Imani Kuhusu Kunyonyesha Katika Bara La Afrika Zinafichuliwa

Imani Kuhusu Kunyonyesha Katika Bara La Afrika Zinafichuliwa

Bara la Afrika ni nyumba ya imani na itikadi zisizo za kweli. Inapofika wakati wa kupatia mama ushauri kuhusu mtoto, imani kuhusu kunyonyesha zimejaa kote. Imani nyingi na hadithi kuhusu kunyonya zimepitishwa kutoka kwa kizazi hadi kingine, familia na hata marafiki. Hata kama kwa kawaida watu huwa na nia njema, sio hadithi hizi zote zilizo za kweli. Baadhi ya ushauri huwa si wa kweli ama umepitwa na wakati.

Wakati ambapo viwango vya kunyonyesha duniani kote na Nigeria vinaendelea kuongezeka, kuna idadi kubwa ya watu wasio jua kuhusu mada hii. Ukweli ni kuwa, kunyonyesha ni njia ya afya ya kumlisha mtoto wako. Uamuzi wa kumnyonyesha ni wa kipekee na unapaswa kufanywa baada ya kuelimishwa kuhusu mada hii. Katika makala haya, tutaangazia baadhi ya imani kuhusu kunyonyesha zisizo za kweli ambazo huenda ukawa umezisikia.

Imani kuhusu kunyonyesha zikilinganishwa na ukweli kuhusu kunyonyesha

imani kuhusu kunyonyesha

  • Imani 1: Kumnyonyesha mtoto kutafanya matiti yako kusag

Hakuna jambo ambalo huenda likawa mbali na ukweli. Ni ujauzito na wala sio kunyonyesha mtoto kunako fanya ligaments za matiti yako kunyooka. Kwa hivyo, kadri unavyo zidi kuwa na kupata watoto wengi ndivyo nafasi zako za kuwa na matiti iliyo sag kunaongezeka kwa kuzeeka na pia uvuto wa ardhi. Walakini, ni jambo la busara kusitiri matiti yako na sindiria nzuri.

  • Imani 2: Iwapo matiti yako si kubwa, huwezi nyonyesha.

Muundo ama saizi ya matiti ya mama haiathiri uwezo wake wa kunyonyesha. Ikiwemo ukubwa wa areolas ama chichu zake ama hata wanawake waliofanyiwa upasuaji wa matiti. Iwapo matiti yako yalipunguzwa, walakini, kuna uwezekano kuwa baadhi ya ducts za maziwa zilitolewa pia na huenda kukaathiri uwezo wako wa kunyonyesha.

  • Imani 3: Iwapo matiti yako ni makubwa sana, una uzito mwingi, huwezi nyonyesha.

imani kuhusu kunyonyesha

Baadhi ya watu huamini kuwa wanawake walio na matiti makubwa hutatizika kunyonyesha watoto wao. Hiyo ni imani nyingine za kiafrika isiyo ya kweli. Kama tulivyo angazia hapo awali, muundo na saizi hazi athiri uwezo wa mama wa kunyonyesha.

  • Imani 4: Kufanya mapenzi kunachafua maziwa ya mama na kusababisha kifo cha mtoto.

Wataalum wametupilia mbali imani hii na kusema kuwa hakuna utafiti unao egemeza imani hii. Walakini imedhibitika kuwa kunyonyesha kwa kipekee huenda kukatumika kama njia asili ya kuepuka kupata mimba hasa siku za kwanza baada ya kujifungua. Ni uamuzi wako wakati ambapo utaanza kufanya mapenzi baada ya kujifungua. Ila, kunyonyesha mtoto kunaweza saidia kuepuka kupata mimba ingine, hata inapo punguza uterasi yako irudi ilivyokuwa hapo awali.

  • Imani 5: Maziwa ya kwanza (colostrum) huua mtoto

Inaaminika kuwa maziwa ya kwanza ni mojawapo ya uchafu baada ya kujifungua kama vile placenta. Na kuwa ni mbaya kwa afya ya mtoto wako kwa sababu ina rangi ya kinjano. Ukweli ni kuwa maziwa haya yana afya zaidi na virutubisho vingi. Maziwa ya rangi ya kinjano yanayo toka kwa matiti ya mama siku za kwanza baada ya kujifungua.

  • Imani 6: Mwanamke anarogwa iwapo haanzi kunyonyesha mtoto punde tu baada ya kujifungua.

Sababu nyingi zinaweza kuathiri unyonyeshaji wa mtoto, kusababisha kutoka kwa maziwa ya mama. Pia, baadhi ya wanawake hawanyonyeshi hata! Wanawake wanaopata watoto kupitia upasuaji wa C-section wanapata kuwa hawatoi maziwa kwa urahisi. Itachukua muda wa angalau siku moja ama mbili kabla kuanza kunyonyesha. Kwa kweli haihitaji mambo zaidi ili mwanamke aanze kunyonyesha.

  • Imani 7: Mwanamke hapaswi kunyonyesha akiwa amekasirika ama kama hana furaha

Baadhi ya wanaafrika huamini kuwa wakati mwanamke anapokuwa amekasirika, lazima awache kunyonyesha mtoto hadi pale atakapo hisi vizuri, kwani atakuwa anampitishia mtoto hisia hizi. Ila, fikira nyingi, kukasirika na uwoga huenda kuka athiri kiwango cha maziwa ambacho mama anatoa na kuathiri kuwepo kwa maziwa. Ila haiathiri ubora wa maziwa haya. Wamama wana shauriwa kupata ushauri nasaha jinsi ya kuepuka hali hizi ili kuwepo kwa maziwa kusi athirike.

imani kuhusu kunyonyesha

  • Imani 8: Kutoka nje ya ndoa kunachafua maziwa ya mama na huenda kukasababisha kifo cha mtoto

Baadhi ya watu wanaamini kuwa kutoka nje ya ndoa ama kuwa na wapenzi wengi (zaidi ya mmoja) kunachafua maziwa ya mama na kubadili ubora wa maziwa ya mama. Watu wana amini kuwa huenda jambo hili likasababisha kifo cha mtoto. Hii si kweli. Ukweli ni kuwa kutoka nje ya ndoa ama kuwa na wachumba wengi kuna mweka mama katika hatari ya kupata maambukizo ya ngono. Na haya ndiyo maradhi ambayo mama anaweza sambaza kwa mtoto wake na hatimaye kusababisha kifo chake.

Na kuweko ama kuzingatiwa kwa ustaarabu wa kibinadamu na mtandao unao zidi kukua, wanawake wengi wa Afrika wanazidi kulitilia maanani jambo la kunyonyesha watoto ili wapate virutubisho bora. Wakati ambapo tunajua kuwa imani hizi hazitaisha kwa kasi, tujaribu kadri tuwezavyo kuwafahamisha wengine ukweli kuhusu kunyonyesha hasa wamama wapya tunao kutana nao. Kwa muda mdogo, tutapata kuwa imani hizi zimetupiliwa mbali.

Chanzo:

UNICEF

Kapital FM

Business Daily

Soma pia 7 Breastfeeding hygiene tips for new mums

Makala haya yali andikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio