Masomo Ya Chloroquine Kama Matibabu Ya Homa Ya Corona Yasimamishwa

Masomo Ya Chloroquine Kama Matibabu Ya Homa Ya Corona Yasimamishwa

Kulingana na  New York Times, utafiti mdogo kuhusu chloroquine kwa homa ya corona uliofanyika huko Brazil umesimamishwa na viongozi. Wagonjwa wa majaribio waliochukua kiwango cha juu cha dosi ya chloroquine walipata mpigo wa moyo usio wa kawaida ambao uliongeza hatari yao ya kupata matatizo ya moyo. Chloroquine, inayo husika kwa karibu na hydroxychloroquine, ili kuzwa kama matibabu yanayo wezekana ya homa ya corona na Trump licha ya hofu zilizo zuka kutoka kwa wataalum wa matibabu.

Utafiti wa majaribio wa chloroquine kwa homa ya corona huko Brazil yasimamishwa

chloroquine

Katika mwezi wa tatu, utawala wa Chakula na Dawa ulipatia mahospitali kibali cha dharura ili wapate madawa ya chloroquine na hydroxychloroquine kwa idadi kubwa ili watumie katika majaribio yao ya hospitali. Utafiti huu wa Brazil uliohusisha wagonjwa 81 katika mji wa Manaus, ulidhaminiwa na taifa la Brazil la Amazonas. Utafiti uliwekwa kwenye mtandao kwa makala ya kimatibabu ili uweze kupelelezwa zaidi na wataalum wengine.

Wakati wa utafiti huu, nusu ya waliohusika walipata miligramu 450 za chloroquine mara mbili kila siku kwa siku tano. Na hao wengine wakapata dosi ya miligramu 600 kwa siku 10. Watafiti walianza kugundua heart arrhythmias kwa wagonjwa waliochukua dosi ya juu katika muda wa siku tatu. Wagonjwa 11 walikufa siku ya 6 ya matibabu haya na kulazimisha kuto endeleza kwa dosi ya juu ya majaribio.

chloroquine trial for coronavirus

Baadaye, wataalum wa maradhi hatari walihakikisha kuwa majaribio haya yalikuwa na ushuhuda kuwa chloroquine na hydroxychloroquine, dawa mbili zinazo tumika kutibu malaria, yana athari kwa baadhi ya wagonjwa na hasa hatari kali ya heart arrhymthmia.

Kwa daktari David Juurlink, ambaye ni internist ama na mkuu wa pande ya clinical pharmacology katika Chuo Kikuu cha Toronto, na utafiti haukufeli. Kwake, utafiti ule ulidhihirisha uwezekano wa cardiac arrest kulingana na kiwango cha chloroquine ni muhimu.

hospital

Majiribio mengi ya zahanati ya chloroquine na hydroxychloroquine kwa sasa yana pima dosi za chini kwa muda mfupi kwa wagonjwa wa virusi vya homa ya corona

Soma pia: NAFDAC Orders For Production Of Chloroquine For Treatment Of COVID-19

Chanzo: New York Times

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio