Ikiwa uko katika uhusiano na kuwa na shaka kuhusu uhusiano wenu na iwapo utafunga ndoa na mchumba wako. Ishara hizi zinaashiria kuwa hauko tayari kufunga ndoa.
Ishara kuwa hauko tayari kufunga ndoa

- Unahisi kuwa kuna mengi haujafanya
Kuna watu wengi wanaoingia kwenye ndoa bila kufanya uamuzi dhahiri kuwa wanataka kuwa katika ndoa. Wanahisi kuwa hawajamaliza kufanya mambo fulani ya maisha ya kuwa pekee kabla ya kuwa na familia. Hata kama unahisi kuwa mchumba wako anakufurahisha na ungependa kuwa na familia naye, hisia za kutomalizana na maisha ya kuwa pekee yatakujia. Kuwa na mazungumzo wazi na mchumba wako kuhusu unavyohisi na unachotaka.
2. Una uhusiano na wachumba wako wa hapo awali
Kuwa marafiki na wachumba wako wa awali sio chanzo cha shaka. Wajulishe wako huru kuja kwenye harusi yako na kufanya urafiki na watu wengine. Lakini ikiwa ungali una hisia zao na ungependa kuwa na zaidi ya urafiki nao, ni ishara kuwa kamwe hauko tayari kufunga ndoa. Hisia na akili zako ziko mbali na mchumba wako wa hivi sasa. Ikiwa ungali una urafiki na wachumba wako wa hapo awali, ni vyema kuwa na mipaka dhahiri ambayo wao pia wanafahamu na kuiheshimu.
3. Humwamini mchumba wako na siri zako
Kabla ya kufunga ndoa na mpenzi wako, ni muhimu kuhakikisha kuwa unamwamini na habari zako za siri. Tunaelewa kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo sio lazima kumjulisha. Hata hivyo, kuhisi kuwa humwamini mchumba wako na siri zako ni bendera nyekundu. Huenda ikawa kuna jambo linalokufanya kuhisi hivyo. Ikiwa una hofu zinazokufanya usihisi kuwa huru kuzungumza naye, mjulishe na kwa pamoja mtaweza kupata suluhu. Suluhu inapokosekana, ni ishara kuwa hamko tayari kufunga pingu za maisha.

4. Hauna ndoto za maisha yenu pamoja baada ya harusi
Watu wengi hufurahishwa na harusi na kuyafumbia macho maisha baada ya ndoa. Ikiwa hauna maono ya maisha yenu pamoja baada ya kufunga ndoa. Hiyo ni ishara kuwa haujayafikiria maisha yenu pamoja kwa kina.
5. Wewe ni mgumu kusamehea
Watu wanapoishi pamoja, ni vigumu kuto vurugana. Mara kwa mara mtakosania vitu vidogo na mchumba wako. Huenda mchumba wako akasahau kutupa takataka kwenye pipa na badala yake kuacha jikoni. Ikiwa hauko tayari kumsamehea mara kwa mara hata anapofanya vitu vinavyokaa vya kitoto machoni mwako, hauyuko tayari kufunga ndoa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Faida Ya Kufanya Tendo La Ndoa Wakati Wa Ujauzito