Utakapo zingatia siri hizi, utajua kuwa kuwaelewa wanawake sio vigumu kama watu wanavyosema. Kuna vitu ambavyo mwanamke hufanya pale tu anapompenda mwanamme. Tazama ishara kuwa mwanamke anakupenda tunazoangazia.
Ishara kuwa mwanamke anakupenda

- Kuzungumza nawe siku nzima
Mwanamke anapompenda mwanamme, ni vigumu kwake kwenda siku nzima bila kuzungumza na mwanamme anayempenda. Mwanamke anapokupenda, atakujulisha kuhusu kila kinachofanyika kwenye siku yake, hata mambo madogo.
2. Anayapa mahitaji yako umakini
Wanawake wanapopenda huwa makini kujua vitu ambavyo wapenzi wao wanapenda na mahitaji yao. Ikiwa kwa kweli anakupenda, mara kwa mara atakununulia zawadi. Hasa ya kitu ambacho umekuwa ukikitamani kwa muda. Ikiwa lugha yako ya mapenzi ni zawadi, bila shaka utazawadiwa vitu vingi.
3. Anakuambia siri zake
Hakuna watu wambea kama wapenzi wawili. Iwapo mwanamke kwa kweli anakupenda, atakwambia siri zake asizoambia watu wengine. Mwanamke anapoanza kukuambia vitu vya kisiri kuhusu maisha yake, bila shaka anakupenda kwa kweli.

4. Kutaka kuwa nawe wakati wote
Iwapo mwanadada huyo amekupenda, atataka kuwa nawe wakati wote. Unapomdokezea kuwa ungetaka kuondoka na kujumuika na marafiki wako, ataanza kukasirika ovyo. Kwani angependa muwe pamoja kwa muda zaidi, hata kama mmekuwa pamoja siku nzima. Hataki kukuwachilia uende zako.
5. Kutabasamu nawe
Mwanamke anayekupenda hutabasamu nawe mara kwa mara. Ni ishara kuwa anahisi ako salama anapokuwa karibu nawe. Mwanamke asipohisi salama kando ya mwanamme, ni vigumu kwake kutabasamu.
Wanaume wengi hudhani kuwa ni vigumu kumwelewa mwanamke. Ukweli ni kuwa, ni rahisi sana kumwelewa mwanamke. Anapokupenda, utaona ishara kupitia kwa matendo yake. Kabla ya kusema kuwa anakupenda, matendo yake yatakuwa yanaonyesha kuwa bila shaka angependa kuwa nawe.
Mwanamke anayekupenda atakupa muda wake, kutabasamu kwa sana nawe, kukuambia siri zake, kutakata kuwa nawe wakati wote na kuyapa mahitaji yako umakini.
Anapojaribu kuzungumza nawe ama kutengeneza muda zaidi wa kuongea nawe, usipuuze. Mbali, tenga muda wako uwezi kuzungumza naye pia.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Je, Nitaweza kubaini vipi kati ya Mapenzi Bandia na ya Kweli