Kupata mimba baada ya kutimiza umri wa miaka 35 kunawezekana. Wanawake wanaopata mimba na kujifungua baada ya umri wa miaka 35 bila shaka wanajifungua watoto wenye afya. Kushika mimba ukiwa na miaka 35 na zaidi kunafahamika kama mimba ya geriatric kwa kimombo. Ni jukumu la mama kutunza afya yake na kuchukua hatua zote awezavyo kuboresha afya yake na ya mtoto. Kushika mimba baada ya miaka 35 kuna hatari zake kwa wote, mama na mtoto, tazama.
Hatari za kushika mimba baada ya miaka 35

- Shinikizo la juu la damu
- Kujifungua kabla ya wakati
- Kujifungua mtoto mwenye uzani wa chini
- Kujifungua mtoto aliye fariki
- Kupoteza mimba
Manufaa ya kutunga mimba baada ya miaka 35
Mwanamke huwa amepata fursa tosha ya kujipanga maishani mwake, kifedha na kimasomo. Mama ana uwezo wa kukimu mahitaji ya mtoto bila kutatizika.
Watoto wanao zaliwa kwa wanawake wenye umri zaidi wamedhibitishwa kuwa na furaha zaidi, na kupata elimu bora.
Mwanamke anaye jifungua katika umri huu, huwa amefanya uamuzi kuwa hili ndilo jambo ambalo angependa kufanya. Pia huwa amepita hatua za kujivinjari maishani na ako tayari kuwa mzazi.
Jinsi ya kuboresha nafasi za kujifungua mtoto mwenye afya
Ni muhimu kwa kila mzazi kuchukua hatua kuhakikisha kuwa ana afya katika safari yake ya mimba. Kufanya hivi kuna ongeza nafasi zake za kujifungua mtoto mwenye afya bora. Tazama baadhi ya mambo ambayo wanandoa wanaweza fanya ili kupata mtoto mwenye afya.
Kumwona daktari

Mwanamke anastahili kufanyiwa vipimo muda kabla ya kutunga mimba. Kuhakikisha kuwa ana afya bora kutunga mimba na kudhibitisha iwapo ako tayari kihisia kupata mtoto. Baada ya vipimo hivi, daktari atamshauri mwanamke anacho paswa kufanya na tembe za vitamini za kuchukua kabla ya kupata mimba.
Kula lishe bora
Lishe ya mama inapaswa kuwa vyakula vyenye afya. Inasaidia mtoto kukua ipasavyo, kuepuka magonjwa na kuwa na afya njema hata baada ya kuzaliwa. Hakikisha unachukua vitamini za kabla ya kujifungua kama ulivyo shauriwa na daktari wako.
Kwa wanawake walio na matatizo ya kiafya kama kisukari, hakikisha kuwa unawasiliana na daktari wako na kuchukua dawa zako ipasavyo.
Soma Pia:Je, Mwanamke Anaweza Kupata Ujauzito Bila Kujiingiza Katika Tendo La Ndoa?