Ishara 6 Wazi Kuwa Mwanamme Anataka Kukuoa

Ishara 6 Wazi Kuwa Mwanamme Anataka Kukuoa

Wanaume wanajulikana kwa kuto wajuza watu kinacho endelea ama kinacho wasumbua. Mchumba wako anapo anza kukueleza kinacho msumbua ni ishara kuwa angependa kukuoa.

Dunia imebadilika na mengi pia yame badilika. Tabia na mitindo ya maisha pia imebadilika. Na kufanya iwe vigumu kubainisha kilicho cha kweli na kisicho cha ukweli kati ya tabia za watu hasa katika mapenzi. Ila, usiwe kasi kufanya uamuzi kuwa mwanamme hayuko tayari kukuweka pete. Baadhi ya wakati hasa kwa mapenzi ambapo wanandoa wamekuwa pamoja kwa wakati mrefu, huenda wanawake wakashindwa kuona ishara kuwa mchumba wako anataka kukuoa.

Ni rahisi kufikiria kuwa mwanamme hapangi maisha yenu pamoja, lakini usiwe kasi kufanya uamuzi huu.

Ishara kuwa mchumba wako anataka kukuoa

ishara kuwa anataka kukuoa

Picha: Shutterstock

 

  1. Hana siri

Kawaida ya wanaume ni kujiwekea mambo mengi, na hata kama sio kuyaficha, hatayaweka siri nawe. Lakini anapo anza kukueleza kinacho endelea maishani mwake, bila shaka ni ishara kuwa ana kuamini na angependa kusikia maoni yako kuhusu mambo tofauti. Hii ni ishara kuwa angependa kuishi maisha yake nawe.

2. Anakwambia kuwa angependa kukuoa

Ni watu wacheshi tu wanao kuwa na mzaha na kufunga ndoa. Lakini kama unamfahamu mchumba wako vyema na kamwe hana mzaha, anapo kwambia kuwa angependa kufunga ndoa nawe, bila shaka hilo ndilo wazo lake.

3. Anapanga maisha ya usoni nawe

Anapo anza kukuhusisha katika mipango yake ya siku za usoni na kukuuliza maoni yako kuyahusu kwa sababu usemi wako ni muhimu, hiyo ni ishara kubwa kuwa angependa kufunga pingu za maisha nawe.

4. Hakuwachi hata mambo yanapo kuwa magumu

how to get married in nigeria legally

Kitu moja kilicho maarufu na aina zote za uhusiano ni nyakati ngumu na changamoto baada ya wakati. Ikiwa mchumba wako hakimbii na kukuwacha peke yako mambo yanapo kuwa magumu, kamwe hatakuwacha.

5. Ana andamana nawe kila mahali

Ikiwa mwanamme hakutaki ama anataka muwe pamoja kwa kipindi kifupi, dalili ni kama vile kukuona pale tu anapo kuhitaji. Kamwe hata andamana nawe panapo kuwa na watu wengi ama jamaa na marafiki zake. Ilhali mwanamme anapo ona maisha marefu nawe, ata ringa kuwajulisha marafiki wako kukuhusu.

6. Anachukua muda kuwa nawe

Ikiwa wewe ni wa maana kwake, ata tenga muda kuwa nawe, kwani ana taka kukujua zaidi na kufahamu yanayo kupendeza na yasiyo ili afanye kinacho stahili kushinda mapenzi yako.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio