Mambo Ambayo Wanawake Wanaogopa Katika Uhusiano

Mambo Ambayo Wanawake Wanaogopa Katika Uhusiano

Kuna sababu nyingi ambazo huchangia uhusiano kuisha. Ni jambo linalo waumiza wachumba wote wawili, hata ingawa mwanamke huumia zaidi kwani ni rahisi kwa mwanamke kupenda.

Baadhi ya wakati, mwanamke hukosa kujihusisha na mwanamme yoyote ama kuingia katika uhusiano naye kufuatia uwoga na hofu za wanawake katika uhusiano. Sio kana kwamba hangependa kupenda ama kupendwa, mbali kuna vitu anavyo hofia kuwa zitatendeka katika uhusiano huo na kumwumiza mtima wake. Huenda ikawa hofu hizi ni kutoka uhusiano alio kuwa nao hapo awali ama mambo aliyo ona yakiwatendekea watu walio karibu naye.

Na sababu hizi kumfanya abaki peke yake bila mchumba. Ni muhimu kwa mwanamke kufahamu mambo yanayo mtia kiwewe na shaka ili apate njia ya kukumbana na hofu hizi. Tazama orodha yetu itakayo kujuza kuhusu mambo ambayo wanawake wengi siku hizi wanaogopa katika ndoa.

Hofu za wanawake katika uhusiano

hofu za wanawake katika uhusiano

  1. Kutoka nje

Kila mtu anaogopa kuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye baada ya wakati ataanza kutoka nje na kutafuta wachumba wengine. Jambo hili linawafanya wanawake wengi kufanya uamuzi wa kubaki peke yao bila kujihusisha katika uhusiano wowote ule. Kutoka nje huwa na athari hasi kwa mwanamke kwa sababu ataanza kujiuliza maswali na kushangaa kama hatoshi ama ikiwa kuna mambo anayo yafanya isivyo faa.

2. Kuwa na mchumba asiye mtosheleza

Wanawake wengi wana hofu ya kuwa na wanaume wasio kimu mahitaji yao ya kihisia, kiakili ama hata kifedha. Hasa ikiwa mwanamke huyu ana uwezo wa kuyakimu mahitaji yake bila matatizo yoyote yale. Pia, kuna hofu ya kuwa na mwanamme ambaye wakati wote anatarajia uende mrama na imani zako ili kumtosheleza.

3. Mwanamme sawa na mchumba wake wa awali

Mabinti huwa na uwoga kuwa wanaume wote ni sawa. Kumaanisha kuwa kama mchumba wako wa hapo awali alikuumiza, huenda utakaye mpata baada yake awe sawa na akufanyie mambo sawa na kukuumiza.

4. Kuto heshimiwa

hofu za wanawake katika uhusiano

Hakuna anaye penda kuto patiwa heshima, hasa katika uhusiano. Unapo ingia kwenye uhusiano na mtu yeyote yule, maono yako ni kuwa mtakuwa pamoja kwa muda mrefu na mapenzi yenu yatadumu. Ila ndoto hizi hukatizwa mmoja wenu anapo anza kuto heshimu mwingine.

5. Kufikiria kuwa yeye sio mrembo vya kutosha

Mabinti wengi hufikiria kuwa wanapaswa kuwa warembo vya kutosha ikiwa mwanamme atabaki nao. Wakati mwingi, ama wakati wote, sio lawama ya mwanamke mwanamme anapo toka nje ya ndoa. Na jambo hili humvunja mwanamke moyo.

6. Uhusiano kuisha baada ya wakati mdogo

Kuna sababu nyingi ambazo huchangia uhusiano kuisha. Ni jambo linalo waumiza wachumba wote wawili, hata ingawa mwanamke huumia zaidi kwani ni rahisi kwa mwanamke kupenda. Wanawake wengi hawaoni haja ya kuwa katika uhusiano kisha ukaisha baada ya siku chache. Na kufanya uamuzi wa kuto penda ama kupendwa.

Soma PiaSababu Kwa Nini Mchumba Wako Atatoka Nje Ya Ndoa Yenu

Written by

Risper Nyakio