Ishara Za Kuwacha Kufanya Kazi Unapokuwa Na Mimba

Ishara Za Kuwacha Kufanya Kazi Unapokuwa Na Mimba

Ulifahamu kuwa kufanya kazi baada ya miezi minane ya mimba ni hatari kama kuvuta sigara? Kuna utafiti kuunga usemi huu mkono.

Hii ni mojawapo ya hali ambapo kila mtu ni tofauti. Baadhi ya wamama huchagua kufanya kazi hadi dakika ya mwisho ili wahifadhi siku za mapumziko ya mimba ya kuwa na mtoto wao anapo zaliwa. Wengine wanachagua siku ya mwisho ili kupumzika kabla ya siku kuu ya kujifungua, ama kufanya mipango ya kufanya kazi kutoka nyumbani siku zao za mwisho. Hakuna jibu hasa kwa swali hili, "ishara za kuwacha kufanya kazi unapokuwa na mimba" ni zipi? Ila, kuna miongozo ya kiafya inayo weza kukusaidia kupanga mapumziko yako ya uzazi. Kuwa hakika kujadili sababu zinazo husishwa na kazi na mimba yako na mtunzaji wako wa kiafya.

Wanawake wengi wanaweza pambana kifizikia na kazi wanazo zifanya hadi karibu wiki 32-34 za mimba. Karibu na wakati huu, wanawake wengi pia wanabadili umakini wao kutoka kazi yao hadi kwa kuwa mama, na huenda ika athiri uamuzi wa wakati wa kuwacha kufanya kazi. Iwapo una biashara, huenda ukataka kungoja hadi mwisho wa mimba yako ili uwache kufanya kazi. Sio hiari mbaya, ila, unapo ona mojawapo ya ishara hizi, koma kufanya kazi na umtembelee daktari wako bila kusita.

Ishara Za Kuwacha Kufanya Kazi Unapokuwa Na Mimba

ishara za kuwacha kufanya kazi unapokuwa na mimba

Baadhi ya kazi huenda zika ongeza hatari za kuwa na mtoto ambaye hajakomaa, kazi zinazo husisha kuinua vitu vizito, kelele nyingi, kusimama kwa masaa marefu. Ongea na daktari wako kuhusu kupata ruhusa kazini. Wanawake walio shuhudia kujifungua kabla ya wakati hapo mbeleni huenda wakafikiria kumaliza kazi yao mapema.

Haijalishi kazi unayo ifanya, kuna baadhi ya ishara za tahadhari za kawaida unazo paswa kuangazia unapo panga kuendelea kufanya kazi. Je, kukosa usingizi usiku kuna athiri utendaji kazi wako? Una hofu kuhusu matayarisho yote ya mtoto wako kuwa tayari nyumbani mwako? Huenda ukawa wakati wa kuanza kufikiria kuwacha kufanya kazi mapema.

1. Unakosa umakini kati kati ya siku.

Kukosa usingizi usiku kuna athiri utendaji kazi wako mchana na kusababisha kulegea, kukasirika na kusahau. Pia, unajipata ukikwaza kuhusu matayarisho ambayo yame tupiliwa mbali yanayo kungoja nyumbani.

2. Kusimama na kukaa hakuna starehe.

Kuumwa na mgongo, kufura miguu, kukosa hewa ni ishara kuwa unahitaji muda wa kupumzika, hasa ikiwa kazi yako inakuhitaji kuwa umesimama wakati mwingi.

3. Una ishara za uchungu wa uzazi wa mapema.

Kuumwa na mgongo upande wa chini, uchungu wa hedhi na madoa ya hedhi yana maana kuwa unapaswa kuangaliwa na daktari bila kusita. Kuna uwezekano mtunzaji wako atashauri upumzike bila kufanya kazi.

Iwapo unahisi hivi siku za mwanzo za mimba yako, ongea na daktari wako kwa sababu una uwezo tosha wa kufanya kazi wakati huu. Ila, ikiwa unashuhudia ishara hizi miezi ya mwisho ya ujauzito wako, koma kufanya kazi na upumzike nyumbani. Kwa sababu, ubongo wa mama ulio na afya unaweza msaidia mtoto kukua kwa kasi ndani yako.

Kama tulivyo sema hapo awali, kila moja kati ya hizi inapaswa kuwa ya kibinafsi na kujadiliwa na daktari wako.

Hali za Kimatibabu Zinazo Hitaji Uwache Kufanya Kazi

ishara za kuwacha kufanya kazi unapokuwa na mimba

Kuna hali fulani ambazo madaktari hushauri uwache kufanya kazi. Baadhi ya hizi huhitaji kulazwa hospitalini na kuangaliwa kwa umakini. Wengine wana kuruhusu kukaa nyumbani. Kila hali inapaswa kuwa ya binafsi na kujadiliwa na daktari wako:

Hapa ni baadhi ya hali za mimba na kimatibabu ambapo madaktari huenda wakashauri kupunguza ama kuwacha kazi:

  • Placenta previa
  • Placenta accreta
  • Premature rupture ya fetal membranes
  • Kufunguka kwa kizazi kabla ya wakati
  • Mapacha na hatari ya kujifungua kabla ya wakati
  • Shinikizo la juu la damu
  • Kujifungua kabla ya wakati hapo awali
  • Fetusi iliyo na intrauterine growth restriction
  • Uchungu wa mama usio komaa
  • Amniotic fluid iliyo punguka 

Kama tulivyo sema hapo juu, kila kati ya hizi inapaswa kuwa ya kibinafsi na kujadiliwa na daktari wako.

Faida za kuwacha, muda kabla ya kujifungua

Kwa wanawake wengi, kufanya kazi wanapokuwa na mimba huenda ikawa sio jukuma. Pengine unafurahia kutoka nje ya nyumba na kuwa na kitu cha kufanya wakati wa mchana.

Hatimaye, utalazimika kuchukua muda wa kupumzika wiki chache za mwisho kwa sababu za kimatibabu. Ila itakuwa na thamana. Tena, uamuzi wa wakati wa kuwacha kazi inalingana na uamuzi wako wa kibinafsi na unapaswa kuwa makini na kufikiria kwa kina wakati wa kupata mimba.

Soma pia: The Symptoms Of Stillbirth And How To Avoid Them

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio