Imani Za Nyonga Za Kujifungua Ni Kweli Ama La?

Imani Za Nyonga Za Kujifungua Ni Kweli Ama La?

Huenda ukawa kuwa umesikiwa kuwa wanawake wenye mapaja pana wana urahisi wanapo jifungua. Mtu kuambiwa kuwa ana nyonga za kujifungua inapaswa kuwa jambo nzuri. Ina maana kuwa mwanamke huyo hatakuwa na matatizo inapofika wakati wa kujifungua. Ila, imani za nyonga za kujifungua huwa kweli?

Je, wanawake walio na paja nyembamba wana shuhudia kujifungua kuliko na matatizo ikilinganishwa na walio na paja pana?

birthing hips myth

Imani za nyonga za kujifungua: je, kujifungua ni rahisi kwa wanawake walio na nyonga pana?

 Imani kuhusu nyonga za kujifungua: kwa nini baadhi ya wanawake huwa na nyonga kubwa kuliko wengine?

Saizi ya nyonga yako ina mengi ya kufanya na saizi na shepu ya pelvis yako. Kuna aina 4 kuu za shepu ya pelvis kama ifuatavyo:

  • nyonga ya anthropoid
  • nyonga ya gynaecoid
  • nyonga ya android
  • nyonga ya platypoid

Nyonga ya anthropoid

android

Karibu asilimia 20- 30 ya wanawake wana shepu ya anthropoid pelvis. Ina mviringo na kipenyo kipana. Ni kawaida sana kwa wanawake wa rangi maarufu kama black women. Pia, wanawake wanao kuwa na anthropoid pelvis huwa na makalio mapana ikilinganishwa na shepu zingine.

Nyonga ya gynaecoid

imani za nyonga za kujifungua

Gynaecoid pelvis ndiyo pelvis maarufu kwa wanawake. Ina mviringo na ni pana. Hii ndiyo pelvis inayo ongelelewa watu wanapo ongea kuhusu nyonga za wanawake za kujifungua. Wanawake wenye pelvis hii wana shepu na hips.

Wanabeba uzito wao mwingi kwenye mapaja na mara nyingi huwa na tumbo laini. Huenda kukawa na kiasi cha ukweli kwenye imani ya nyonga za kujifungua za gynaecoid pelvis kwa sababu ya upana wake unao tengeneza njia tosha ya upitaji wa mtoto.

Nyonga ya android

android pelvis

Muundo huu wa pelvis una shepu ya miramba mine, ambayo huenda ikatatiza watoto wakubwa kupita. Watoto wadogo wanaweza pita bila tatizo kubwa kwa mama na mtoto.

Pelvis hii ya android ni kawaida kwa wanaume ikilinganishwa na wanawake. Wanawake walio na shepu hii huwa na makalio laini na tumbo zao huenda zikawa laini ikilinganishwa na wanawake wenye shepu zingine. Pia, wakati ambapo imani za nyonga za kujifungua zinapo ambiwa, imani ya android pelvis huwa tofauti kabisa.

Nyonga ya platypoid

pelvis

Shepu ya pelvis ina sacrum pana na iliyo laini ndani. Platypoid ni fupi ikilinganishwa na shepu zingine zote. Ni kawaida kwa wanawake walio na shepu hii kushikilia uzito mwingi kwenye sehemu yao ya chini.

imani za nyonga za kujifungua

Imani na kweli kuhusu nyonga za kujifungua

imani za nyonga za kujifungua

Imani: Wanawake wenye nyonga pana wana jifungua kwa urahisi ikilinganishwa na wanawake wakonda.

Ukweli: Kujifungua sio rahisi kwa mtu yeyote. Hii haina maana kuwa wanawake wenye nyonga pana hawa tatiziki. Sababu zinazo athiri kujifungua ni upana na shepu ya pelvis. Mwanamke huenda akawa na nyonga pana na pelvis konda.

Imani: Wanawake walio na nyonga pana hutunga kwa urahisi.

Ukweli:  Kukosa kutunga huenda kuka athiri mtu yeyote, haijalishi shepu na saizi yake. Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikamfanya mwanamke kutatizika kupata mtoto.

Imani: Wanawake na wanaume walio na nyonga pana wanapendeza zaidi ya wanawake wenye nyonga konda.

Ukweli: Urembo, kama wanavyo sema, yako katika macho ya anaye tizama. Hii ni kusema kuwa kinacho mpendeza mtu mmoja hakita mpendeza mwingine. Na cha zaidi ni kuwa kila mtu ana maana ya urembo.

Imani: Wanawake walio na nyonga pana wana nafasi zaidi za kupata mapacha

Ukweli: Shepu ya mwanamke haiathiri nafasi zake za kupata mapacha

 Baadhi ya sababu ambazo huenda zika athiriwa iwapo mwanamke atapata mimba ya mtoto zaidi ya mmoja:

  • Genes/jeni – mamake ama ndugu yake ana mapacha
  • Uzito – utafiti umeonyesha kuwa wanawake walio warefu na wazito wana nafasi zaidi za kupata mapacha wasio fanana
  • Umri – Kadri mwanamke anavyo zeeka, mabadiliko kwenye utaratibu wake wa ovulation humzidishia nafasi za kupata mapacha wasio fanana. Hii ni kweli kwa wanawake walio na umri wa miaka 35 na zaidi
  • Matibabu ya kukosa kutunga – madawa ya ulezi huenda yakamfanya mwanamke kutoa mayai zaidi ya moja, na hivyo kuongeza nafasi zake za kujifungua mapacha wasio fanana
  • Kujifungua mapacha hapo awali – mwanamke aliye jifungua mapacha ana nafasi zaidi za kujifungua mapacha wengine

Imani: Wanawake walio na nyonga nyembamba wakati wote wanafanyiwa upasuaji wa C-section

Ukweli:Kuzaliwa kwa mtoto haku athiriwi na saizi ya nyonga ila na shepu na upana wa pelvis. Mwanamke yeyote huenda akahitajika kufanyiwa C-section.

Kumbukumbu: Medline Plus

BirthBalance.com

Soma pia: Study: Giving birth to a baby boy can be more painful than delivering a baby girl

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio