Kuna usemi maarufu kuwa, " Mwanamme yeyote anaweza kuwa baba, lakini inachukua mwanamme kamili kuwa mzazi." Kuwa baba kuna maana kuwa wewe ndiye nguzo ya nguvu, kuegemezwa na nidhamu. Je, ishara za baba mwema ni zipi? Na vipi unaweza kuwa mmoja?
Sawa na kuwa mama, jukumu la kuwa baba linahitaji juhudi zisizoisha, lakini kuna fanaka nyingi kuona mtoto wako akikua kuwa mtu mzima. Tazama baadhi ya vidokezo vya kukusaidia kuwa baba anayependwa na watoto wake!
Ishara za baba mwema

- Patia familia yako kipau mbele ikilinganishwa na kazi yako
Jukumu la kulisha familia yako ni mojawapo ya majukumu ambayo baba huchukulia kwa kina. Walakini, kazi inaweza chukua muda wako mwingi ambao unaweza kutumika na watoto na bibi yako.
Kama baba, unaweza kuwa na juhudi na kuwa bora katika uyafanyayo, lakini kumbuka kuwa familia huja kwanza, wakati wote. Fanya kazi unapokuwa kazini na usibebe kazi za ofisini kuzimalizia nyumbani. Ili upate wakati tosha wa kuwa na familia yako.
2. Husika katika masomo na michezo ya mwanao
Baba mwema siye anayewajibika kuwalisha watoto wake tu, mbali anachukua hatua zaidi katika kuhakikisha kuwa amehusika katika kazi zote za watoto wake. Kuwajulia jinsi siku yao nyumbani ama shuleni ilivyokuwa. Kwa kuwasaidia kufanya kazi za ziada pamoja, kucheza nao baada ya kazi. Ni muhimu kwa baba kuuliza maswali haya.
Siku yako shuleni imekuwa vipi leo?
Umepata marafiki wapya shuleni?
Mwalimu alifunza nini leo?
Je, unapendelea somo gani zaidi?
Hakikisha kuwa, unamsaidia mke wako kuwalaza watoto. Wasomee hadithi kabla ya kulala kisha uombe nao.
3. Kuwa na wakati tosha na familia

Mfunze mtoto wako jinsi ya kuendesha baiskeli na kupika. Cheza na vidoli vyake, tazama vipindi vya watoto anavyopenda naye. Onyesha hamu katika vitu anavyopenda kufanya. Kumbuka kuwa unaweza kutengeneza fedha zaidi lakini sio makumbusho yasiyoweza kulipiwa.
4. Wafunze maadili mema
Maadili unayowafunza watoto wangali wachanga ndiyo watafuata hata uzeeni wao. Wafunze kufungulia mabinti milango, kutoa sahani mezani baada ya kula. Baba mwema atafanya kadri awezavyo kuwafunza watoto wake maadili. Kuwa funza kuwa wapole, kuheshimu watu na kutokata tamaa ni maadili muhimu kwa watoto wangali wachanga. Kuwa mfano mwema wa kuigwa. Kumbuka kusisitiza nidhamu kwa watoto wako, waelewe sawa na mbaya wangali wachanga. Kutumia maneno kama, pole, shukrani, niwie radhi ni muhimu.
5. Mpende na umheshimu mama yao
Je, unasaidia mkeo na kazi za kinyumbani kama kuwalisha watoto, kuwalaza ama kupika? Je, unambusu bibi yako kabla ya kwenda kazini? Ikiwa jibu la maswali haya ni "ndiyo", wewe ni baba mwema! Ulezi sio rahisi na huchukua muda na nishati nyingi, kutoka kwako na bibi yako. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa unamsaidia bibi yako ili asiwe amechoka wakati wote. Wakati mwingine, mpe muda afanye vitu anavyovipenda ama apumzike.
Chanzo: Independent
Soma Pia: Kwa Nini Watoto Wengi Hupendelea Kuwa Na Mama Zao Na Wala Sio Baba