Baadhi ya hospitali bora zaidi nchini Kenya za wamama waja wazito kujifungua

Baadhi ya hospitali bora zaidi nchini Kenya za wamama waja wazito kujifungua

Ni muhimu kwa wana ndoa wanao tarajia kumpata mtoto mchanga kuwa wameji tayarisha vilivyo. Moja baadhi ya mambo wanayo paswa kushughulikia ni kujua hospitali ambayo watao jifungulia.

Ni ndoto ya kila binti kuweza kupata mtoto siku moja. Wote wake kwa waume wana ndoto hili. Mama anapo pata mimba, ni dua lake kuwa ataweza kujifungua salama salmini. Mama mja mzito anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida. Iwapo anapata matatizo wakati wa kujifungua unapo wadia, inafanyiwa upasuaji. Kuna sababu kadha wa kadha zinazo mfanya mama kufanyiwa upasuaji anapojifungua. Moja wapo ni kuwa na mtoto mwenye uzito mwingi. Mtoto anapokuwa mkubwa zaidi, hutatiza kujifungua kawaida. Daktari hana budi wala kumfanyia upasuaji. Kupata mtoto kwa njia yoyote ile si bure nchini Kenya. Kuna gharama yake. Ni muhimu kwa mke na mme kujua hospitali bora za kujifungua nchini na gharama yake. Ili wakati unapo wadia kulingana na uwezo wao wa kimaisha wajue hospitali watakayo itembelea.

Tutazungumzia baadhi ya hospitali bora za kujifungua nchini Kenya

Baadhi ya hospitali bora zaidi nchini Kenya za wamama waja wazito kujifungua

 • Hospitali ya Aga khan, Nairobi

+254 20 3662000

Uzuri wake

 • Ina madaktari bora zaidi
 • Wana services bora zaidi za kujifungua
 • Wana zingatia usafi

Masaibu yake

 • Ni ghali Kwani ni hospitali ya kibinafsi
 • Bei ya juu ya masilahi
 • Ina madaktari wachache
 • Ina furika wagonjwa, watakikana kufika mapema kuepuka kupanga foleni ndefu

Katika hospitali hii, kujifungua kwa njia ya kawaida ni Ksh. 150,000 na kupitia upasuaji ni Ksh. 280,000.

 

 • Hospitali Kuu ya Kenyatta, Nairobi

 + 254 729 406939

Hii ni mojawapo ya hospitali nzee zaidi nchini. Ni ya serikali na wala si ya kibinafsi. Bei zake za kujifungulia humu ni Ksh 35,000- Ksh. 53,000 kujifungua kawaida. Kupitia njia ya upasuaji itamgharimu mama Ksh. 100,000- Ksh. 152,000.

Faida 

 • Bei zao ni za chini kulinganisha na za hospitali ya kibinafsi.
 • Huduma zake ni bora

Ubaya 

 • Ni vigumu kupata mahali pa kuliegesha gari lako

 • Hospitali ya Mater

+254 20 6903000

Hii ni hospitaali ya kikatholiki.

Faida 

 • Mojawapo ya hospitali bora zaidi za kibinafsi
 • Wana kubali wagonjwa kutumia bima

Ubaya 

 • Huduma zao si za bei ghali
 • Huduma zao ni pole pole
 • Kujifungua kikawaida ni Ksh. 60,000 na kupitia upasuaji ni Ksh. 165,000.

 

 • M.P Shah Hospital

+254 722 204427

Faida 

 • Wana mashine bora 
 • Wafanya kazi bora

Ubaya 

 • Huduma zao ni pole pole
 • Foleni ndefu unapo enda kutibiwa

Kujifungua kikawaida ni ksh. 120,000 ilhali kupitia upasuaji ni Ksh. 220,000.

 

 • Karen Hospital

Uwasiliano: +254 702 222222

Hii ni mojawapo mwa hospitali bora zaidi nchini Kenya.

Faida 

 • Ina teknologia ya kiduniani na huduma bora zaidi.

Ubaya 

 • Ni ghali Kwani ni ya kibinafsi
 • Kupitia upasuaji ni 230,000 na kwa njia ya kawaida ni 120,000.

 

 • Hospitali ya Nairobi

Uwasiliano: +254 20 2845000

Hospitali hii inajulikana East Africa yote kupitia matibabu bora zaidi

Faida 

 • Matibabu yake ni ya kibinafsi kwa kila mgonjwa
 • Wana angalia usafi wa hospitali
 • Huduma zao ni bora

Ubaya 

 • Ina furika watu, kwa hivyo magonjwa anapaswa kufika hospitalini mapema.

Kujifungua kikawaida ni Ksh. 95,000 iwapo kupitia njia ya upasuaji ni Ksh. 220,000.

 

 • Nairobi women’s hospital

+254 20 2726821

Hospitali hii ilianzishwa mwaka wa 2001.

Faida

 • Ina madaktari na wauguzi wema
 • Ina mashini bora zaidi zinazohitajika katika kujifungua

Ubaya

 • Huduma za kipole pole
 • Ni ghali
 • Kupanga foleni kwa muda mrefu

Kupata mtoto kwa njia ya kawaida ni Ksh. 64,000 na kupitia upasuaji ni takriban Ksh. 145,000.

 

 • Hospitali ya Coptic

+254 716 896965

Faida 

 • Usafi wa hospitali umezingatiwa
 • Huduma bora

Ubaya

 • Wafanyakazi si wataalamu
 • Unakawia kuhudumiwa

Kujifungua kwa wamama walio waja wazito kupitia njia ya kawaida ni 45,000. Anapo jifungua kupitia upasuaji ni Ksh. 120,000.

 

 • Hospitali ya Metropolitan

+254 722 207665

Faida

 • Wana huduma bora kwa mama anaye jifungua
 • Wauguzi wanam saidia mama mpaka anapo kubalishwa kuenda nyumbani na mtoto wake
 • Madaktari wana huduma na masomo ya juu

Ubaya

 • Huduma zao ni ghali

Kwa njia ya upasuaji ni Ksh. 50,000 taaslimu iwapo kujifungua kwa njia ya kawaida ni Ksh. 100,000.

 

 • Hospitali ya Guru Nanak

+254 722 203884

Faida

 • Madaktari na wauguzi wana utaalamu
 • Usafi umezingatiwa
 • Wana huduma bora za kujifungua
 • Wana bei nafuu

Ubaya

 • Madaktari wengine wana siku maalum na kukosa zingine
 • Kujifungua kwa njia ya kawaida ni Ksh. 45,000 ilhali kupitia upasuaji ni taaslimu Ksh. 155,000.

Read Also: A Go-To List of The Top Kenyan International Schools

 

Written by

Risper Nyakio