Hakuna anayependa kuzeeka, ila, hakuna anayeweza kuhepa uzee. Kuna vitu ambavyo vimekuwa vikitendeka na kila mara unajiuliza kama umezeeka kisha kutupilia mbali wazo hilo kwa sababu hutaki kukubali kuwa unazeeka. Ishara kuwa unazeeka unazopuuza wakati wote.
Ishara kuwa unazeeka
- Unapendelea kulala kuliko kwenda kujivinjari

Kuna wakati ambapo hungekosa kwenda sherehe. Wewe ndiye ulikuwa maisha ya sherehe, kila mahali kulipokuwa na sherehe, hungekusokena. Lakini kwa sasa, hauna nishati ya kwenda nje. Huenda wakati mwingine ukawadanganya marafiki wako kuwa una kazi, ili usitoke nyumbani na upate muda wa kulala. Kufika nyumbani ili ulale ndiyo furaha yako siku hizi.
2. Kuhisi maumivu kwenye viungo vya mwili unapodensi
Kuna wakati ambapo ungesakata densi usiku mzima kisha kwenda sherehe siku iliyofuata. Ila kwa sasa, baada ya kwenda sherehe kwa masaa machache, unahitaji siku mbili za kuutuliza mwili. Unahisi uchungu kwenye viungo vya mwili sawa na mtu aliye kuwa akilima siku nzima. Tunachukia kukatiza furaha yako, lakini, kubali unazeeka.
3. Unaongeza uzito kwa kasi na kutatizika kuupoteza

Unapokuwa mchanga, unaweza kula chochote kwani unaweza kukata uzito wa zaidi kwa kasi. Huenda watu wengine wakakosa kuongeza uzito licha ya kula vitamu tamu vingi. Kwa sasa, unakula vipande vichache vya mkate na uzito wako kuongezeka maradufu. Kuupoteza ni shida, inakuchukua muda mrefu zaidi. "Hakuna aliye ni tayarisha kwa upande huu wa kuzeeka". Wewe hujipata ukiwaza wakati mwingi.
4. Hauna pesa wakati wote

Unakumbuka ulivyowashangaa wazazi wako walipokwambia kuwa hawana pesa? Ulidhani kuwa wanakudanganya na kukunyima pesa. Ila sasa hivi unashangaa jinsi walivyoweza kufanya vitu vingi na pesa kidogo walizokuwa nazo. Pia, unajipata bila pesa zozote wakati mwingi.
5. Kulala mapema
Siku ambazo ungelala asubuhi ukiongea na marafiki wako, kutazama runinga ama sinema. Sasa hivi, unataka kufika nyumbani, ukoge, ule kisha ulale. Kufika nyumbani mapema ni lengo lako la kwanza, kuingia kitandani la pili.
6. Unapenda amani na utulivu

Unapenda kuwa mahali palipo tulia na pana amani. Marafiki na wapenzi unaowachagua pia ni watu wenye amani na wala sio vurugu. Uko makini zaidi kuchagua marafiki wako. Kwa wachumba, unataka watu walio maliza michezo ya kuwa na kila mtu, unataka mtu anayefahamu anachotaka.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Kupata Watoto Baadaye Maishani Kuna Manufaa?