Imani 7 Zisizo Za Kweli Kuhusu Mimba Zinazo Aminika Sana

Imani 7 Zisizo Za Kweli Kuhusu Mimba Zinazo Aminika Sana

Kuvumbua ukweli kuhusu mimba na imani zisizo za kweli za kupotosha mama mwenye mimba. Kulinda afya ya mama na mtoto.

Hongera, una mtoto mdogo aliye tumboni mwako na maisha yako yatabadilika. Ujauzito ni wakati wa kufurahia na wenye matarajio mengi, kama jinsi wamama wengi watakavyo kueleza. Pia ni wakati ulio jazwa na maswali mengi, kwa bahati mbaya, kulingana na imani. Tuna orodhesha imani 7 zisizo za kweli kuhusu mimba ambazo huenda ukawa umesikia. Wewe na mtoto wako mnahitaji afya njema na amani ya kimawazo na tutakusaidia kutimiza haya.

Mwanamke anapo tunga mimba, hasa katika siku za hapo awali, anapatiwa orodha ndefu ya mambo anayo paswa kufanya na asiyo paswa kufanya na wakati mwingine huambiwa. Masharti hasa ya kuongoza mama huyu mpya na kumsaidia katika kipindi chake cha mimba hadi inapo komaa. Baadhi ya wakati, maagizo haya hutoka kwa mamake, aliye shauriwa na mamake. Wakati mwingine, masharti haya hutoka kwa mama mkwe wake, marafiki na wanao fanya kazi naye. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa masharti haya hayana egemezo la kimatibabu. Ni imani tu zilizo aminiwa na kufuatwa kwa kipindi kirefu. Imani zisizo za ukweli zilizo pitishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine na kutoka kwa mama mmoja hadi mwingine. Hata kama kila kabila na utamaduni una imani zake.

Ukweli ama La? Imani Zisizo Za Kweli Kuhusu Mimba

  • Usiwajulishe watu kuwa una mimba hadi pale inapo onekana ili mtoto asife

Mojawapo ya vitu ambavyo mamako hukuambia ni kuwa unapaswa kuweka habari za ujauzito wako siri. Watu husema kuwa haujui adui yako ni nani, kwa hivyo inapaswa kuwa siri. Mbali na kumjulisha mwenzi wako na familia iliyo karibu zaidi na wewe, haupaswi kufanya matangazo yoyote hadi mimba yako ianze kuonekana kupitia kwa saizi ya tumbo yako, na kwa wakati huu, hakuna haja ya kusema chochote. Siri haihitajiki. Mtoto ni habari nzuri na habari nzuri zinapaswa kutangazwa.

  • Usiende nje wakati wa alasiri ili mapepo yasim shambulie mtoto wako

Unaambiwa usitoke wakati wa alasiri kunapokuwa na jua kali, kwa sababu kuna aminika kuwa mapepo yana sambaa katika wakati huo, na huenda yakamwingia mtoto wako. Inaaminika kwa sana kuwa hivyo ndivyo watoto wakaidi ndivyo wanavyo tengenezwa. Iwapo ni lazima uende nje wakati wa alasiri, unapaswa kuweka pini ya usalama chini ya chupi yako karibu na tumbo yako. Pini hii itamlinda mtoto wako kutokana kwa mapepo.

Hakuna uhusiano wa kisayansi unao unganisha pini za usalama na mapepo. Hakuna utafiti wa jambo hili na punde tu unapo fanyika, tutakuwa wa kwanza kukujuza.

7 Nigerian pregnancy superstitions

  • Usitizame filamu za uigizaji bandia

Unaambiwa usitizame filamu za uigizaji bandia kwa sababu mtoto wakoa atakaa kama waigizaji hawa. Ama mbaya zaidi, huenda ikasababisha kifo cha fetusi. Huku kuna maana kuwa hauwezi jumuika na sherehe za fanfares na carnivals kwa sababu una mimba. Isipokuwa pale ambapo waigizaji hawa wanakuchapa kwenye tumbo ama kukugusa, haijulikani jinsi wata sababisha kifo. Na hatuna uhakika jinsi ambavyo DNA ina sambazwa kuwa kutizama. Kulingana na tunayo yafahamu, waigizaji bandia husakata densi na kuwatumbuiza wanao angalia. Ili kuwa na uhakika, watoto huwa na sura za watu walio na DNA zao.

  •  Usile konokono, ama okro

Unapokuwa na mimba, unaambiwa usile konokono, okra ama ewedu. Wanakwambia ukila vitu hivi, utajifungua mtoto mwenye mahitaji spesheli kama vile kumwaga mate siku yote.  Imani hii inachekesha zaidi kwani wazee wa hapo awali walidhani kuwa kula konokono hufanya baadhi ya watoto kuzaliwa tofauti. Hakuna anaye uliza kwa nini konokono ni bora kwa watu wasio na mimba na sio kwa wanawake walio na mimba. Mwanamke uliye na mimba, iwapo unatamani kula konokono unapokuwa na mimba, uko huru kuzila. Hakikisha kuwa unakula chakula chenye afya wakati wote.

  • Ukila nyama ya nyasi iliyo katwa ukiwa na mimba, lazima ukusanye mifupa na uiweke

Hatuna uhakika kwa nini ila inasemekana kuwa mwanamke mwenye mimba anapokula nyama ya nyasi iliyokatwa, lazima akusanye mifupa yote na aiweke hadi pale anapojifungua mtoto. Lazima ashike mifupa ile mikononi mwake anapo sukuma mtoto atoke. Wanasema kuwa itasaidia kujifungua kwa urahisi zaidi. Angalau unakubalishwa kula nyama ya msituni. Tuna shuku kuwa utakumbuka mifupa mtoto wako anapo karibia, lakini iwapo utakumbuka, ni sawa.

  • Tengeneza fundo kwenye sketi yako na uweke jiwe ndani

Watu wengi huamini kuwa unapokuwa na mimba, unapaswa kufunga vifundo na kuweke mawe ndani. Wanasema kuwa unapofanya hivi, na kuweka sketi hiyo kwenye kichwa chako, uchungu wa uzazi bila shaka utapungua na utashuhudia kujifungua bila ya kuhisi uchungu. Kitu chochote kinacho kupa uzazi usio na uchungu na kisicho hatarisha maisha ya mtoto wako kime karibishwa. Ila usiwe na shaka iwapo hakitafanya kazi. Hakuna utafiti wa kisayansi.

  • Usinywe moja kwa moja kutoka kwa chupa

Tuna sikia kuwa mama mwenye mimba anapo kunywa moja kwa moja kutoka kwa chupa, mtoto wake atakuwa awe kigugumizi. Watu wana amini kuwa kugugumaa ni kufuatia mama yake kunywa kutoka kwa chupa anapokuwa na mimba. Sio jambo la afya kunywa moja kwa moja kutoka kwa chupa ambayo watu wengine watatumia. Una mimba na unapaswa kuwa makini zaidi hasa na usafi wa lishe. Lakini iwapo hiyo chupa ni yako mwenyewe, kuwa huru kunywa moja kwa moja. Kugugumaa hupitishwa kwenye familia kwa sababu ya kupitishwa kwa kitu kisicho kuwa sawa kwenye upande wa ubongo unao tawala lugha. Iwapo wewe ama mzazi wako mna kigugumizi, huenda watoto wenu wakawa na tatizo hili pia.

Katika karne hii na kipindi cha mtandao kila mahali. Kila kitu unacho hitaji kujua kuhusu mimba kiko kwenye mtandao. Uko huru kutuuliza. Pia, mwulize daktari wako kwani yeye ndiye ana ujumbe wote unaopaswa kujua. Atakuwa na furaha kujibu maswali yako kwa sababu hiyo ni kazi yake. Ni wakati wa kuvumbua ukweli kuhusu imani zisizo za kweli kuhusu mimba, ama sivyo?

Je, umesikia imani zingine zipi kuhusu mimba? Umewahi sikia tulizo orodhesha? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

 

Soma pia: Babywearing In Africa: The Good, The Bad, and the how to

Written by

Risper Nyakio