Hatari Katika Ujauzito: Dalili Za Kukutia Kiwewe Katika Mimba

Hatari Katika Ujauzito: Dalili Za Kukutia Kiwewe Katika Mimba

Hali hii inafahamika kama oedema ambapo mwanamke anafura kwenye mikono na miguu. Mara nyingi hali hii husababishwa na kushinikiza uzito kwenye miguu.

Ni kawaida kwa mama mjamzito kusoma na kuzungumza na wanawake wengine kuhusu mimba. Ili apate maarifa mengi kuhusu kipindi hiki na mambo anayo stahili kutarajia. Ukweli ni kuwa, haijalishi idadi ya vitabu utakavyo soma na ushauri utakao sikia, huenda ukakumbana na dalili mpya ambazo hakuna mtu aliye zitaja. Tazama dalili hizi zinazo ashiria hatari katika ujauzito.

Dalili Za Hatari Katika Ujauzito

Hatari Katika Ujauzito: Dalili Za Kukutia Kiwewe Katika Mimba

  1. Kuumwa na tumbo ya kati

Kuhisi maumivu makali katika tumbo yako ya kati kukiambatana na kichefu chefu huenda kuka ashiria mojawapo kati ya matatizo haya ya kiafya:

  • kuvimba kwa sana
  • Kuwa na tatizo la kiungulia
  • Kuchafuka kwa tumbo

Kwa wanawake walio zidisha miezi mitatu ya mimba, huenda ikawa uchungu huu una sababishwa na shinikizo kutokana na tumbo inayo zidi kukua. Ni vyema kuwasiliana na daktari wako ili ufanyiwe vipimo vinavyo faa.

2. Kuumwa na tumbo la chini

Kuhisi uchungu mwingi kwenye sehemu ya chini ya tumbo yako ni dalili hatari na unastahili kufanyiwa vipimo bila kusita. Uchungu huu huenda ukawa ni dalili ya matatizo haya:

  • Ujauzito wa ectopic - mimba kukua nje ya uterasi ama nje ya mji wa mimba
  • Kuharibika kwa mimba
  • Kuvunja damu ndani kufuatia kuvimba kwa kizazi
  • Matatizo ya placenta (inayo zingira kiinitete)

hatari katika ujauzito

3. Kuvimba kwa miguu na mikono

Hali hii inafahamika kama oedema ambapo mwanamke anafura kwenye mikono na miguu. Mara nyingi hali hii husababishwa na kushinikiza uzito kwenye miguu. Na sio jambo la kutia shaka. Ila pale ambapo umefura kwa kasi na baada ya kipindi kifupi, huenda mama akawa na pre-eclampsia.

4. Kuvuja damu

Katika mwezi wa kwanza wa ujauzito, mama huvuja kiasi kidogo cha damu. Ila damu hii inapo toka kwa matone, ni dalili ya kumtia mama kiwewe. Kutoa kiasi kingi cha damu pamoja na kuumwa sana na tumbo huenda ikawa ni ishara kuwa mimba ina haribika. Usi site kuwasiliana na daktari wako kuhusu jambo hili.

5. Uchungu mwingi wa kichwa

Kuhisi uchungu mwingi wa kichwa kwa muda mrefu usio koma huenda ika ashiria kuwa una tatizo la kiafya. Huenda maumivu haya yaka ashiria pre-eclampsia ama shinikizo linalo tokana na mimba.

Soma Pia: Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Written by

Risper Nyakio