Kuharibika kwa mimba ni kupoteza ujauzito katika ama kabla ya kufikisha wiki ya 20 katika ujauzito. Kuna sababu nyingi zinazosababisha kuharibika kwa mimba. Kupoteza mimba huwa na athari hasi kihisia na kiakili kwa mwanamke. Tazama baadhi ya ishara za mama kupoteza mimba.
Dalili za kuharibika kwa mimba

- Maumivu ya tumbo
Kuumwa na tumbo huwa ishara maarufu zaidi ya kupoteza mimba. Mama huhisi uchungu kwenye tumbo ya chini ama sehemu ya pelviki. Uchungu huu huwa sawa na uchungu wa hedhi, ni vyema kwa mama kukaguliwa upesi.
2. Kutoka damu
Kutokwa na damu ni ishara nyingine ya kuharibika kwa mimba. Damu huenda ikawa ya hudhurungi ama nyekundu iliyokolea. Kwa wanawake wengine, hutokwa na damu nyingi zaidi ya ilivyokawaida katika mimba.
Kuna baadhi ya wanawake ambao hutokwa na damu kiasi kidogo katika wiki za kwanza 12 za mimba.

3. Kupunguka kwa ishara za mimba
Huenda mama akafikiria kuwa hii ni ishara chanya, ila sio hivyo. Kushuhudia kupunguka kwa ishara za mimba kama kutapika, kuumwa na chuchu ama kichefu chefu huenda kukaashiria kuwa mimba imeharibika. Mama akigundua kuwa ishara hizi zimekoma kwa kasi, ni vyema kuwasiliana na mtaalum wa afya ya kike ama gynaecologist.
4. Kutohisi mwendo wa fetusi
Kwa kawaida, mwendo wa fetusi huhusishwa na ukuaji wa mtoto tumboni. Ni ishara chanya kuwa mtoto anakua ipasavyo. Mwendo huu huanza kuhisiwa kati ya wiki 16 na wiki 25. Huenda mama akahisi mwendo huu kabla ya wiki 16 na ni sawa na salama. Baada ya wiki 24 za ujauzito, mama anapaswa kuhisi mwendo zaidi. Lakini mwendo huu ukikoma, ni vyema kuwasiliana na gynaecologist.
Vyanzo vya kupoteza mimba katika trimesta ya pili
Magonjwa ya mtindo wa maisha. Ikiwa mwanamke ana kisukari, shinikizo la juu la damu, na magonjwa ya figo, nafasi zake za mimba kuharibika ziko juu.
Maambukizi. Baadhi ya maambukizi kama rubella, toxoplasmosis na malaria katika ujauzito kabla ya kujipandikiza kwa yai huenda kukasababisha mimba kutoka.
Cervix. Kizazi cha mwanamke huanza kuwa chembamba na kufunguka ili mtoto atoke. Lakini kizazi kikifunguka mapema katika trimesta ya pili, hali inayofahamika kama kizazi dhaifu, mama anaweza poteza mimba.
Kulinda dhidi ya kuharibika kwa mimba
- Koma kuvuta sigara katika mimba
- Epuka utumiaji wa vileo na mihadarati katika mimba
- Zingatia lishe yenye afya
- Jilinde dhidi ya maambukizi katika mimba kama vile rubella.
- Zingatia kuongeza uzito wenye afya katika mimba na fanya mazoezi yaliyo salama kwako na kwa mtoto
- Tumia vitamini za prenatal kama ulivyoshauriwa na daktari
Mwanamke anapogundua baadhi ya ishara za mama kupoteza mimba, ni vyema kwenda katika kituo cha hospitali bila kukawia. Kipindi baada ya kupoteza mimba huwa kigumu kwa wanandoa. Ila ni vyema kukumbuka kuwa huo sio mwisho wa kujaribu kuwa na mtoto. Wasiliana na daktari na kisha mzidi kujaribu kupata mtoto.
Chanzo: NCBI, Reuters
Soma Pia: Bwanangu anataka ngono kwa mdomo baada ya kupoteza mimba