Je, Ni Ishara Zipi Zinazo Msaidia Mama Kujua Kuwa Anatarajia Mtoto?

Je, Ni Ishara Zipi Zinazo Msaidia Mama Kujua Kuwa Anatarajia Mtoto?

Ukishuku kuwa una mimba kisha ushuhudie mojawapo ya ishara hizi za mapema za mimba, hakikisha kuwa unaenda kufanyiwa kipimo kwenye kituo cha afya.

Je, una wasiwasi kuwa huenda ukawa na mimba? Njia pekee ya kudhibitisha ni kwa kufanya kipimo cha mimba. Lakini kuna ishara za mapema za mimba ambazo huenda zika elekeza kuwepo kwa mimba. Tazama.

Je, wanawake wote hupata ishara za mapema za mimba?

Wanawake wote ni tofauti, na wanacho kipitia kabla ama wakati wa mimba pia kina tofautiana. Ishara za mimba za mapema huwa tofauti kwa kila mwanamke. Na huenda wengine wakakosa kugundua kuwa wana ishara hizi kwa sababu huwa sawa na ishara kabla ya kipindi chako cha hedhi. Kinacho fuata ni maelezo ya ishara za mapema za mimba, lakini kumbuka kuwa huenda ishara hizi zikasababishwa na kitu tofauti na mimba. Njia hasa ya kuwa na majibu sahihi kuhusu kuwa na mimba ni kufanya kipimo.

Orodha ya ishara za mapema za mimba

  • Kuvuja damu na kuumwa na tumbo

ishara za mapema za mimba

Baada ya kutunga mimba, yai linajipandikiza kwenye kuta ya uterasi na kusababisha mojawapo ya ishara za mapemza zaidi; kuvuja damu na wakati mwingine kuumwa na tumbo.

Damu ya aina hii inafahamika kama damu ya kujipandikiza kwa yai (implantation bleeding). Na hufanyika siku 6 hadi 12 baada ya yai kupatana na manii yenye afya na kurutubishwa. Kuumwa kwa tumbo kunako shuhudiwa katika hatua hii ni sawa na uchungu wa hedhi. Huenda mwanamke akadhania ni uchungu wa kuanza kwa kipindi chake cha hedhi. Tofauti ni kuwa, uchungu huu ni mwepesi na pia kiwango cha damu ni kidogo ikilinganishwa na cha hedhi.

  • Mabadiliko kwenye matiti

Hii ni ishara  nyingine ya mapema ya mimba. Baada ya kutunga kwa yai, homoni hubadilika sana mwilini mwa mwanamke. Kufuatia mabadiliko haya, chuchu huenda zikafura, kuuma ama kuwasha baada ya wiki moja ama mbili. Huenda zikahisi nzito kuliko kawaida ama laini zaidi. Sehemu inayo zunguka chuchu(areola) huenda ikawa nyeusi zaidi.

Uchungu huu huenda ukawa na vyanzo vingine. Lakini kama ni ishara ya mapema ya mimba, itachukua muda kabla ya viwango vya homoni kubadilika. Ikifanyika, uchungu huu utapungua.

  • Kichefu chefu (ugonjwa wa asubuhi)

Kuhisi kichefu chefu ni ishara maarufu ya mimba, lakini sio wanawake wote wanao ishuhudia. Wataalum hawaja dhibitisha chanzo cha kichefu chefu bado, mwanamke anaweza shuhudia hali hii wakati wowote wa mchana, ila ni maarufu zaidi asubuhi.

Baadhi ya wanawake huathiriwa na harufu ya vyakula fulani wanapokuwa na mimba. Chakula walicho kifurahia hapo awali kinaweza badilika na kuwa wasicho penda kukiona. Haya yote ni kufuatia mabadiliko ya homoni mwilini. Kuna uwezekano wa kichefu chefu kudumu safari yote ya mimba. Mama anaye tarajia anapaswa kukumbuka kula chakula chenye afya kitakacho mfaa yeye na mwanaye.

  • Uchovu mwingi

Kuhisi uchovu mwingi ni ishara ya kuwa mjamzito ya mapema. Mwanamke anaweza anza kuhisi uchovu mwingi wiki moja baada ya kutunga mimba. Uchovu huu unahusishwa na kiwango cha juu cha homoni ya progesterone. Hakikisha unapata usingizi tosha na pia kula protini kwa wingi.

Mbali na mimba, huenda uchovu huu ukasababishwa na viwango vya chini vya sukari kwenye damu, shinikizo la chini la damu na kuboresha utoaji wa damu.

  • Kukosa kipindi cha hedhi

Hii ndiyo ishara wazi zaidi ya mimba, na inayo wafanya wanawake wengi wafanye kipimo cha mimba. Kuna sababu zingine zinazo sababisha kuchelewa kwa kipindi chako cha mimba kama vile kuwa na fikira nyingi, kutumia tembe za kudhibiti uzazi ama kubadilisha mazingira.

Katika kesi zilizo nadra, baadhi ya wanawake hushuhudia kuvuja damu wakiwa na mimba. Huenda ikawa ishara kuwa una tatizo la kiafya. Hakikisha kuwa una wasiliana na daktari akufanyie vipimo. Fanya kipimo cha mimba kuhakikisha kama una mimba ama la.

Ishara zingine za mimba za mapema ni kama vile:

kupoteza mimba ya wiki mbili

Kuumwa na mgongo na kichwa. Baadhi ya wanawake hushuhudia kuumwa na mgongo na wengine maumivu ya kichwa.

Kuhisi kizungu zungu na kuzirai. Inaweza husishwa na kupanuka kwa mishipa ya damu ama viwango vya chini vya sukari kwenye damu.

Mhemko wa hisia. Huwa kawaida sana katika trimesta ya kwanza.

Kuenda haja ndogo mara kwa mara. Kwa wanawake wengi, hili huanza katika wiki ya sita ama nane baada ya kutunga mimba. Fanya kipimo kwani huenda ikawa pia ni ishara ya maambukizi ya mfumo wa kukojoa ama kisukari.

Ukishuku kuwa una mimba kisha ushuhudie mojawapo ya ishara hizi za mapema za mimba, hakikisha kuwa unaenda kufanyiwa kipimo kwenye kituo cha afya.

Chanzo: WebMD

Soma Pia:Mbinu Ya Kupima Mimba Kutumia Baking Soda Ni Ya Kuaminika Ama La?

Written by

Risper Nyakio