Sindano ya depo provera ni mojawapo ya njia maarufu za kupanga uzazi. Inamkinga mwanamke dhidi ya kupata mimba kwa kipindi cha miezi mitatu. Mbinu hii ilivumbuliwa mwaka wa 1996 na kutumika katika nchi tofauti, ila huko Kanada, ilipigwa marufuku kwa maelezo kuwa ina athari hasi kwa wanawake. Tuna angazia hedhi baada ya kuacha sindano na athari hasi za depo provera kwa wanawake.
Jinsi sindano inavyo athiri hedhi ya mwanamke

Sindano ya uzazi wa mpango ya depo provera ina fahamika kwa kuwa na athari hasi kwa kipindi cha hedhi cha mwanamke. Kama vile kufanya mwanamke atoe kiwango kikubwa cha damu katika hedhi yake. Huenda kukamfanya mwanamke augue hali ya anaemia ambayo ni kupungukiwa kwa damu mwilini.
Baadhi ya wanawake hukosa kupata vipindi vya hedhi kwa muda mrefu, huku wengine wakivuja kiwango kidogo cha damu kisicho jaza pedi.
Madhara ya kutumia sindano ya kupanga uzazi ya depo provera
- Kubadilisha mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baadhi ya wakati, mwanamke huenda akatoa damu nyingi kuliko kawaida, kutoa damu kidogo isiyo jaza pedi, kuvuja damu baada ya kipindi cha hedhi
- Kuongeza uzito wa mwili kwa kasi zaidi
- Kuumwa na magoti
- Kupunguza uzito wa mwili kwa kasi
- Wanawake walio na umri chini ya miaka 35 wako katika hatari ya kuugua saratani ya matiti
- Kuziba kwa mishiba ya damu ama hewa
- Kupasuka kwa mishipa ya damu kufuatia kuganda kwa damu
- Mwanamke ana hatari ya kuugua saratani ya kizazi
- Kujaa maji kwenye mishipa ya mwili kwa kimombo water retention
- Kuhisi kichefu chefu
Mwanamke anapo tumia sindano ya kupanga uzazi na kufanya mapenzi na mwanamme aliye na wapenzi wengi, ako katika hatari ya kuugua magonjwa ya zinaa. Kama vile clamdiya, herpes ama gonorrhea.

Vichocheo vilivyo kwenye sindano hizi huenda zikamfanya mwanamke akae kwa muda mrefu kabla ya kupata mimba. Na hata anapokoma kuzitumia, atabaki kwa muda kabla ya homoni hizo kutoka mwilini ili aweza kutunga mimba kwa urahisi.
Mwanamke anaye tunga mimba angali anatumia sindano ya depo provera ako katika hatari kubwa ya kujifungua mtoto njiti. Huku wanawake wengine wakikaa muda mrefu kabla ya kupata hedhi baada ya kuacha sindano ya kupanga uzazi ya depo provera.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Je, Tawi Kali Linaweza Kutoa Mimba? Mambo Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Mmea Huu