Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikafanya ujipate ukichukua chajio chako usiku wa maanani. Hasa kwa watu wanaotoka kazi jioni sana mijini, na kukaa kwenye foleni ndefu wakingoja magari ya kuwasafirisha manyumbani mwao. Baada ya haya yote, nafasi kubwa ni kuwa utafika nyumbani usiku sana na kulazimika kula chajio chako usiku wa maanani. Kuna hatari nyingi za kula usiku, hata kama unakula chakula chenye afya.
Mara nyingi baada ya siku ndefu kazini na kufika nyumbani usiku wa maanani, hutakuwa makini na chakula unacho kula. Utatafuta chakula kilicho rahisi kutengeneza ama chakula ulicho nunua kando ya barabara. Ambacho mara nyingi huwa kimetayarishwa kutumia mafuta nyingi.

Kumbuka kuwa ubora wa chakula unacho kila ni muhimu sana. Jaribu uwezavyo kula chakula chenye afya.
Hatari Za Kula Usiku Wa Maanani
- Kuongeza uzani wa mwili

Utafiti mwingi uliofanyika kuhusu miili za binadamu, umedhihirisha kuwa kula usiku wa maanani kuna sababisha ongezeko la uzito wa mwili. Chakula kilicho kuliwa usiku sana huhifadhiwa mwilini kama ufuta na ni vigumu kukichakata chakula hiki inavyofaa. Pia, wakati wa usiku, hakuna kitu unacho fanya, kwa hivyo, nishati kutoka kwa chakula haitumiki, mbali ina hifadhiwa mwilini kama ufuta.
2. Hatari ya kuugua mshtuko wa moyo
Kadri na siku za hapo awali, magonjwa kama mshtuko wa moyo yamekuwa maarufu sana. Kinacho changia sana katika ongezeko la maradhi haya ni aina ya vyakula watu wanavyo amua kula na pia kula usiku sana. Unapo kula usiku sana, viwango vya kolesteroli mwilini huongezeka kwa sababu chakula hicho hakikuchakatwa. Na kuchangia katika shinikizo la damu mwilini mwako kuongezeka.
3. Hatari iliyo ongezeka ya kisukari
Chakula kinacho hifadhiwa mwilini mwako kama ufuta baada ya kuto chakatwa kina ongeza viwango vya homoni ya insulin mwilini. Uwezo wa mwili kutumia insulin uko juu wakati wa mchana ikilinganishwa na usiku. Na insulin isipo tumika mwilini, ina badilishwa kuwa glucose mwilini na kuhifadhi kama sukari. Ni hatari kwa mwili wako.
Hitimisho

Tunaelewa kuwa kazi ni ngumu na haupati wasaa tosha wa kula kabla ya kutoka kazini ama kula mapema baada ya kufika nyumbani. Kuna mbinu nyingi unaweza tumia kuhakikisha kuwa unakula mapema kabla ya kulala. Kama vile kujaribu kula baada ya kazi ama kutayarisha chakula cha wiki moja kisha kukihifadhi kwenye friji yako. Kwa njia hii, hautatumia wakati mwingi kutayarisha chakula chako baada ya kutoka kazini. Pia, utaweza kujidhibiti kununua vyakula vya barabarani.
Kumbuka kuwa una shauriwa kula masaa angalau matatu kabla ya kulala.
Soma Pia: Fahamu Faida Za Kula Mayai Kwenye Lishe Yako