Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

3 min read
Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

Baadhi ya wanawake wanaweza shuhudia kuvuja damu kwa uke wakiwa na mimba. Lakini haiwezekani kuwa na hedhi ukiwa na mimba. Hedhi hufanyika pale tu ambapo mwanamke hana mimba. Kila mwezi, ovulation hufanyika ovari inapo achilia yai lipevushwe na manii. Kuta za uterasi hunenepa ziki ngoja yai lipevushwe baada ya kujipandikiza na kusababisha mimba. Ikiwa yai halita pevushwa, yai na kuta za uterasi zitatolewa kupitia kwa uke kama hedhi.

Kwa hivyo, unaweza pata hedhi ukiwa na mimba? Jibu ni la. Kwa sababu wanawake hawa ovulate ama kuachiliwa yai wakiwa wajawazito. Hawata pata vipindi vyao vya hedhi.

Sababu Kwa Nini Unaweza Pata Hedhi Ukiwa Katika Trimesta Yako Ya Kwanza Ya Mimba

ishara za mapema za mimba

 

Kuna uwezekano wa kuvuja damu ukiwa na mimba. Kuvuja damu huku haku ashirii tatizo la kiafya wakati wote. Lakini ni muhimu kuelewa chanzo chake- na ikiwa unapaswa kuenda hospitalini.

Kutoa damu hufanyika sana katika trimesta ya kwanza ya ujauzito ikilinganishwa na ya pili ama ya tatu. Watafiti wana pendekeza kuwa angalau asilimia 25 hadi 30 za wanawake wajawazito hushuhudia kutoa damu katika hatua moja ama nyingine katika trimesta ya kwanza. Kuna nambari ya sababu za kutoa damu huku:

  • Kutoa damu ya kupandikiza (implantation bleeding)

Ni kuvuja damu nyepesi kunako fanyika siku 10 ama 12 baada ya kutunga mimba. Huu ni karibu na wakati ambapo unatarajia kipindi chako cha hedhi. Wanawake wengi katika hatua hii bado hawaja fanya kipimo cha mimba, kwa hivyo ni rahisi kudhani kuwa hiki ni kipindi chao cha hedhi cha kawaida. Damu hii ni nyepesi ikilinganishwa na hedhi, walakini, huwa ya siku chache tu. Hufanyika kwa sababu ya kupandikiza kwa yai lililo pevuka kwenye kuta za uterasi.

  • Mabadiliko ya kizazi

Kuvuja damu hufanyika wakati mfupi baada ya kupata mimba kwa sababu ya mabadiliko kwenye kizazi. Hasa baada ya kufanya mapenzi. Kama hauna maambukizi, hakuna haja ya kuwa na shaka.

Sababu zingine

Kuvuja damu nyingi inayo karibiana na hedhi katika trimesta ya kwanza ya mimba kunaweza ishiria kitu sugu zaidi, kama vile:

  • Mimba ya ectopic
  • Maambukizi
  • Mimba ya molar
  • Kutoa damu kati ya placenta na kuta ya uterasi

Hivi vyote ni visa vya dharura na ni muhimu kumtembelea daktari wako bila kukawia. Mara nyingi vina andamana na ishara zingine mbali na kuvuja damu.

Kuvuja damu baadaye katika mimba: Kwa nini kunatendeka

Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

Kuvuja damu katika trimesta ya pili na ya tatu kunawezekana, hata kama sio kawaida, na kunaweza kuwa ishara kuwa kuna jambo linalo endelea. Ukishuhudia kuvuja damu baadaye katika mimba, ni muhimu kumwona daktari.

  • Kufanya mapenzi
  • Uchungu wa uzazi usio komaa
  • Placenta previa
  • Kuathiriwa kwa placenta
  • Kupasuka kwa uterasi

Kuvuja damu katika trimesta ya pili na tatu pia kunaweza sababisha kuharibika kwa mimba ama kuwa ishara ya vasa previa.

Unapo paswa kumwona daktari

Kwa sababu huwezi pata hedhi ukiwa na mimba, ni muhimu kuwa makini unapo ona ishara zozote za kuvuja damu katika kipindi hiki. Wakati ambapo kuvuja damu kiasi katika trimesta ya kwanza mara nyingi hakuna kitu cha kuwa na wasiwasi kuhusu, kuvuja damu kunako andamana na ishara zingine kunaweza ashiria kitu sugu zaidi, na unapaswa kumwona daktari wako bila kukawia. Ishara hizi ni kama vile:

  • Kuumwa na tumbo na kuhisi uchungu
  • Kuhisi kizungu zungu
  • Kuvuja damu nyingi
  • Uchungu mwingi kwenye tumbo ama pelviki

Unapaswa kumtembelea daktari wako ikiwa unatoa damu ya rangi nyekundu inayo ng'aa na ni nyingi na kuchafua kitambaa cha pedi. Uchungu wa pelviki na kuvuja damu kwa uke katika hatua za mapema za ujauzito huenda kuka ashiria mimba ya ectopic. Ukiwa na shaka hii, hakikisha kuwa unaenda hospitalini kasi uwezavyo.

Soma pia:Kutapika Katika Mimba Ni Ishara Kuwa Huenda Mtoto Wako Akawa Mwenye Maarifa

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?
Share:
  • Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

    Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

  • Maambukizi Yanayo Sababisha Mwanake Mwenye Mimba Kuharibika Kwa Mimba

    Maambukizi Yanayo Sababisha Mwanake Mwenye Mimba Kuharibika Kwa Mimba

  • Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

    Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

  • Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

    Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

  • Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

    Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

  • Maambukizi Yanayo Sababisha Mwanake Mwenye Mimba Kuharibika Kwa Mimba

    Maambukizi Yanayo Sababisha Mwanake Mwenye Mimba Kuharibika Kwa Mimba

  • Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

    Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

  • Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

    Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it