Mambo Ya Kutarajia Unapo Poteza Ubikira (Kwa Wake Na Waume)

Mambo Ya Kutarajia Unapo Poteza Ubikira (Kwa Wake Na Waume)

Kwa wanaume, ishara huwa za kihisia zaidi kuliko kifizikia. Katika dunia inayo wahimiza wanaume kujiumba kuwa miungu ya kingono ili kutambulika zaidi kitandani.

Baada ya kufanya ngono mara ya kwanza, wanaume na wanawake wengi mara nyingi hushangaa ikiwa kutakuweko na ishara zozote za kifizikia za kupoteza ubikira wanapo endelea kusonga mbele.

Ubikira ni jambo kuu kwa watu wengi. Huwa na sherehe ndogo kabla ya ngono ya kwanza. Walakini, katika miaka hii ya kuhusishwa na kufahamu kinacho endelea, baadhi ya watu hawaamini jambo hili. Ama kulipuuza kwa kuwa shinikiza watu kuwa ama kuto kuwa na ngono.

Kwa wanawake, mbali na upande wenye hisia wa mambo, mojawapo ya mabadiliko ya kifizikia yaliyo maarufu sana ya kupoteza ubikira huenda ikawa ni ujauzito. Kwa hivyo kama mwanamke anaye vutiwa na jinsia tofauti kabla ya kufanya ngono mara ya kwanza, hakikisha kuwa una mbinu mojawapo ya panga uzazi.

Ishara za kifizikia za kupoteza ubikira kwa wanawake

ishara za ubikira

Kwa wanawake, kuna mabadiliko machache unayo weza kuona baada ya kufanya ngono mara ya kwanza. Ishara hizi ni kama vile.

  • Matiti yako yanakuwa dhabiti kwa muda mfupi

Unapo kuwa na furaha ya kingono, mfumo wako wa neva huwa na furaha pia. Na kufanya mishipa ya damu kupanuka na kufanya matiti yako kuvimba. Tafadhali, kumbuka kuwa udhabiti huu ni kwa muda mfupi tu. Sio kusema kuwa hali hii itadumu maisha.

  • Chuchu zako huwa nyeti zaidi

Unapo anza kufanya ngono, mwili wako huongeza mzunguko wa damu na kufanya chuchu ziwe nyeti. Chuchu zako husimama na kuwa ngumu unapo kuwa na furaha ya kingono na kunaweza kusaidia kufika kilele.

  • Mabadiliko katika uke wako

Kwa sababu kuna shughuli mpya kwenye uke wako, itabadili unyumbufu wake. Lakini huenda ikachukua muda kidogo kabla ya kuzoea kupenywa. Kwa mara ya kwanza, huenda kukawa na uchungu. Hakikisha mmefanya foreplay ya kutosha. Uchungu ukizidi, hakikisha kuwa umemtembelea daktari.

  • Ubongo wako hutoa homoni za kuhisi vizuri

Ubongo wako una uwezo wa kuhisi vizuri na homoni kama vile endorphins na serotonin, oxytocin na dopamine. Homoni hizi zinaweza kufanya kuhisi vizuri na kukufanya uamini mtu unaye fanya mapenzi naye.

  • Mji wa mimba na kisimi zitabadilika

Muda unapo pita baada ya kufanya ngono mara ya kwanza, uterasi yako na clitoris zitazoea na kufahamu jinsi ya kubadilika, kupanuka na kubana.

Ishara za kifizikia za kupoteza ubikira kwa wanaume

ishara za kupoteza ubikira

Kwa wanaume, ishara huwa za kihisia zaidi kuliko kifizikia. Katika dunia inayo wahimiza wanaume kujiumba kuwa miungu ya kingono ili kutambulika zaidi kitandani, shinikizo hili baada ya ngono yako ya kwanza huenda ikawa ya kuchosha sana.

Shinikizo hilo ni kama kuchukua mtihani na kuenda nyumbani kushangaa kama ulitosheleza na kuwacha rekodi nzuri.

Shinikizo hili hukufanya uhisi haja ya kupiku utendaji wako wa wakati ulio pita wakati wowote unapo jipata kitandani.

Je, ubikira wako ni zawadi?

Ubikira wako sio zawadi ya kumhifadhia mtu yeyote. Ubikira wako ni wako peke yako. Ikiwa uta uhifadhi, inapaswa kuwa kwa sababu ambazo uko sawa nazo. Ni uamuzi wako mtu ambaye ungependa kufanya ngono naye wa kwanza.

Katika na baada ya ngono yako ya kwanza, hakuna kitu kilicho andikwa kwa vitabu. Kwa hivyo, baada ya ngono yako ya kwanza, huenda ukaona tabia kutoka kwa mchumba wako zisizo za kawaida. Mpe wakati yaishe.

Soma Pia:Sababu 7 Za Kuwa Hamasisha Wanawake Kwenye Jamii

Written by

Risper Nyakio