Kulingana na Shirika la Afya Duniani, milioni 73 ya kutoa mimba hufanyika duniani kila mwaka. Sita kati ya mimba 10 huwa haijapangwa na tatu kati ya mimba 10 hutolewa mwishowe. Kutoa mimba bila usaidizi wa kimatibabu humweka mama katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya na kumweka katika hatari za utoaji wa mimba wa kinyumbani.
Ikiwa mwanamke amepata mimba isiyokusudiwa, anashauriwa kutembelea kituo cha afya. Kujaribu kutoa mimba kutumia mbinu za kinyumbani za kutoa mimba punde tu anapoanza kupata dalili za mimba kunamweka katika hatari.
Kutoa mimba kunapofanyika kwenye kituo cha afya na mtaalum, mama huwa salama, ila kufanyia nyumbani bila usaidizi wa daktari kuna athari hasi. Hata hivyo, kutoa mimba nchini Kenya kumepigwa marufuku. Katika visa ambapo maisha ya mama yapo hatarini, utoaji wa mimba unaruhusiwa. Ukosefu wa mbinu za utoaji wa mimba zisizo salama huleta kutengwa kunakohusishwa na utoaji wa mimba na kuwaweka wanawake katika hatari za kifizikia, kihisia na kiakili.
Hatari za utoaji wa mimba wa kinyumbani

- Utoaji wa mimba usiokamilika
Utoaji wa mimba usiokamilika hufanyika pale ambapo tembe za kutoa mimba hazina ufanisi wa kutamatisha utoaji wa mimba. Hili linapofanyika, upasuaji wa dharura unahitajika. Kukosa matibabu ya dharura kuna muweka mwanamke katika hatari ya kupata maambukizi hatari.
2. Matatizo ya afya ya kiakili
Utoaji wa mimba unaofanyika nyumbani bila uangalifu wa mtaalum humuacha mwanamke bila egemezo la kihisia ama kimatibabu. Mara nyingi wanawake wanaopitia hili huripoti kupata matatizo ya afya ya kiakili.
3. Kutatizika kutunga mimba siku za usoni
Utoaji wa mimba ya kinyumbani hasa usio kamilika unaweka mwanamke katika hatari ya kutatizika kushika mimba siku za usoni.

4. Ugonjwa wa pelvic inflammatory disease
Maambukizi ya chlamydia baada ya utoaji wa mimba unaongeza nafasi za mwanamke kupata ugonjwa wa pelvic inflammatory disease kwa asilimia 23. Ugonjwa huu una athari hasi zaidi kama kuongeza uwezekano wa mimba ya ectopic ama kukosa kupata mimba.
5. Kukosa uhusiano na watoto wako siku za usoni
Utoaji wa mimba huwa na athari hasi kihisia kwa mwanamke hasa utaratibu huu usipofanyika upasavyo. Mwanamke aliyepitia haya huenda akatatizika kuwa na uhusiano mzuri wa kihisia na watoto wake katika siku za usoni.
Kabla kufanya uamuzi wowote kuhusu mimba yako, wasiliana na daktari. Ataweza kukupatia ushauri wa kitaalum kuhusu uamuzi unaotaka kufanya.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Maswali 7 Maarufu Kuhusu Ngono Katika Mimba