Homa Ya Korona Na Barakoa Za Uso Zina Usawa Upi?

Homa Ya Korona Na Barakoa Za Uso Zina Usawa Upi?

Iwapo una shaka ya kupata virusi hatari vya homa ya korona, unapaswa kuvalia mask ya uso kujikinga?

Masaa 24 tu baada ya kisa cha kwanza cha homa ya korona nchini Nigeria, bei ya masks za uso na sanitizers za mikono zilipanda sana. Na hiyo ni kama ulipata duka lolote lililokuwa na vitu hivi. Wana Nigeria wengi walipatwa na wasiwasi wa kununua vitu vya nyumba na wauzaji wengi wakaliona jambo la busara kuficha masks za uso na sanitizers za mikono. Ni nini ambacho homa ya korona na barakoa za uso zinako nacho kilicho sawa? Inaaminika kwa sana kuwa masks za uso ni hatua ya kuzuia dhidi ya COVID-19. Makala haya yata angazia na kukusaidia kupata ufanuzi zaidi ya imani hii iwapo ni kweli ama la. Angalia hapa chini.

Homa ya korona na Barakoa za Uso: Hatua Ya Kuzuia ama Kupoteza Wakati?

coronavirus and face masks

Watu mashuhuri na masks za kipekee| Google

Kulingana na CDC, masks za uso za upasuaji hazita kuzuia kunusa particles za hewa zinazo sababisha maambukizo. Na wala hizi masks hazifuniki mapua yako kabisa. CDC inashauri kuwa barakoa za upasuaji ni za watu ambao tayari wana dalili za homa ya korona na lazima watoke nje; kwani kuvalia mask kunaweza saidia kuzuia kueneza kwa virusi hivi kwa kuwalinda wengine walio karibu unapo kohoa ama kuchemua. Wakala hii pia inashauri kuwa masks hizi iwapo wewe ni mtunzi wa mtu aliye athiriwa na virusi hivi.

Ila, inaonekana kuwa watu hawakubaliani, kwani hata watu mashuhuri wana onyesha picha zao wakiwa na mask hizi katika mitandao ya kijamii.

“Bila mchezo watu-WACHENI KUNUNUA MASK HIZI!” alisema DR. Jerome Adams, Surgeon General wa Umerikani tarehe 29 mwezi wa pili. “Hazisaidii katika kuepusha umati wa kijumla kutoka kuambukizwa #homa ya korona; ila, iwapo watunzaji wa afya hawawezi kuzipata wanapo watunza wagonjwa, inatuhatarisha sote na jamii zetu!”

Katika mahojiano, Adams alisema kuwa kuvalia barakoa kuna weza ongeza hatari yako ya kupata virusi hivi. “Watu wasio jua jinsi ya kuvalia mask hizi vizuri wakati mwingi hujigusa usoni mara nyingi na kuongeza kusambaa kwa homa ya korona.”

Ila watu wanazidi kununua na kuvalia barakoa za uso. Kwa nini? Baadhi ya watu wana amini kuwa kuvalia mask kuna punguza mara wanazo shika mapua na midomo yao; hata kama hakuna utafiti wa kuunga jambo hili mkono. Sababu zingine ni za kisykolojia. Mojawapo inatokana na uwoga wa kupoteza udhabiti wa virusi hivi ambavyo hatuna maarifa kuhusu kuzuia kwake.

Kwa kutumia mask, hata kama haifanyo mengi, inakupatia uwezo wa kudhibiti hali; mbali na virusi hivi. Inapatia mtu binafsi hisia nyingi za udhibiti katika hali hii ambayo haiwezi thibitika.

COVID-19 Na Mask Za Uso: Shirika La Afya Duniani Lina Yapi Ya Kusema

coronavirus and face masks

Health worker screening travellers at airport | Google

Kulingana na WHO, unapaswa kufahamu mambo yafuatayo kuhusu mada ya kuvalia barakoa.

  • Iwapo una afya, unahitaji kuvalia mask pale ambapo una mtunza mtu anayesemekana kuwa na maambukizo ya 2019-nCoV.
  • Valia mask iwapo unakohoa ama una chemua.
  • Mask zinafanya kazi pale zinapo tumika kwa kufuatiwa na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sanitizer ama maji safi na sabuni.
  • Iwapo unavalia mask, unapaswa kujua jinsi ya kuitumia na kuitupa kwa utaratibu.
Jinsi ya Kuvalia, Kutoa na Kutupa barakoaYako
  • Kabla ya kuvalia barakoa, nawa mikono yako kwa kutumia sanitizer iliyo na idadi inayohitajika ya kileo ama sabuni na maji.
  • Funika mdomo wako na mapua kwa kutumia mask, hakikisha kuwa hakuna nafasi iliyobaki katikati ya uso na mask yako.
  • Epuka kugusa barakoa unapoitumia; iwapo utafanya hivi, nawa mikono kwa kutumia sanitizer ama sabuni na maji safi.
  • Badilisha barakoa na nyingine mpya punde tu inapo pata unyevunyevu na usitumie zaidi ya mara moja mask ambazo zinapaswa kutumika mara moja.
  • Kutoa barakoa: itoe kutoka upande wa nyuma (usiguse sehemu ya mbele ya mask); itupe kwa kasi kwenye sanduku la taka; nawa mikono kwa kutumia sanitizer, ama sabuni na maji.

 

Kaa na ujumbe kuhusu maendeleo ya hivi punde ya COVID-19. Fuata ushauri unaopatiwa na daktari wako, mamlaka ya afya ya umma ya mtaani ama kitaifa ama mkubwa wako jinsi ya kujilinda na wengine kutokana na virusi vya COVID-19.

Mbona? Mamlaka ya Kitaifa ama Mitaani watakuwa na ujumbe ulio afikiana na tarehe iwapo COVID-19 inasambaa katika sehemu unayo ishi. Wako mahali pema zaidi kukushauri jinsi watu walioko katika sehemu unayo ishi wanacho paswa kufanya kujikinga.

Jinsi ya Kujilinda na Wengine Kutoka na Maambukizi haya

hands

Haijalishi ama una valia mask kama hatua ya kujilinda dhidi ya homa ya korona, kumbuka kujilinda wakati wote. Zingatia usafi; nawa mikono yako vyema kwa kutumia sabuni na maji mara kwa mara; na utumie sanitizer ya mkono. Wakati wote unapo chemua ama kukohoa, tumia sehemu ya ndani ya kiwiko chako ama kwenye tissue kisha kuitupa bila kukawia.

KAA NYUMBANI iwapo unahisi vibaya/mgonjwa, hata na dalili nyepesi kama vile kuumwa na kichwa na homa, hadi utakapo pona. Mbona? Epuka kugusana na wengine na kutembelea vituo vya matibabu kutakubalisha vituo hivi kufanya kazi vyema zaidi na kusaidia kukulinda wewe na wengine kutokana na virusi vya COVID-19 na vinginevyo.

Iwapo unapata joto jingi, kukohoa ama matatizo ya kupumua, wasiliana na daktari bila kukawia kwani hii huenda ikawa ni maambukizo ya mfumo wa kupumua ama hali nyingine ya dharura. Piga simu kabla ya kwenda na umfahamishe daktari wako iwapo umetembea nchi zingine hivi karibuni ama kupatana kifizikia na watembeaji wengine. Mbona? Kupiga simu kabla ya kuenda kutampatia daktari wako nafasi ya kukuelekeza kwa kituo cha afya kinacho faa. Huku kutakusaidia kuepuka kusambaa kwa virusi vya COVID-19 na visuri vingine.

Time , World Health Organization

Originally Written by Lydia Ume

Translated by Risper Nyakio

Soma Pia: 12 Coronavirus Myths Busted! Coronavirus Myths You Should Know About

Written by

Risper Nyakio