! Baada Ya Kungoja Miaka 10, Mwimbaji Evelyn Wanjiru Ana Mimba