Janga La Homa Ya Corona Lina Athiri Ndoa Na Kuchangia Katika Talaka Nyingi

Janga La Homa Ya Corona Lina Athiri Ndoa Na Kuchangia Katika Talaka Nyingi

Homa ya corona itashindwa na tuizidi siku moja; huenda jambo hili lisitendeke kwa kipindi cha wiki moja ama hata mwezi mmoja.

Na mamia ya watu wakiambukizwa na hata kufa kufuatia homa ya corona, nchi nyingi zimeamurisha lockdown kama njia ya dharura kupambana na janga la corona. Huku kuna maana kuwa watu wamefungwa manyumbani mwao, na hawawezi kutoka hadi pale wanapo endea vitu vya dharura na kubaki kuingiliana na watu wachache sana kwa mara nyingi wana familia wao. Umbali wa mwingiliano umehakikisha watu wana patana na watu wachache sana na kulazimishwa kuingiliana na watu wachache sana. Ila, hakuna shaka kuwa homa ya corona haitu athiri kifizikia tu hadi afya ya kiakili na pia baadhi ya uhusiano wetu. Duniani kote, wataalum wengi wa sheria za familia wanashuhudia ongezeko la matatizo ya kifamilia na homa ya corona na talaka.

Msemo wa, “familiarity breeds contempt” ulio na maana kuwa "kuzoena huleta chuki" umeinuka kwa kiwango kipa na uhusiano wa kindoa ukiteseka sana kufuatia athari za lockdown.

coronavirus and divorce

Katika miaka ya hapo awali, asilimia ya talaka imekuwa juu sana baada ya likizo za krismasi ama likizo zingine baada ya familia kuwa na wakati mwingi pamoja. Baroness Fiona Shackleton, mwanasiasa wa Kizungu na solicitor, aliwashauri wanarika wake huko Westminister kuhusu ongezeko la talaka baada ya kufungiwa ndani kufuatia virusi vya homa ya corona. Hili ni jambo la kuhuzunisha hasa ukiangalia nchi kama Uchina ambapo ripoti za ongezeko la wanandoa wanaotaka kupatiwa talaka. Uchina ilikuwa nchi iliyokuwa na visa vingi zaidi vya corona na ambapo janga hili lilianza na watu walikuwa kwenye lockdown kwa kipindi kirefu zaidi ikilinganishwa na wananchi wa nchi zingine.

Mahusiano ambayo yanapitia changamoto yata athiriwa sana, huku kukiwa na uwezekano kwa wanandoa kuchukua nafasi na kupumzika mbali na nyumbani. Wanandoa walio kwenye matatizo hawawezi tegemea watu wa nje kama vile wataalum wa afya ya kiakili kuwasaidia, shukrani kwa hali ya lockdown. Mara nyingo, watoto watakumbana na matatizo ya kindoa ya wazazi wao na kuwaacha wakiwa na woga maishani mwao.

Kwa hivyo, kuna maanisha nini? Je, uhusiano wako hautakuwa na mafanikio kwa sababu ya kuwa na mchumba wako wakati mwingi? Je, homa ya corona na talaka zina andamana, na kuwacha maisha yako yakiwa na matatizo? Sio lazima. Hapa kuna vidokezo kuhakikisha kuwa ndoa yako haivunjiki kufuatia virusi hatari vya homa ya corona.

Homa ya Corona na Talaka: Jinsi ya Kuvunja mnyororo

Tafuta tena kiinimacho

coronavirus and divorce

Sio rahisi kukuza mapenzi huku ukiwa umefungiwa kwa nyumba yako. Mapenzi yana husu kugawana yote mema na mabaya. Wacha kungoja mchumba wako akose doa; badala yake, anza kufanya mambo pamoja. Unaweza jaribu kupika chakula pamoja na hapo baadaye, mtizame sinema pamoja. Geuza sebuleni yako iwe kilabu. Ifanye iwe na giza, weka muziki, valia kana kwamba unapelekwa mahali pazuri na mfurahie usiku wa densi na mchumba wako.

Kuwa na huruma na mchumba wako

Ni rahisi kupenda mtu ambaye ana kuonea huruma. Jaribu kutazama vitu na jicho la mchumba wako na uelewe wasiwasi wake. Sio lazima uwe na suluhu kwa matatizo yake yote; kitu ambacho huenda mchumba wako akahitaji kutoka kwako huenda kikawa ni sikio la kusikiza na akili yenye kuelewa.

Nafasi yako ya kipekee

Binadamu ni watu wanao penda muingiliano; sisi wote tuna hitaji nafasi yetu ya kipekee. Hii ni muhimu hasa kwa wanandoa walioko kwenye karantini. Tafuta kona ya nyumba yako na uifanye iwe yako. Kila mara unapo taka kuwa peke yako, enda kwenye nafasi hii. Huenda hata ikawa ni dirisha kwenye chumba chako cha kulala. Upate wakati wako. Soma kitabu, kunywa chai na ujiburudishe. Jaribu kupaka rangi ama kufanya kitu kinacho kupendeza. Heshimu "wakati wa kipekee" wa mchumba wako iwapo anahitaji kuwa peke yake.

Mazungumzo ni muhimu sana

Fanaka ya uhusiano wowote una amuliwa na jinsi wachumba wote wawili wanazungumza. Kuto elewana kuna weza tendeka, ila umefungiwa kwenye nyumba yako huku dunia ikipambana na virusi hatari vya homa ya corona. Jaribu kuto kuwa na hakimu nyingi. Himiza mazungumzo na majadiliano na mchumba wako;sio lazima yawe ya jambo la dharura. Mazungumzo ya jambo lolote hata mambo mepesi ya mara kwa mara yatawavuta pamoja ili muwe na uhusiano wa karibu na mcheke pamoja.

Kura ya mtoto

homa ya corona na talaka

Kubishana ni jambo moja ambalo haliwezi kuepukika kwenye ndoa. Ila, watoto wako hawapaswi kushuhudia jambo hili. Sio rahisi kubishana kama watoto hawako kukiwa na lockdown. Hapa ndipo kujidhibiti kunaingilia kati. Pia unaweza kuwa na ubunifu mkiongelelea tofauti zako; badala ya kurushiana maneno, mnaweza chekeshana. Huku kuna weza pelekea kupata mtoto aliye ndani yako na kukuwacha na mchumba anayependa kucheza na ndoa yenye afya. Iwapo bado unasisitiza kurushiana maneno, fanya hivi kupitia mtandao wa WhatsApp ama mtandao mwingine. Huku kuta hakikisha watoto hawakomi katikati ya mabishano yenu jambo ambalo litakufanya ujute hapo baadaye.

Homa ya corona itashindwa na tuizidi siku moja; huenda jambo hili lisitendeke kwa kipindi cha wiki moja ama hata mwezi mmoja. Ila, wakati litatendeka, unapaswa kuwa na maisha ya familia utakayo yarudia, familia ambayo ni egemeo lako na kipande cha kati cha maisha yako. Kumbuka kuwa vita dhidi ya virusi hivi sio kwa hospitali tu ama mashirika ya utafiti tu. Pengine kiwanja kikubwa zaidi cha vita hivi ni nyumbani, kwa sababu tukifeli hapa, kutakuwa na haja gani kushinda vita hivi mahali pengine?

Soma Pia: COVID-19 Pandemic: Italian Couple Celebrate 50th Wedding Anniversary In ICU

Kumbukumbu:
https://en.wikipedia.org/wiki/Fiona_Shackleton

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Zu Ying na kuchapishwa tena na idhini ya theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio