Baba Awanyanyasa Kimapenzi Wasichana Wake Wenye Umri Kati Ya 1-5

Baba Awanyanyasa Kimapenzi Wasichana Wake Wenye Umri Kati Ya 1-5

One of the girls had reportedly told her grandmother about the abuse a year ago but no one believed her...

Huenda ukadhania kuwa umeolewa na mtu ukidhani kuwa unamfahamu nje na ndani, lakini unapata kugundua kuwa, wao ni chaguo mbaya zaidi ulilolifanya la kuanza familia nao. Hivi majuzi, mwanamke wa miaka 32, aligundua kuwa mumewe, wa miaka 32, pia alikuwa akiwanyanyasa kimapenzi wasichana wao watatu wadogo. Watoto hawa wenye umri wa mwaka mmoja, mitatu na mitano walikuwa wame lalamika kuwa baba yao alikuwa anawanyanyasa kimapenzi mara kwa mara.  Kwa kuweka vidole vyake kwenye sehemu zao za siri.  Tizama ishara za kunyanyaswa kimapenzi kwa watoto wadogo ambazo zitakusaidia kujua iwapo mtoto amedhalilishwa kimapenzi.

Baba akamatwa kwa kuwanyanyasa kimapenzi wasichana wake

kudhalilishwa

Baba akamatwa baada ya kuwa dhalilisha kimapenzi wanawe

Mama ya watoto hawa aliweza kujua tu baada ya mtoto wa umri wa miaka mitatu kumwambia nyanya yake.

OCPD wa Kajang Msaidizi Ahmad Dzaffir Mohd Yussof alisema kuwa msichana huyu wa miaka mitatu, pia alikuwa amemwambia mamake kuwa baba yake alikuwa amemwingiza kidole kwenye uke na mkundu wake.

“Ufunuo huu uliwawezesha watoto hao wengine kumwambia mama yao kuwa wao pia walikua wamenyanyaswa kimapenzi na baba yao kwa njia sawia,” akasema.  Msichana huyu wa miaka matatu alikuwa amemwambia nyanya yake mwaka mmoja uliopita, lakini hakuna aliyemwamini.

ACP Ahmad Dzaffir alisema kuwa hao watoto watatu walikuwa wamepelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi.

“Daktari waliweza kupata kuraruka katika uke wa watoto hao lakini hakukuwa na ishara ya kunajisiwa kwenye mkundu,” akasema.

Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa miaka minane na walikuwa wamejaliwa watoto wanne akiwemo kijana wa umri wa miaka saba.

Polisi waliweza kumshika baba yao katika makazi yake Oktoba tarehe 25 Sungai Long, Malaysia.

“Alishikwa  na makaratasi ya ujasusi yakapelekwa  kwa naibu wa kiongozi wa mashtaka yakiwa na vidokezo  mshukiwa ashitakiwe  kulingana na kipengele 14(a)  cha Sexual Offences Against Children Act 2017,”akasema.

Ikiwa atahukumiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 na kuchapwa viboko.

Jinsi ya kujua iwapo watoto wako wananyanyashwa kimapenzi

kudhalilishwakimapenzi

Ni jambo la kusikitisha mtoto anapo dhalilishwa kimapenzi

Watoto amabao wananyanyaswa kimapenzi hawatongea kuhusu kile wanacho tendewa, kwani wanahisi ni tendo la aibu.  Pia inaweza kuwa yule anawanyanyasa, anawashurutisha  ama kuwapumbuza kiakili ili wasimwambie yeyote.

Kwa hivyo, utawezaje  kugundua iwapo watoto wako wananyanyaswa kimapenzi.  Hizi ni mojawapo ya ishara za kunyanyaswa kimapenzi kwenye watoto.

Ishara za kunyanyashwa kimapenzi kwenye watoto:

 1. Mabadiliko ya ghafla ya kitabia. Iwapo utagundua mtoto wako amejitenga, anakwamilia ama mwenye hasira hii yaweza kuwa dalili. Pia wanaweza kuwa na wakati mgumu kupata usingizi, ama kuanza kukojoa kitandani, ama kupatwa na jinamizi kwa mara nyingi.
 2. Kuhepa yule mtu anawanyanyasa. Mtoto anaweza kuonyesha dalili za kutompenda anayemnyanyasa, ama ana anza kumwogopa fulani na kuanza kukataa kukaa nao.
 3. Tabia za kujamiana sizisofaa. Watoto ambao wamenyanyaswa kimapenzi wanaweza anza kutumia lugha isiyofaa ama kuonyesha tabia za kimapenzi zisisofaa.
 4. Watoto wengine wanaweza kudokeza kuwa wananyanyaswa kimapenzi. Wengine hata wanaweza kukwambia wazi.  Ni bora kuchunguza na kuto litupilia mbali wanalo lisema.

 

ishara za kunyanyaswa kimapenzi

Adhari Za Kunyanyaswa Kimapenzi Kwa Watoto

Watoto walionyanyaswa kimapenzi wafaa kupata ushauri ili kukomesha mawazo hayo. Pia njia mojawapo ya kukabiliana na hio dhuluma. Hizi ndizo athari kwa watoto walio dhulumiwa kimapenzi:

 1. Mavurugano – mara nyingi watoto hufanywa kufikiria kuwa kunyanyaswa kulikuwa sawa. Kinyume na vile watu wengi hufikiria, si kila kunyanyaswa kimapenzi mwisho wake ni uchungu. Matokeo ni kuwa watoto wanaweza kupoteza fahamu. Na waweza kuchanganyikiwa kati mguso sawa na usio faa. Hawezi elewa kilicho tendeka kwa vile hawakifahamu. Ilikuwa kosa kweli? Hii inanifanya kuwa mchafu?  Nini kitafanyika sasa nimezungumza.  Familia na marafiki zangu watafikiria nini kunihusu?
 2. Hatia – wakati watoto wanafanywa kuamini si tendo mbaya wanaanza kuwaza walishirikiana katika unyanyashaji. Wanaamini uongo kuwa wao ndio wenye hatia na walichangia kwenye dhuluma kwa kuidhinisha kunyanyaswa kimapenzi.   Aibu- hata kama watoto hawatelewa kwa uwazi nini kinachoendela hicho kitendo bado chaweza wafanya wajihisi wachafu na wasio na dhamana.
 3. Woga – wanaonyanyasa hutumia  vitisho na aibu  ili watoto wasiwaambie watu wengine. Cha kusikitisha, itakuwa miaka mingi baadaye kabla waanze kuhisi salama tena.
 4. Huzuni – ikiwa anayemnyanyasa ni familia watoto wanaweza kuhuzunishwa na uhusiano wao kuisha. Ndiyo, uhusiano wa karibu waweza kufanyika kati ya mtoto na anayemnyanyasa.
 5. Hasira – watoto wengine wanaweza kuonyesha hasira kali na isiyodhibitika. Kwa kukosa sauti ya kuongea juu ya unyanyasaji, wanaweza laumu watunzaji kwa kutokomesha ama kutowalinda kutokana na unyanyasaji .
 6. Kuwa hoi – Vile vile iwapo itachukua miaka kabla ya kusahua hilo tendo, pia inamaanisha miaka mingi ya kujihisi hoi. Iwapo itatendeka tena?
 7. Mfadhaiko – wakati hali ya akili ya mtoto wako haijashughulikwa inaweza kuwafanya wajitenge kupoteza mvuto  katika maisha.

Read also: How the underwear rule can protect your kids from sexual abuse

Written by

Risper Nyakio