Hedhi baada ya mimba kutoka ni jambo la kawaida baada ya mwanamke kuavya mimba. Damu hii inafanana na damu ya hedhi, ila kuna tofauti. Kuna baadhi ya wanawake wasio vuja damu baada ya kutoa ama kuharibika kwa mimba. Kwa walio katika kundi hili, damu hutoka wanapo shuhudia kipindi chao cha kwanza cha hedhi.
Kipindi cha kuvuja damu baada ya kutoa mimba ama kuharibika kwa mimba

Mwanamke anaweza kuvuja damu kwa kipindi cha wiki moja ama mbili baada ya kutoa mimba ama kupoteza mimba. Utatumia pedi nyingi kwa hivyo ni vyema kujihami ipasavyo. Kuna baadhi ya mabinti ambao huenda waka shuhudia kutokwa na damu siku tatu ama nne kisha kuacha. Na kuwa na kipindi kizito cha hedhi baada ya hapo.
Damu ya kuavya mimba
Kuna tofauti kati ya damu ya hedhi na damu ya kuavya mimba. Hata ingawa zote huwa nzito katika siku za kwanza. Rangi hutofautiana. Huku rangi ya damu ya hedhi ikiwa nyekundu iliyo kolea, damu ya kuavya mimba huwa nyekundu inayo karibia hudhurungi. Damu ya mimba iliyo haribika huwa nzito zaidi na inayo jaza pedi zaidi na kwa kasi ikilinganishwa na damu ya hedhi.
Hedhi baada ya mimba kutoka

Vipindi vya hedhi huweza kurudi kawaida baada ya mwezi mmoja. Kipindi hiki hutofautiana kati ya wanawake. Kwa baadhi ya wanawake, baada ya mimba kutoka, homoni ya mimba, hCG hupungua na ishara za mimba kupotea. Katika kisa hiki, vipindi vya hedhi vitarudi kawaida baada ya mwezi mmoja. Kwa wanawake ambao homoni ya mimba itazidi kuwa mwilini, huenda wakakosa kupata vipindi vya hedhi kwa muda zaidi. Kwani mwili bado una dhihirisha dalili za kuwepo kwa mimba.
Kipindi cha hedhi cha kwanza baada ya kuharibika kwa mimba yako huenda pia kikawa kizito zaidi ya ilivyo kawaida. Pia kitachukua siku zaidi. Kwenye damu hiyo, utagundua kuna vidonge vidonge. Utagundua kuwa una hisi tumbo limejaa gesi, uchovu mwingi, kuumwa na kichwa na mhemko wa hisia.
Soma Pia:Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi