Nani ana uwezo wa kutueleza siri za kutoka nje, kuliko mtu ambaye amekuwa mwanamke huyo mwingine? Clare mwanamke wa miaka 29, aliye tengana na mpenzi wake ambaye alikuwa na bibi, anataka kuwasaidia wanawake kufahamu ishara kuwa bwana yako anatoka nje.
"Sikuwahi dhania kuwa ningekuwa mwanamke huyo mwingine - nachukia wazo wa kuchukua mume wa mwanamke mwingine. Nilidanganywa na kujipata mchumba wa mwanamme aliye kuwa amefunga ndoa," alieleza. Na amini kuwa wanaume hutoka nje kwa sababu wana fika katika hatua wanapo shangaa ama hayo ni yote na wanataka kupima uume wao.
Alihisi kuwa na lawama kwa kuwa katika uhusiano na mume na baba wa watoto wawili. Aliye mweleza kuwa ndoa yake ilikuwa imeisha. "Nime jiahidi kuwa kamwe sitarudi kuwa mwanamke huyo mwingine tena. Kwani uhusiano wake na mwanamme aliye kuwa ameoleka uliisha vibaya sana na akabaki amefilisika kimawazo. Ila, nina furaha naweza kuwasaidia wanawake wengine kugundua ishara za kuwaonya.
Ishara kuwa bwana yako anatoka nje

- Kufika usiku kila mara
Unajipata mara kwa mara ukienda kulala bila mchumba wako? Ikiwa mchumba wako anapenda kubaki sebuleni mara nyingi wakati ambapo kila mtu ameenda kulala, huenda akawa na vitu ambavyo angependa kuweka siri. Ila, huenda pia akawa anafanya kazi ama anataka usiri wake. Hakikisha haupuuzi ishara za kitendo cha kuwa na mchumba mwingine.
2. Kubadili mitindo yake ya matumizi
Wachumba walio na wenzi wengine nje hujihusisha katika mitindo ya kutumia pesa zaidi. Huenda akapata kadi nyingine ya matumizi bila ufahamu wako. Pia, kuwa mwangalifu kugundua ununuzi wa vitu ghali. Tuna uhuru wa kutumia pesa tulizo tafuta kwa jasho, ila kama wanandoa, unapaswa kumfahamisha mchumba wako kuhusu mitindo yako ya ununuzi. Ili isije ika athiri ndoa yako.
3. Mabadiliko katika ladha yake ya nyimbo
Huenda ukapuuza ishara hii, lakini mwanamme ambaye kwa kasi anabadili nyimbo anazo penda kusikiza, huenda akawa ameathiriwa na mwanamke mwingine. Kujaribu kumpendeza mwanamke anaye penda aina fulani ya nyimbo. Sio lazima ishara hii kuwa kwa wanaume wote, la, lakini kuwa makini.
4. Kuficha simu yake

Hii ndiyo ishara iliyo maarufu zaidi na mara nyingi huwa ni ukweli. Unapo ona kuwa mume wako kwa ghafla tu ameanza kuficha simu yake ama kuficha apps fulani, kuna ashiria kuwa kuna mambo anayo kufichia na hawezi penda ujue. Hata kama kila mtu anastahili kuwa na ubinafsi wake, usipuuze ishara hii.
5. Kujitenga kihisia
Kamwe hakuelezi kinacho fanyika maishani mwake ama kuhusu hisia zake. Hata mnapo bishana, hataki kuzungumza nawe na kutatua masuala yenu. Hii ni ishara kuwa huenda akawa na mchumba mwingine, ama ana jambo linalo msumbua.