Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ishara Za Kansa Unazopaswa Kujua Kuhusu

3 min read
Ishara Za Kansa Unazopaswa Kujua KuhusuIshara Za Kansa Unazopaswa Kujua Kuhusu

Kufahamu ishara za kansa kunakusaidia kujua wakati unapo paswa kwenda kwenye kituo cha hospitali kufanyiwa vipimo.

Ugonjwa wa kansa umekuwa maarufu sana. Ni vyema kufahamu ishara za kansa na wakati unapopaswa kwenda kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo.

ishara za kansa

  • Doa kwenye ngozi

Kuwa na doa kwenye ngozi inayobadilika saizi, shepu na rangi huenda ikawa ishara ya saratani ya ngozi. Huenda ikawa doa hii ni tofauti na doa zingine mwilini mwako. Unapogundua kuwa una ishara zisizo za kawaida, ni vyema kukaguliwa na daktari wa ngozi. Vipimo vya ngozi hutoa seli kidogo za uso ili kubaini iwapo kuna seli za saratani zinazokua.

  • Mabadiliko kwenye matiti

Mabadiliko kwenye matiti mara zote sio kufuatia saratani. Hata hivyo, mwanamke anapaswa kujikagua mara kwa mara kwa kugusa matiti yake kuona iwapo kuna uvimbe. Ishara za hatari ni kama uvimbe, mabadiliko kwenye chuchu, kuhisi uchungu ama chuchu kuwa nyekundu.

  • Kukohoa

Kwa watu wasiovuta sigara, kuna kiwango cha nafasi kuwa, kuwa na kikohozi kisicho isha ni ishara ya saratani. Kikohozi huenda kikasababishwa na maambukizi ama astham. Kinapozidi kwa muda mrefu na kuanza kukohoa damu, unapaswa kuenda kwenye kituo cha afya. Vipimo vitadhibitisha iwapo una saratani ya mafua.

  • Uchungu kwenye koo

Kuhisi uchungu kwenye koo unapomeza chakula ama vinywaji mara nyingi husababishwa na baridi ama aina fulani ya dawa. Ni vyema kutembea kwenye kituo cha afya. Kutatizika kumeza vitu huenda ikawa ni ishara ya saratani ya koo. Vipimo vitabaini iwapo ni tatizo la kawaida ama kwa kweli una saratani inayokua.

  • Uvimbe ama kufura tumbo

Kufura tumbo husababishwa na kuwa na mawazo mengi ama lishe hafifu. Ishara hii inapoambatana na uchovu, kuhisi mnyonge, kukata uzani na uchungu kwenye mgongo, ni vyema kufanyiwa vipimo. Kuhisi uvimbe mara kwa mara katika wanawake huenda ikawa ishara ya saratani ya ovari.

  • Kuvuja damu kusiko kwa kawaida kutoka kwa uke

Kuvuja damu na sio hedhi mara nyingi huhusishwa na kuwa na fibroids ama kutumia aina ya uzazi wa mpango. Unapovuja damu ovyo bila kufahamu chanzo, ni vyema wakati wote kuwasiliana na daktari ili vipimo vifanyike kubaini chanzo cha tatizo lile.

  • Kukata uzani kwa kasi

ishara za kansa

Mojawapo ya ishara maarufu za kansa ni kukata uzani kwa kasi. Kuna sababu zingine ambazo huenda zikamfanya mtu kukata uzito wa mwili. Kama unapoanza kufanya mazoezi na kula lishe bora, ila, uzani utakuwa wenye afya. Unapoanza kupunguza uzito kwa kasi bila chanzo, ni vyema kuwasiliana na daktari.

  • Damu kwenye mkojo

Kuona damu unapoenda msalani sio jambo la kawaida. Kwa hivyo unapoenda msalani kisha uone damu ama uvimbe, kuna nafasi huenda ukawa unaugua saratani ya koloni ama ya kibofu.

Soma Pia: Unaufahamu Ugonjwa Wa Listeria Katika Ujauzito?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Ishara Za Kansa Unazopaswa Kujua Kuhusu
Share:
  • Athari Hasi Za Bhangi Kwa Uzalishaji Wa Kiume

    Athari Hasi Za Bhangi Kwa Uzalishaji Wa Kiume

  • Sababu Kwa Nini Sukari Nyingi Ina Athari Hasi Kwako

    Sababu Kwa Nini Sukari Nyingi Ina Athari Hasi Kwako

  • Vyanzo vya Uvimbe Baada ya Kujifungua na Jinsi ya Kuupunguza

    Vyanzo vya Uvimbe Baada ya Kujifungua na Jinsi ya Kuupunguza

  • Athari Hasi Za Bhangi Kwa Uzalishaji Wa Kiume

    Athari Hasi Za Bhangi Kwa Uzalishaji Wa Kiume

  • Sababu Kwa Nini Sukari Nyingi Ina Athari Hasi Kwako

    Sababu Kwa Nini Sukari Nyingi Ina Athari Hasi Kwako

  • Vyanzo vya Uvimbe Baada ya Kujifungua na Jinsi ya Kuupunguza

    Vyanzo vya Uvimbe Baada ya Kujifungua na Jinsi ya Kuupunguza

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it