Ni Mtoto Mvulana! Hauwa Indimi Na Muhammad Yar'Adua Wakaribisha Mtoto Wao Wa Kwanza

Ni Mtoto Mvulana! Hauwa Indimi Na Muhammad Yar'Adua Wakaribisha Mtoto Wao Wa Kwanza
Hongera kwa Hauwa Indimi na bwanake, Muhammad, baada ya kumkaribisha mtoto wao wa kwanza. Wanandoa hawa wali karibisha mtoto wao wa kwanza siku ya Jumatano, Oktoba 2. Mama huyu wa kwanza alienda kwa mitandao yake kuwajuza watu habari hizi nzuri. Kwa picha akimkumbatia mwanawe, aliandika: "Mdogo wetu ako hapa nasi. Alhamdulillah." Hauwa Indimi ni bintiye billionea wa Hausa, Mohammed Indimi. Alifunga pingu za maisha na Muhammad Yar'adua kwa sherehe ya kufana mwaka uliopita.
billionaire daughter
Mama huyu wa mara ya kwanza aliwajuza watu kuwa alitoka hospitalini na alikuwa nyumbani aliko pokelewa na mikono mikunjufu na jamaa na marafiki wake. Pia, aliweka picha za maua ya kupendeza aliyo pata kutoka kwa familia na marafiki.
Hauwa Indimi

Kumbuka kuwa Hauwa Indimi alifanya harusi katika sherehe ya kufana mwaka uliopita.

Hauwa Indimi
Hauwa ni binti mchanga zaidi wa bilionea wa Maiduguri, Alhaji Mohammed Indimi. Alifanya harusi na bwanake, Muhammad Yar’Adua mwaka wa 2008. Muhammad ni mtoto wa mkuregenzi mstaafu wa Nigerian National Petroleum Corporation (NNPC). Harusi yao ilikuwa ya kupendeza na ya kifahari iliyokuwa ya siku tatu na kusifika nchini Nigeria kote.
Binti ya bilionea na ndugu yake wa kike Meram Indimi walikuwa na sherehe ya Kamu huko Maiduguri. Kamu inafanyika upande wa Kaskazini, ambapo familia ya bwana harusi huenda kuomba bi harusi aachiliwe. Familia ya bwana harusi hujadili kuhusu mahari na familia na marafiki wa bi harusi. Kwa sherehe hii ya kitamaduni, Hauwa na Meram bila shaka walikuwa bibi harusi wa kupendeza zaidi.
Hauwa huwa na biashara ya kuuza manguo kwa mtandao maalum kama 'House of Hauwa' iliyoko Boca Raton huko Florida. Ali hitimu kutoka Chuo Kikuu cha Lynn cha Florida na anapenda vitu vyema vya maisha.
 Hauwa Indimi Na Mchezo Wa Kuigiza Wa Harusi Yake

Familia ya Indimi inafahamika kwa kuwa wakwe wenye kusema katika jamii. Ukihusisha rais wa Nigeria Mohammadu Buhari, ambaye bintiye Zahra aliolewa na mvulana wa billionea Mohammed Indimi. Sherehe zao za harusi huwa za kifahari na tabaka la juu. Lakini kabla ya harusi ya Hauwa mwaka wa 2018, kulikuwa na mambo ambayo haya kutarajiwa. Familia hii tajiri ili shuhudia vita kati ya watoto wao, hasa kati ya madada wa kambo.

Muhammad kijana wa mkuregenzi mkuu wa NNPC aliye staafu, Abubakar Yar'Adua alikuwa afanye harusi na mpenzi wake Hauwa Indimi katika mwezi wa July 2018. Sio jambo kubwa, isipokuwa Muhammad walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Fatima Indimi. Cha kuzidisha ni kuwa alikuwa na uhusiano pia na Zahra Buhari (ambaye ni mkwe wa familia ya Indimi) kwa miaka miwili kabla na baada ya babake kuwa rais wa Nigeria. Hayo yote ni kale kwa sasa kwani wapenzi hawa wawili wameanza familia, haijalishi yaliyo tukia hapo awali. Hongera kwa Hauwa Indimi na bwanake.

Tuna watakia mema katika maisha yao!

Soma pia: Toyin Abraham Is A New Mom! Pros And Cons Of Sharing Family Photos Online

Written by

Risper Nyakio