Video Za Ngono Ya Watoto Kwenye WhatsApp

Video Za Ngono Ya Watoto Kwenye WhatsApp

Without sufficient human moderators, disturbing content is freely shared on WhatsApp’s groups.

Wazazi, jua na uchukue tahadhari za hatari za Whatsapp iwapo unawakubalisha watoto wako kuitumia. Mtandao wa kijamii wa kutuma jumbe unao aminika duniani kote umekuwa mahali pa watu kutuma picha na video zisizo kubalika za ngono ya watoto.

Kulingana na Financial Times, watafiti walipata maelfu ya vikundi vya WhatsApp ambazo zina picha na video za udhalilishaji kingono wa watoto zikitumwa kwa wazi.

Watafiti waliangalia apps za mtumiaji wa tatu zilizo shauri vikundi vya Whatsapp kufuatia mapendekezi. Hapa, links za vikundi vya mazungumzo zinazo pitisha picha za udhalilishaji wa watoto zinapatikana na kumbukumbu za picha mbaya za nambari za kipekee.

Watafiti hawa walisema kuwa walipitisha ujumbe huu kwa Facebook (Facebook wanamiliki WhatsApp). Hata kwa hayo, nyingi kati ya vikundi hivi bado zi ‘hai’.

“Haya ni maafa: aina hii ya jumbe mara moja zilipatikana tu kwenye Darknet (sehemu ya mtandao ambao hauko huru kuonekana na watu wote). Kwa sasa iko kwenye WhatsApp,” alisema moja wapo wa watafiti hao kwenye ripoti hiyo.

Hatari za WhatsApp kwa watoto

hatari za whatsapp

Chanzo cha picha: Pixabay

WhatsApp sio mtandao wa kipekee wa kijamii unao kuwa na tatizo la kuepusha usambazi wa jumbe za video za ngono kutumia mtandao huo. Chumba cha hifadhi cha Apple App kilitoa Tumbler kwa mwezi mmoja Novemba ya mwaka uliopita kwa sababu ya video za ngono ya watoto.

Kwa WhatsApp, ni encryption ya mwisho-kwa-mwisho kulinda watumiaji na siri zaidi. Walakini, huku kuna maana kuwa wanao fuatilia sheria hawana uwezo wa kuona jumbe zinazo kisiwa kuwa dhidi ya sheria ama zisizo kubalika.

Kuna maana pia kwamba Facebook haiwezi tumia vifaa sawa vya ugunduzi kwenye kurasa yao kuangalia WhatsApp. Cha zaidi WhatsApp ina wafanyakazi 3000 kwa kufuatilia watumizi bilioni 1.5 duniani kote. Kulinganishwa, Facebook ina maelfu ya watu wa kufuatilia watumiaji wa kurasa lao.

Dhidi ya sheria

Video za ngono ya watoto ina dhibitiwa na sheria mbili huko South Africa: section 24B Films and Publications Act (Act 65 of 1996) na section 20 Criminal Law (Sexual Offences and Related Matters) Amendment Act (Act 32 of 2007).

Ni kosa kuweka jumbe mbaya kwenye mitandao ya kijamii ama kuuza video za ngono zozote.

Maana ya hii ni kuweka watoto salama kutokana na watu wenye hiari mbaya na kuwanyanyasa.

Ku ripoti video za ngono ya watoto kwenye Whatsapp

WhatsApp inasema kuwa watakataza mtu kutumia mtandao huu iwapo wataamini kuwa anapitisha ujumbe usio kubalika kisheria, za picha mbaya ama kuhimiza vitendo visvyo kubalika.

hatari za whatsapp

Hapa kuna vidokezo:

  • Unaweza tuma ripoti kwa WhatsApp kutoka ndani ya mtandao huo.
  • Tafadhali toa ujumbe mwingi kadri uwezavyo.
  • Inapo hitajika, piga picha ya ujumbe huo na uripoti pamoja na nambari ya mtu huo.
  • Ripoti mtu ama kikundi kutoka kwa ujumbe wa nambari hiyo kwa kufuata vidokezo hivi:
  1. Fungua ujumbe huo.
  2. Bonyeza kwenye ujumbe wa nambari yake ama wa kikundi hicho.
  3. Shuka kwenye sehemu ya chini kisha ubonyeze ‘ripoti kikundi’.

Soma pia: Sex addiction symptoms to watch out for

Vyanzo:  Businessinsider , Unicef na WhatsApp

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio