Mnapoanza uhusiano wenu, mapenzi huwa yamenoga. Ni vigumu kuenda masaa mawili kabla ya kuongea na kujua vitu ambavyo mwingine anafanya. Ila kwa sasa, dhamana yako imepungua. Hausikizwi wala kuheshimiwa kama ilivyo kuwa hapo awali. Tazama ishara za kuondoka kwa uhusiano zinazokuashiria wakati wa kupanga virago vyako na kuondoka kutoka kwa uhusiano huo.
Ishara za Kuondoka Kwa Uhusiano
- Hana hisia kwako tena

Ikiwa mtu ana hisia za kweli kwako, watakutunza kwa njia yoyote ile. Kuhakikisha kuwa uko sawa na hukosi chochote, na kukuegemeza kadri awezavyo. Wanakoma kufanya walichokuwa wakifanya hapo awali. Hawakupigii kuhakikisha kuwa uko sawa wala kukujulia ulivyo, ni ishara kuwa hisia zao kwako zimeanza kufifia. Kitu kidogo kinazua mgogoro usio isha. Huenda wakaanza kukulaumu kwa vitu ambavyo hukufanya.
2. Mna maono tofauti ya kimaisha
Mwanzoni mwa uhusiano, mna maono na maadili sawa. Lakini inafika wakati ambapo unahisi kana kwamba hamkubaliani kwa jambo lolote. Ikiwa hapo awali mlikuwa na kikao kila wiki kuzungumzia uhusiano na maisha yenu, ila kwa sasa mchumba wako hajali. Ikiwa unasikia kuwa kwa kweli mambo yamebadilika, usione haya ama uwoga kuondoka.
3. Hawataki kuzungumza kuhusu yanayokusumbua
Wanapokukosea kisha unawaambia kuwa hujafurahia. Hawaombi msamaha wala kujaribu kuzungumzia vitendo vyao. Mahusiano yenye afya ni ambapo wachumba wanaheshimiana na kutoumizana kimakusudi. Mchumba mmoja anapohisi kuwa haonekani wala kusikizwa wala kuheshimiwa. Uhusiano wa aina hiyo hautafuzu. Kwani mmoja atamchukia mwingine.
4. Unajitolea ila hawathamini juhudi zako

Katika mahusiano yenye afya, kila mchumba hujitolea. Juhudi hutoka kwa pande mbili. Uhusiano wenu unapofika hatua ambapo juhudi zinatoka upande mmoja, ni wakati wa kuondoka. Usijipuuze katika uhusiano ili kumpendeza mchumba wako.
5. Anakudhulumu kifizikia, kingono, kimapenzi ama kihisia
Usiamini maneno ya mtu mbali vitendo vyao. Ikiwa mara kwa mara anakudhulumu kwa njia yoyote ile anapokasirika, ni wakati wa kufunga virago vyako. Usijaribu kuzungumza nao ama kufikiria kuwa utawabadilisha. Unavyoendelea kuzungumza naye na kumkubalia kuendelea kukudhulumu, ndivyo atakavyoendelea kukutesa zaidi. Amani yako na afya ya kiakili ni muhimu kuliko mahusiano yoyote yale.
Soma Pia: Ishara Kuwa Mchumba Wako Wa Awali Anajuta Kukuwacha