Riwaya kwa Bwanangu mpendwa asiye penda kuiweka simu yake chini

Riwaya kwa Bwanangu mpendwa asiye penda kuiweka simu yake chini

Bwanangu mpendwa, ningependa uelewa nafasi muhimu zinazo kupita unapo fika nyumbani na bado uko kwa simu yako. Unakosa kuwa na wakati na familia yako haswa watoto wetu wanao kua na wanakuhitaji.

Bwana mpendwa,

Kwanza, ningependa kukushukuru kwa upendo na furaha unayoileta kwa familia yetu. Watoto wetu nami tumebarikiwa kuwa nawe na tuna lifahamu hilo. Kwa hivyo, Asanti.

Lakini, kumbuka wakati ambapo mtoto wetu wa kike alipo sema jina lake la kwanza? Tulikuwa tumekaa sembuleni tukitazama sinema uliyo ichagua. Ila, haukuwa unaitazama kwani umakini wako ulikua kwa chochote kile kilichokuwa kikikufanya utabasamu simuni mwako. Hiyo ndo maana alipo sema “dada”, hili ni jambo unalofanya wakati wote. Una sisitiza tutizame sinema ila unachukua simu yako. Baada ya masaa mawili, sinema inaisha na pia fursa ya kuwa na wakati wa kimafilia.

 

Naelewa, tafadhali najua ni simu yako ni kifaa cha kujuwana na watu na wakati mwingine cha kazi pia. Pia najua simu yako inakusaidia kupumzika baada ya siku ndefu. Pia nina hatia ya kuchagua mtandao wao instagramu badala ya Kucheza mchezo wa peekaboo na kijana wetu kwa mara ya 57 sasa mfululizo. Naelewa usumbufu inayo sababisha. Lakini hapa ni baadhi ya mambo usiyo yafahamu. Unakosa. Unakosa kwa kumbukumbu za kupendeza za familia za watoto wako ambazo huwezi pata tena.

Nachukia tupo kanisani, mafunzo yanaendelea, unaufikia mfuko wako kuchukua simu yako kwa sababu “ mteja anaweza tuma ujumbe mdogo.” Kanisani? Je, unafunza watoto wako nini? Uzazi ni uongozi kwa mfano, na hawa wako tayari kufuata mambo yote wanayo ona tukiya fanya.

Lilikuwa jambo la kuudhi sana tulipokuwa wawili. Nililipata jambo hili la kuudhi sana, na mara nyingi kurudia jina lako kwani hukunisikia mara ya kwanza. Lilikuwa lina niaibisha tulipokuwa nje na familia na ulikuwa aliye kuwa anakaa na simu yake wakati wengine wote walikuwa wakiongea.

Ilipokuwa sisi wawili, nilihisi kana kwamba ulikuwa na mimi nusu. Nilikuwa naongea ila tu ulikuwa ukinipa umakini kidogo wakati umakini ulio baki ulikuwa unajaribu kufikia Blackberry Messenger. Hata ni ngumu kukumbuka hapo kale ambapo simu mahiri hazikuwa zina tambulika bado na ulikuwa ukienda kwa masaa mengi bila simu mkononi mwako.

Sasa, sisi ni familia, iliyo barikiwa na watoto warembo. Hizi dakika chache zinazo kaa hazina maana zinazo kupita uki kupeleka kidole gumba chako kikiwa kwa simu. Zina thamani kubwa. Sitaki uangalie nyuma na ugundue mengi ambayo haukuyaona kwani ulikuwa unaangalia chini kwa simu yako.

Bwana mpendwa, nakupenda wewe, ila uzoefu wako kwa simu unaniumiza. Ina adhiri ndoa yetu na uhusiano tulio nao na mtoto wetu. Tafadhali fikiria kuhusu ujumbe unao pitisha kwa mtoto wako wa kike na bibi yako. Unaweza kosa kujua nguvu uliyo nayo ya kuunganisha ama kututawanyisha.

Tafadhali, nakuomba, iweke simu yako chini wakati mwingine. Kuwa hapa nasi wakati mwingi.

Tutizame kwenye macho simu yako inapo kuwa chumbani kingine. Nakuahidi hauta juta.

Mapenzi,

Bibi yako.

Read Also: Open Letter: My Tryst With Postpartum Depression

Written by

Risper Nyakio