Kuna baadhi ya watu wanaosema kuwa hawana hamu ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi. Baada ya kuwauliza maswali kuhusu maisha yao ya kimapenzi, una ng'amua kuwa hiyo ni njia ya kujilinda na kujikinga dhidi ya kuumizwa katika mapenzi. Hujuma katika uhusiano ni jambo la kawaida hata kama lina athari hasi. Je, kipi kinacho sababisha tabia hii?
Hujuma katika uhusiano

Hujuma katika mahusiano ni tabia zinazo komesha uhusiano wenye mafanikio ama kufanya watu wakome kuwa katika uhusiano. Cha muhimu zaidi, hujuma katika uhusiano ni njia ya kujilinda kuepuka kuumizwa.
Kwanini tuna hujuma kuhusu uhusiano?
Watu huwa na tabia hii kufuatia uwoga. Hata kama wangependa kuwa na uhusiano wa kimapenzi. Hata hivyo, sio rahisi kugundua ama kuona uwoga huu. Kwa sababu hisia zetu zimetandazwa kutulinda. Uwoga huwa umefichwa na hisia zetu kama kujihami ama kujikinga.
Unafahamu baadhi ya mitindo hii?
Hujuma katika uhusiano sio jambo la mara moja katika mahusiano. Hufanyika uwoga unapo anzisha mitindo ya tabia kutoka kwa uhusiano mmoja hadi mwingine. Angazia mitindo hii ya tabia katika mahusiano yako.
Kuzikinga hisia zako kama vile kukasirika ovyo ama kuongea vibaya unapoongeleshwa kwa njia usiyopendelea. Watu wanaojikinga hivi huwa na motisha ya kujihalalisha, wanataka kuonekana kuwa wanachofanya ni sawa.
Vitisho vinavyofanya wajikinge huwa kufuatia maumivu kutoka kwa uhusiano uliopita, kukosa tumaini, uwezekano wa kuumizwa tena na uwoga wa kufeli, kukataliwa, ama kuwachwa. Walakini, kujikinga huwa tabia inayoeleweka baadhi ya wakati.
Watu wanaweza amini kuwa mahusiano mara nyingi huishia kwa "kuvunjwa roho".

Kutatizika kuamini wengine huhusisha kutoamini wachumba wa kimapenzi na kuhisi wivu wa umakini kwa wengine. Watu wanaohisi hivi huenda wakakosa kuhisi salama na kuepuka kuonyeshana udhaifu wao katika mahusiano.
Hii huwa mara nyingi kufuatia mambo yaliyofanyika hao awali, imani yako kusalitiwa ama kutarajia kusalitiwa. Watu huchagua kuto amini kama njia ya kuepuka kuumizwa tena.
- Kukosa ujuzi wa mahusiano
Mtu anapokosa maarifa kuhusu tabia zinazo fanya mahusiano yake kuisha. Huenda ikawa ni kufuatia kukosa mifano miema ya kuigwa katika mahusiano, mahusiano hasi na matokeo kutoka mahusiano ya hapo awali.
Lakini ujuzi wa mahusiano unaweza kusomwa. Mahusiano yenye afya yanaweza kuboresha ujuzi wa mahusiano na kupunguza athari za kujikinga na kukosa imani katika mahusiano.
Gharama ya hujuma katika mahusiano
Hujuma ya mahusiano wakati wote haifanyi mahusiano kufika kikomo. Inategemea na iwapo mitindo hii ni ya muda mrefu.
Kwa watu wasio katika mahusiano, hujuma ya mahusiano itawafanya wasiingie katika mahusiano. Kwa watu walio katika mahusiano, kutumia mbinu za kujikinga kwa muda mrefu kutafanya uwoga wao kugeuka kuwa ukweli wao.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi