Ishara Za Kumjuza Mama Kuhusu Kuharibika Kwa Mimba

Ishara Za Kumjuza Mama Kuhusu Kuharibika Kwa Mimba

Mama anapo kuwa na mimba ama kutarajia kutunga mimba, anapaswa kuwa na maarifa mengi kadri iwezekanavyo kuhusu mambo tofauti yanayo husika na ujauzito. Kufahamu vitu tofauti kutamjuza wakati ambapo mimba inakua ipasavyo na wakati ambapo kuna taswishi. Dalili mojawapo inayo ashiria kuharibika kwa mimba ni kutoka damu nyingi. Mama pia huhisi uchungu mwingi tumboni.

Mimba inapo haribika, kiwango cha damu nyingi kinatoka na ni tofauti na damu ya kawaida ama damu ya hedhi. Mambo mengi yana badilika katika maisha ya mama anapo poteza mimba.

Ishara za kuharibika kwa mimba

kuharibika kwa mimba

  • Kutokwa na damu jingi. Kiasi zaidi kinacho lowesha pedi zaidi ya moja kwa muda katika ama chini ya lisaa limoja
  • Uchungu mwingi tumboni
  • Kuhisi kana kwamba upande mmoja wa tumbo umekufa ganzi

Japo kuwa kutokwa na kiasi kidogo cha mimba ni kawaida katika chanzo cha mimba, ni vyema mama kuwa makini. Unapo gundua kuwa unahisi uchungu mwingi tumboni ama kuvunja damu sana, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako bila kusita.

Unapo hofia kuwa umepoteza mimba:

Jambo la kwanza unapo shuku kuwa una mimba ni kuwasiliana na daktari wako. La sihivyo, hakikisha kuwa unaenda hospitalini mwenyewe kufanyiwa kipimo.

Kwa wanawake walio na mimba isiyo zidisha miezi sita, huenda mwuguzi wako aka kushauri kubaki nyumbani ili uone kitakacho fanyika.

Ikiwa mimba yako ina zidisha miezi sita, unahitajika kufanyiwa ultrasound ili kudhibitisha kilicho fanyika.

Utahitaji kutumia taulo ama pedi siku chache kwa sababu ya damu unayo vunja. Daktari ata kupatia dawa za kupunguza uchungu.

kuharibika kwa mimba

Ni muhimu sana kwa mama kuegemezwa ifaavyo katika kipindi hiki. Kwani dhiki huenda ikamfanya kusombwa na mawazo. Mchumba wake ana paswa kuwa naye na kumhimiza na pia kuhakikisha kuwa ako miongoni mwa watu ili asifilisike kimawazo. Ni vyema kwa mama kuzungumza na wanawake walio pitia jambo sawa. Hivi, ataweza kupiga moyo konde na pia kupona kutokana na jambo hilo kwa kasi.

Kufuatia kuharibika kwa mimba, mama anaweza vunja damu kwa kipindi cha wiki moja ama wiki mbili. Hakikisha kuwa una kula vizuri na kuichunga afya yako ya kimawazo, kihisia na kifizikia.

Hakikisha kuwa unaenda hospitalini mara kwa mara kufanyiwa vipimo kuangalia iwapo tishu zote zimetoka mwilini.

Chanzo: WebMd

Soma Pia: Mwongozo Wa Mimba Wiki Baada Ya Nyingine

Written by

Risper Nyakio