Ishara Tatu Za Mama Mjamzito Kuacha Kazi

Ishara Tatu Za Mama Mjamzito Kuacha Kazi

Did you know that work after eight months of pregnancy is as harmful as smoking? There's actually a study to back this up.

Je, unafahamu ishara za mjamzito kuacha kazi? Na ni wakati upi bora zaidi wa mama mjamzito kuacha kazi? Hili ni mojawapo la maswala ambayo ni tofauti kwa kila mtu. Kina mama wengine huchagua kufanya kazi hadi siku za mwishoni za ujauzito ili kuhifadhi siku za likizo ya kujifungua mtoto anapowasili. Wengine huchagua kuwa na siku ya mwisho kabla ya siku ya kujifungua ili kupumzika ama kufanya mipango ili kufanyia kazi nyumbani. Hakuna jibu moja kwa swali, “ni ishara zipi thabiti za kujiepusha na kazi wakati wa ujauzito?” Lakini kuna mwongozo kutoka kwa wataalumu wa afya inayoweza kukusaidia kupanga likizo yako ya kujifungua. Hakikisha kuzungumza na mhudumu wako wa afya juu ya kazi yako na ujauzito.

Wanawake wengi wanaweza kufanya kazi zao za kawaida hadi kati ya wiki 32 hadi 34 ya ujauzito.  Kwa huu wakati pia, kina mama wengi huwa wanaelekeza fikira zao kutoka kwa kazi zao hadi kwa uzazi wanaotarajia . Hili linaweza kuathiri uamuzi wako na ni lini mwafaka kuacha kazi unapokuwa mjamzito. Iwapo unafanya biashara ya kibinafsi, itawakuwa vyema kungoja hadi mwisho wa ujauzito wako ili kuacha kazi.  Haitakudhuru, lakini iwapo utagundua ishara moja au hizi zilizoko hapa chini, acha kazi mara moja na ushauriane na daktari wako.

Ishara za kuacha kazi wakati wa ujauzito

ishara za mjamzito kuacha kazi

Kazi zingine zinaweza kuongeza athari za kumpata mtoto kabla ya wakati.  Kama vile kazi zinazohusu  kuinua vitu mzito, kelele inayopita kiasi ama kusimama kwa masaa marefu.  Zungumza na daktari wako kuhusu kupata maagizo ya kitiba ya  kubadilishiwa kazi unayoifanya.  Wanawake ambao wameweza kupata mtoto kabla ya wakati hapo awali pia wanaweza kuamua kuacha kazi mapema.

Bila kujali kazi unayoifanya, kuna ishara za kawaida ambazo ni ilani kuwa ni wakati mwafaka wa kuacha kazi unapokuwa mjamzito.  Je, kukosa usingizi kunaathiri kazi yako?  Ama unatiwa wasiwasi na matayarisho ya mtoto ambayo hayajakamilika huko nyumbani?  Inaweza kuwa wakati unaofaa kwako kufikiria kuacha kazi.

1. Unapoteza motisha  mchana

Kukosa usingizi usiku kunaathiri kazi yako ya mchana na kukufanya kuwa mnyogofu, kununa au  kusahau vitu.  Pia unajipata ukitilia mkazo matayrisho ambayo hayaja kamilika yanayo kungoja nyumbani.

2. Kukaa chini na kusimama kunachugachuga

Kuumwa na mgongo, miguu iliyofura na Kukosa hewa ni ishara kuwa unahitaji wakati mwingi wa kupumzika iwapo kazi yako inahitaji kusimama mno.

3. Unapata dalili za kupatwa na uchungu wa uzazi wa mapema.

Uchungu uliokithiri wa mgongo na kuvunja damu inamaanisha unahitaji kumwona daktari mara moja. Kuna uwezekano daktari wako ataagiza kupumzika kitandani.

Ikiwa utahisi hivi katika nyakati za mwanzo za ujauzito, ni vizuri kuongea na daktari wako kwani una uwezo wa kufanya kazi vizuri katika kipindi hiki.  Lakini ikiwa hili litafanyika katika vipindi vya mwisho vya ujauzito, acha kazi na uweze kupumzika nyumbani.  Kwa sababu akili ya mama yenye afya inaweza kumsaidia mtoto kukua vizuri ndani yake.

Na kama tulivyosema hapo awali, kila mojawapo wa ishara hizi ni tofauti kwa kila mtu anafaa kujadiliana  na daktari wake.

Hali Za Kimatibabu Zinazo Kuhitaji Kuacha Kazi Mapema

ishara za mjamzito kuacha kazi

Kuna hali ambazo daktari wako atapendekeza uache kazi.  Hizo ni zile zitakazohitaji kulazwa hospitalini na kuangaliwa.  Zingine itabidi ukae nyumbani.  Kila hali yafaa kuwa ya kibinafsi na ushauri kutoka kwa daktari.

Hii hapa chini ni mifano ya sababu za kimatibabu ambazo daktari hupendekeza kupunguza au kuacha kazi unapokuwa mjamzito:

  • Kondo ya nyuma kushuka 
  • Placenta accrete
  • Kupasuka kwa mapema kwa tando za kijusi
  • Kufunguka kwa mapema kwa mlango wa tumbo la uzazi
  • Mapacha walio kwenye athari ya kuzaliwa kabla ya wakati
  • Msogo mkubwa wa damu
  • Kama uliweza kumpata mtoto kabla ya wakati hapo awali
  • Mtoto aliye na kizuizi cha kukua ndani mwa tumbo la uzazi
  • Uchungu wa uzazi wa mapema
  • Kupunguka kwa maji yanayo zingira mtoto 

 

ishara za mjamzito kuacha kazi

Kama tulivyoeleza awali, kila mojawapo wa hizi ishara inafaa kuchukuliwa kibinafsi na ushauri kuchukuliwa kutoka kwa daktari.

Faida za kuacha kazi kabla ya kujifungua

Kwa kina mama wengi kufanya kazi wakati wa ujauzito sio kama kazi za nyumbani. Unaweza furahia kutoka nje ya nyumba na kuwa na jambo la kufanya wakati wa mchana.

Hatimaye, itabidi umechukua wiki chache kwa sababu za kitabibu. Ingawa itakuwa yadhamana.  Pia maamuzi ya lini kuacha kazi unapokuwa mjamzito ni ya kibinafsi na mojawapo ya uamuzi unafaa kufikria vizuri pindi unapokuwa mjamzito.

Also read: The Symptoms Of Stillbirth And How To Avoid Them

 

 

Written by

Risper Nyakio