Fahamu Ishara Hizi Za Kuabisha Katika Mimba Zinazo Mtendekea Mama Mjamzito

Fahamu Ishara Hizi Za Kuabisha Katika Mimba Zinazo Mtendekea Mama Mjamzito

Tazama baadhi ya mambo katika ujauzito yanayo mfanya mama mjamzito kuhisi aibu yanapo tendeka akiwa mbele ya watu.

Mimba hubadilisha mwili, maisha na mtindo wa maisha yako. Utahisi uchovu zaidi kwani sasa hivi una kiumbe kinacho kua tumboni mwako. Mbali na ishara zilizo maarufu za kuwa na mimba, kama vile kuwa na hamu iliyo ongezeka ya kula vyakula fulani huku ukichukia vingine. Kuna ishara za kuaibisha katika mimba utakazo shuhudia na ambazo hauku tarajia. Makala haya yana zungumza kuhusu ishara zaidi za ujauzito ambazo wanawake hupitia, ila sio wengi wanao zungumza kuzihusu.

Kumbuka kuwa hiki ni kipindi tu na kitaisha kabla ufahamu. Kwa hivyo, usione aibu unapo pitia baadhi ya mambo haya katika safari yako ya ujauzito. Tazama baadhi ya ishara zaidi za kutaraji.

Ishara Za Kuabisha Za Ujauzito

ishara za ujauzito

  • Kuwa na hewa nyingi zaidi (kuharibu hewa)

Kuhisi kuwa una hewa nyingi ni kawaida katika ujauzito na wanawake wengi hushuhudia haya. Mimba huja na ongezeko la homoni mwilini na kupunguza uchakataji wa chakula tumboni. Huenda ukashindwa kungoja hadi unapofika msalani na kuharibu hewa mbele ya watu. Ni vigumu kudhibiti misuli yako katika ujauzito na hii ndiyo sababu inayo kufanya kushindwa kujizuia kuharibu hewa.

Unaweza punguza kuwa na hewa nyingi tumboni kwa kufanya mazoezi na kuwa makini na lishe yako. Kufanya mazoezi kunasaidia chakula kusonga kwa kasi kwenye mfumo wako wa utumbo. Kuwa makini kuhusu vyakula unavyo kula kwani kuna vyakula vilivyo na gasi nyingi ikilinganishwa na vingine. Kama vile maharagwe, vinywaji kama soda, matunda yaliyo kaushwa na broccoli.

  • Kuenda haja ndogo kama umesimama

Sio jambo geni kwa mwanamke mjamzito kuchemua kisha kushtukia kuwa amejiendea haja ndogo akiwa amesimama. Hata mbele ya watu ama anapo kuwa kwenye foleni. Hata kama sio kiwango kikubwa cha mkojo, wanawake wanao yapitia haya baada ya kukohoa, kuchemua ama kucheka huona haya.

Wataalum wanawashauri wanawake kuvalia panty liners kuepuka aibu nyingi wanapo jichafua wakiwa miongoni mwa watu. Kuenda msalani unapo hisi haja bila kukawia pia kuna saidia.

  • Nywele kwenye uso

Wanawake wengi huwa na furaha wanapo pima mimba na kupata matokeo chanya. Wana furaha isiyo na kifani kwani baada ya miezi tisa wata itwa mama. Furaha hii hupungua wanapo juzwa kuwa, huenda pia wakaanza kumea nywele kwenye uso, hasa juu ya mdomo. Watu mashuhuri kama vile Adele alishuhudia ishara hii alipokuwa mjamzito.

Bahati nzuri ni kuwa, hili ni tatizo ndogo na kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia kukumbana na tatizo hili kama vile waxing ama tweezing. Mbinu hizi ni salama katika ujauzito na haum hatarishi mtoto wako.

  • Harufu mbaya

Ongezeko la uwezo wa kunusa na kuonja ni maarufu katika mimba. Huenda ukaanza kuchukia vyakula fulani na kuhisi kutapika unapo nusa vitu kama kitunguu ama marashi. Kadri mimba yako inavyo zidi kukua, hasa katika miezi ya mwisho, baadhi ya wamama huanza kujinusa uke. Huenda ikawa ni kufuatia ongezeko katika utoaji wa kamasi la uke. Jambo hili linaweza kutia wasi wasi na kukufanya ubebe karatasi za kujipanguzia kila unapo safiri. Usiwe na shaka, hauna harufu mbaya, ila ni uwezo wako wa kunusa ulio ongezeka. Unapo ona mabadiliko kwenye uchafu wa ute wako, wasiliana na daktari wako bila kukawia.

  • Upele kwenye uso

ishara za ujauzito

Baadhi ya wanawake hushuhudia ongezeko la upele kwenye uso katika trimesta ya kwanza. Homoni nyingi mwilini zina sababisha tatizo hili. Kuna bidhaa za kunawa uso zinazo punguza acne hii na hazina athari hasi kwenye afya ya mama ama mtoto. Lakini mama mjamzito ana shauriwa kuwasiliana na daktari wake kabla ya kutumia bidhaa zozote zile.

Soma pia: Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Written by

Risper Nyakio