Jinsi Ya Kujua Iwapo Mtoto Wako Ameanza Kufanya Ngono

Jinsi Ya Kujua Iwapo Mtoto Wako Ameanza Kufanya Ngono

Watoto wanapo anza kukomaa, huenda mara kwa mara wakafanya uamuzi usiofaa. Usiwa laumu kwani wanaanza kuwa makini zaidi na mili yao na homoni za ngono zinaanza kukua. Maendeleo ya kiteknolojia kwenye dunia imehakikisha kuwa watoto wanapata ujumbe ambao hapo awali haukuwa. Kama mzazi anaye taka kuwaongoza watoto wake kufanya uamuzi unaoafaa, hapa kuna ishara kuwa mtoto wako anafanya ngono.

Ishara kuwa mtoto wako anafanya ngono

Ask your teenager

Watoto wanapo anza kufanya ngono, kuna ishara kwa tabia zao zitakazo kujuza. Ili kujua bila fiche, hizi ndizo hatua ambazo unaweza fuata na vitu vya kuangalia.

  • Mwulize mtoto wako

Kufanya watoto wako wakuogope sio njia nzuri ya kuwalea. Mojawapo ya njia ya kujua iwapo watoto wako wanafanya ngono ni kuwauliza. Walakini, lazima uwe makini na maneno unayo yatumia. Na uwe tayari kujibu maswali. Iwapo utawauliza kwa njia yoyote ya kuogofya, huenda waka kuficha.

  • Angalia ishara za matendo ya kingono

Kuwepo kwa mipira ya kondomu ama tembe za kuthibiti ushalizaji ni ishara ya matendo ya ngono. Haimaanishi kuwa wanafanya ngono, ila ni ishara ya kuongea na wao. Iwapo utapata moja wapo ya hizi, ina maanisha wanapata ujumbe kutoka mahali na unahitaji kuhakikisha kuwa wanaongozwa ipasavyo.

  • Kuvalia nguo za kuvutia

ishara kuwa mtoto wako anafanya ngono

Wakati mwingi watoto hupenda uangalifu. Hii ni kwa sababu katika hatua hiyo wana anza kuwa makini na mili yao, wanavyo kaa. Huenda wakaanza kuvalia nguo zinazo wafanya wahisi na waonekane warembo zaidi kwa njia ya kuvutia.

  • Mienendo isiyo eleweka

Watoto wanapo anza kuhusika na matendo ya kingono, wana anza kuwa na siri nyingi. Hii ni kwa sababu wanataka kuhakikisha kuwa haugundui chochote wanacho kifanya. Kutakuwa na baadhi ya mienendo isiyo na sababu kamili. Huenda wakaanza kufika nyumbani wakiwa wamechelewa kuliko kawaida na kuanza kuficha mambo wanayo yafanya na hata kuficha simu zao wanapo pigiwa.

  • Kufeli shuleni

Moja kati ya sababu ambazo watoto hufeli shuleni ni kuhusika katika matendo ya kingono. Na kwa sababu hii wana shauriwa kukaa mbali na matendo haya hadi pale ambapo wanapo komaa. Ngono inatumia hisia na akili zako na kuingilia kati ya masomo yako. Na kwa sababu hii kusababisha kufeli katika masomo.

  • Husika

Kama mzazi, unapaswa kuwa mtu ambao watoto wako wanaweza zungumza naye kuhusu kitu chochote. Iwapo unahusika kwa maisha yao katika kila kitu, watakuwa huru kukuelezea kinacho endelea maishani mwao. Pia wanaweza kuambia kuhusu marafiki wao wa jinsia tofauti. Na ni rahisi kwako kukaa chini na kujadili wanacho pitia na kuwaeleza kuhusu afya ya ngono.

Hatimaye

ishara kuwa mtoto wako anafanya ngono

Masomo ya ngono ni muhimu sana unapo walea watoto. Punde tu mtoto wao anapo anza kuelewa mambo, lazima uanze kuzungumza naye kuhusu ngono na njia zinazo faa. Kumwambia mtoto wako akae mbali na watoto wa jinsia tofauti haitoshi. Pia, huwezi washtua vijana kwa kuwaambia hivyo tena ama kusema "mwanamme anapo kugusa unapata mimba." Mtandao umejazwa na jumbe za ngono na hata picha za watu wakiwa uchi na pia ujumbe unao weza kuwasaidia kufanya uamuzi unaofaa. Jukumu lako kama mzazi ni kuwa ongoza kwa njia inayo faa. Kwa kupitia kwa masomo ya ngono, unaweza wajulisha kuhusu magonjwa yanayo sambaa kwa kupitia kwa ngono. Pia, watafahamu jinsi ya kukumbana na tabia za kingono na kuangazia hisia zao wakati wote.

Soma pia: Sex Education: Helping Your Kids Through Their Adolescence

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio