Kukua katika familia ambapo wazazi walikuwa wanagombana kila siku, kuwa na wazazi wasioelewana katika jambo lolote, ama kushuhudia mvutano kati ya wazazi ni baadhi ya sababu zinazo wafanya watu waamue kutofunga ndoa kamwe. Utajuaje iwapo unaogopa ndoa? Kuangazia ishara kuwa unaogopa ndoa kutakusaidia kufahamu msimamo wako katika ndoa.
Watoto waliokua kwenye familia zilizokuwa na matatizo mengi na mahitaji yao ya kihisia kutotoshelezwa huenda wakatatizika katika maisha yao ya uchumba. Huenda baadhi yao wakafanya uamuzi wa kuishi peke yao bila wachumba. Kuna sababu nyingi tofauti zinazowafanya watu kuamua kamwe hawataki kuingia katika ndoa.
Ishara kuwa unaogopa ndoa

- Kuhofia kuingia katika uhusiano wa kipekee
Fikira za kuishi maisha yako yote na mtu mmoja zinakujaza kiwewe. Unahofu ya kuingia katika uhusiano wenye matumaini ya ndoa. Kila uhusiano unapoanza kuwa wa kindani, unamwacha mpenzi wako.
2. Ndoa za watu wengine zinakushtua
Unapokuwa na malengo ya kufunga ndoa siku moja, unatabasamu unapowaona wanandoa wenye furaha. Jambo hili huwa tofauti kwa watu wasiolenga kuingia katika ndoa ama wanaoogopa ndoa. Unapowaona wanandoa wengine, unahofia, hauna himizo la kuwa kama wao siku moja.
3. Kuhisi unazidiwa
Unapojumuika na watu walio katika ndoa, walio kwenye mahusiano yanayoelekea kwenye ndoa ama kwenda kwenye maharusi, unahisi unazidiwa. Hisia inayokufanya uogope kuchukua hatua kuingia katika ndoa. Huenda ukachukia kuenda kwenye maharusi ama kuwa miongoni mwa watu walio katika ndoa.

4. Unapenda kukaa peke yako
Watu wanaolenga kuwa katika ndoa siku moja huingiliana na watu mara kwa mara. Wataenda kwenye sherehe na mahali pa umma ili kuongeza nafasi zao za kupatana na watu wa jinsia tofauti ambao wanaweza kuwa katika uhusiano nao siku moja. Watu wasio na malengo ya kufunga ndoa hupenda kubaki peke yao, bila kujihusisha na watu wengine.
5. Una furaha zaidi
Ikiwa kazi, masomo ama biashara yako inakupa furaha na unahisi kuwa umetimiza malengo yako, hauoni haja ya kuwa na mtu ama kufunga ndoa na mtu bila sababu yoyote. Huenda ukahofia kuwa, kuwa na mchumba ama kufunga ndoa kutapunguza furaha yako.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Kyallo Kulture: Betty Kyallo Na Dada Zake Wana Kipindi Kuhusu Maisha Yao