Kufura Kichwani: Uvimbe Kichwani Unachukua Muda Upi Kuisha?

Kufura Kichwani: Uvimbe Kichwani Unachukua Muda Upi Kuisha?

Uvimbe wa kichwa ni kawaida kwa watoto na watu wazima pia. Ila, watoto wana asilimia kubwa zaidi kwa sababu hawana fahamu nyingi wanapo tembea. Kwa hivyo, sio jambo lisilo la kawaida kwa wazazi kuona watoto wao wakija nyumbani kutoka shuleni na uvimbe kwenye kichwa ama zaidi. Na hawana uhakika muda utakao chukua kupotea. Swali la kushtua ni: inachukua muda upi kwa uvimbe kuisha?

Kimatibabu, uvimbe kwenye uso unajulikana kama hematoma. Baadhi ya watu wanaujua kama goose egg. Wakati ambapo watu wazima ama watoto wanapokuwa na uchungu wa kichwa wa uvimbe, hawako tayari kuenda hospitalini. Badala yake, wana amua kuutibu wakiwa nyumbani peke yao, ambayo ni sawa iwapo dalili sio za dharura. Ila, kujua wakati ambapo dalili ni nyingi na wanapaswa kuenda hospitalini huenda kukawa kugumu.

Ina chukua muda upi kwa uvimbe kuisha?

how long does it take for a bump to go away

Kwa kawaida, ishara za uvimbe wa kichwa huisha baada ya masaa 48 kufuatia ajali. Walakini, huenda zikaisha baada hata ya wiki mbili. Ila, ikipita muda huu, huenda ikawa uliumia sana. Huku kuna elezea kwa nini sehemu hiyo bado imefura.

Alama za vidonda haziishi mbio sana. Huenda zikachukua wiki chache kuisha ama hata muda mrefu. Hii ni kwa sababu alama huenda zikapata maji ndani ama unyevu wa tishu chini ya kidonda chako. Katika hatua hii, unashauriwa sana umwone daktari atakaye kukagua sehemu hiyo kuhakikisha kuwa hakuna unyevu chini ya kidonda hicho na kuwa hakuna ishara za maambukizi yoyote.

Pia, huenda uvimbe huu ukageuka kuwa kidonda. Hasa pale ambapo uvimbe huu ni laini na umejazwa na unyevu. Hata kama alama ya tishu huenda ikawa inaonekana tayari, unyevu kwenye kidonda unaweza kaushwa. Na iwapo uvimbe huu hauishi baada ya miezi ama miaka, unapaswa kumwona mtaalum wa upasuaji wa plastiki ili utolewe.

Inachukua muda upi kwa uvimbe kuisha baada ya matibabu ya nyumbani kutumia barafu na joto?

how long does it take for a bump to go away

Kwa kawaida, watu wengi wanaougua uvimbe wa kichwa wanautibu nyumbani bila kuenda hospitalini. Kwa hivyo kati ya joto na barafu ni matibabu yapi bora kwa uvimbe wa kichwa? Fahamu zaidi.

Kutumia barafu kwa uvimbe wa kichwa

Unapo jipaka barafu kwenye uvimbe wa kichwa, utahisi tofauti na pale unapotumia joto. Unapotumia barafu, mishipa ya damu hupunguka kwa saizi, kwa jina la kimatibabu ni vasoconstriction. Barafu hupunguza uvimbe kwa kupunguza mzunguko wa damu kwenye sehemu hiyo. Baridi kwenye barafu inapo fika kwenye tishu chini ya uvimbe huo, inapunguza kazi zinazo endelea. Na kusababisha kifo cha seli za hapo chiini, kupunguza ukuaji wa seli na utoaji mdogo wa uchafu unaotoka kwenye seli.

Kwa hivyo, barafu ndiyo njia nzuri kabisa ya kutibu uvimbe wa kichwa nyumbani. Ili kupata matokeo bora, ongeza shinikizo kidogo unapo finyilia barafu ile. Inasaidia ngozi kushikana ili kupata faida za kutumia barafu.

Kutumia joto kwa uvimbe wa kichwa

Joto huenda ikawa sio njia bora zaidi ya kutibu uvimbe wa kichwa, hata kama inahisi vyema unapoitumia. Njia ya mwili ya kuitikia ongezeko la damu kwenye sehemu hiyo joto inapo tumika kwenye uvimbe wa kichwa. Ila huku kuna sitiza matokeo kwa sababu damu inapo ongezeka, uvimbe unaongezeka zaidi. Na kutumia joto kuna fanya hivyo.

Walakini, huku si kusema kuwa kutumia joto hakuna faida zake. Masaa 24 ya kwanza ya uvimbe wa kichwa tumia barafu, kisha utumie joto mara kwa mara. Sio zaidi ya dakika 15. Kwa njia hii uponaji unaimarishwa kwa sababu joto inaufungua ili damu na virutubisho vifike kwenye tishu zilizo haribiwa.

inachukua muda upi kwa uvimbe kuisha

Unapaswa kumwona daktari lini?

Baada ya kugongwa kichwani, mtembelee daktari bila kukawia iwapo unaanza kushuhudia ishara zifuatazo.

 • Kukosa fahamu, kwa muda mfupi ama muda mrefu.
 • Kugugumaa unapo ongea
 • Matatizo ya kuona
 • Matatizo ya kung'amua
 • Unashindwa kukumbuka vitu kabla na baada ya kugonga
 • Matatizo ya kusoma na kuandika
 • Kuumwa na kichwa sana baada ya kujiumiza kichwa
 • Kutoa damu kutoka kwa sikio moja ama yote mawili
 • Kupoteza uwezo wa kusikia baada ya kugongwa 
 • Kutoa maji maji kutoka kwa mapua na masikio

Kuepuka ajali za kugongwa kichwani kwa watoto nyumbani

inachukua muda upi kwa uvimbe kuisha

Kugongwa kichwa ni kawaida kwa watoto. Kama mzazi, kuhakikisha nyumba yako haina vitu ambavyo vinaweza gonga mtoto ni njia bora salama ya kuhakikisha nyumba yako iko salama. Ila ni vigumu kutarajia nyumba yako kukosa kitu kibaya kabisa kwa sababu kuanguka kunaweza tendeka wakati wowote. Hapa kuna baadhi ya njia za kuepuka.

 • Hakikisha ngazi zako za nyumba ni safi ili wewe ama watoto wako msianguke.
 • Epuka kutumia kiti kilicho vunjika kufikia kitu, badala yake, tumia ngazi kufikia.
 • Usimwage ama kuwacha maji sakafuni. Unapo panguza sakafu, usiwakubalishe watoto kuchezea hapo.
 • Toa fanicha karibu na dirisha. Kwa njia hii, watoto hawawezi jaribu kuzipanda na kuruka nje ya dirisha.

Baada ya kugongwa kichwani, kuwa mwangalifu kwa watoto wako hata baada ya dalili kupunguka. Ishara huenda zikaongezeka baada ya siku chache.

Web MD

Soma pia: What Is Toddler's Fracture Of The Tibia?

Written by

Risper Nyakio