Orodha Ya Matibabu Bora Ya Kinyumbani Ya Homa Katika Mtoto Aliyezaliwa

Orodha Ya Matibabu Bora Ya Kinyumbani Ya Homa Katika Mtoto Aliyezaliwa

Mama aliye jifungua anapaswa kuwa na maarifa ya matibabu ya kinyumbani ya homa. Ili afahamu anacho stahili kwa homa huwa maarufu sana katika watoto wachanga.

Kila mama aliye jifungua anapaswa kuwa na matibabu ya nyumbani ya homa katika mtoto aliyezaliwa kwenye nyumba yake. Kukohoa na homa ni kawaida sana kwa watoto wachanga, kwa hivyo haupaswi kuwa na shaka sana mtoto wako anapo pata homa. Homa ya watoto wadogo ni kawaida sana na ni rahisi kutibu. Pia, ni njia nzuri ya kuboresha kinga ya mtoto! Wakati mwingi, maradhi ya mtoto wako sio kwa sababu amekumbana na viini. Watoto mara nyingi hugonjeka kunapo kuwa na mabadiliko ya hali ya anga.

Kinacho Mfanya Mtoto Apate Homa

Ikiwa mtoto wako kwa ghafla anapata homa, unapaswa kuwa mwangalifu kuhusu uchafu kwenye pazia na neti za mbu. Pia, angalia kama kuna harufu geni nyumbani mwako. Mtoto wako huenda akapata homa kwa sababu ya kuwa karibu na watu wazima ama hata watoto wengine. Chochote kinacho sababisha homa hiyo, matibabu ya nyumbani ya homa katika mtoto aliyezaliwa yana paswa kuwa suluhu.

Ishara za homa katika watoto walio zaliwa

kupata mtoto wa kike

Ishara maarufu ni kama vile:

 • Kukohoa
 • Kukosa hamu ya kula
 • Usumbufu mwingi
 • Kuchemua
 • Joto jingi mwilini
 • Matatizo ya kulala

Mambo ya kuepuka mtoto wako anapokuwa na homa

 • Epuka kumpatia mtoto wa umri chini ya mwaka mmoja asali
 • Hakuna wakati ambapo mtoto anapaswa kuwa uchi hata kama ana joto jingi mwilini
 • Dawa dhidi ya bakteria hazitatua homa katika watoto
 • Matibabu ya kikohozi na homa haishauriwi kwa watoto chini ya miaka miwili
 • Hakikisha kuwa mtoto halali kwa tumbo yake

Baadhi ya matibabu ya kinyumbani ya homa katika mtoto aliyezaliwa

Mtoto wako anapo anza kukohoa na kuchemua, mara nyingi ata shuhudia ongezeko la joto mwilini. Usitie shaka. Joto jingi mwilini ni njia ya mwili wa mtoto kukufahamisha kuwa kuna kasoro. Unacho paswa kufanya ni kutumia matibabu haya ya kunyumbani ya homa katika mtoto aliyezaliwa.

1. Tembelea mtaalum wa afya ya watoto

Watoto wachanga huwa nyeti sana, kwa hivyo utahitajika kumpeleka mtoto wako kuona daktari. Hii ndiyo njia pekee ambayo utaweza kuwa hakika kuwa magonjwa sugu kama vile pneumonia. Matibabu ya kinyumbani hayapaswi kumtenga mtoto na daktari wake.

2. Hakikisha kuwa mtoto anapata maji tosha mwilini

napaswa kumwamsha mtoto ale usiku

Katika wakati huu, mtoto analishwa na maziwa ya mama peke yake. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unam nyonyesha mara kwa mara. Ikiwa amepitisha kiwango hicho, mpe vinywaji vingi hasa maji pamoja na maziwa ya mama na formula.

3. Jaribu kusafisha mapua ya mtoto mara nyingi uwezavyo

Unaweza tumia pamba kusafisha mapua ya mtoto ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinacho ziba mapua yake.

4. Inua kichwa cha mtoto kidogo anapo lala

Mojawapo ya matibabu bora ya homa katika watoto wachanga ni kuinua kichwa chake kidogo anapo lala. Unaweza fanya hivi kwa kutumia mto laini ama ukunje kipande cha nguo na utumie kama mto. Tafadhali kumbuka kuto inua kichwa cha mtoto juu sana kwani huenda ukaumiza kichwa chake na kusababisha kuumwa na shingo.

5. Kumsafisha na maji moto

Msafishe mtoto na maji moto asubuhi na jioni. Maji yanapaswa kuwa moto na sio yenye vuguvugu. Lakini kuwa makini usitumie maji yaliyo chemka na kumchoma mtoto.

6. Safisha chumba cha mtoto

Hakikisha kuwa umesafisha chumba cha mtoto. Neti na pazia na uhakikishe madirisha yote yako wazi ili chumba kipate hewa freshi.

7. Mapumziko

Kubalisha mtoto apate mapumziko tosha. Huenda wakawa wana sumbua na watalala kwa muda mfupi kwa sababu hawana starehe. Lakini wanapo maliza kula, mlaze kitandani na ujaribu kumbembeleza alale.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Tumia Vidokezo Hivi Unapokuwa Na Homa

Written by

Risper Nyakio