Je mapenzi yetu ni ya ukweli ama bandia?
Ikiwa uko katika uhusiano na hatimaye ufikirie kumjuza mchumba wako kuwa unampenda, lakini anaitikia kwa kusema "asanti" ama kunyamaza utahisi kana kwamba dunia yako inaporomoka. Utaanza kushangaa iwapo kwa kweli alikuwa anakupenda ama ulikuwa kwa uhusiano peke yako. Hii ni ishara bayana kuwa hisia zako kwako ni tofauti na hisia zako kwao.
Fahamu ishara za mapenzi bandia zinazodhihirisha kuwa mchumba wako hana mapenzi kwako.
Ishara za Mapenzi Bandia

- Wanajitenga kihisia
Katika uhusiano, wapenzi bandia huwa na uraibu wa kutozungumza. Kisha kutoa vijisababu vingi kama vile walikuwa kazini, walikuwa na kazi nyingi na hawangeweza kuzungumza. Mtu anayekupenda kwa dhati, atazungumza nawe kila mara anapopata chanya na atatia juhudi zaidi hata isipowezekana.
2. Majukumu yote ni yako
Wapenzi bandia hukuacha kupanga kila kitu, hawatii juhudi kujua unavyoendelea na hawachukui majukumu yoyote. Je, mchumba wako anafanya juhudi zozote? Ama wewe ndiye unayejaribu kuhakikisha kuwa mambo yako sawa wakati wote? Uhusiano huwa kati ya watu wawili, ambao wanapaswa kufanya juhudi sawa kuhakikisha uhusiano unasonga mbele. Kutotia juhudi zozote ni ishara ya mpenzi bandia.
3. Kutoshughulika
Katika uhusiano halisi mchumba wako atataka kufahamu unavyoendelea, kukujulia hali, kujua kinachoendelea maishani mwako na nyanja zingine. Ila, ikiwa hazungumzi nawe ama kutaka kujua kinachoendelea. Ikiwa mchumba wako hashughuliki kujua kinachoendelea maishani mwako, bila shaka hakupendi.

4. Hawakusaidii kutatua matatizo yako
Migogoro na kuvurugana huwa kawaida katika uhusiano na wapenzi wote wawili wanahitajika kutia juhudi kuyatatua. Kila mtu akubali jukumu lake kisha nyote mfanye juhudi za kutafuta suluhu la yanayowakumba. Ikiwa mmoja wenu hayuko tayari kukubali jukumu lake na wala hatii bidhii kukusaidia. Bila shaka hakuna mapenzi ya ukweli katika uhusiano wenu.
5. Hana mipango ya siku za usoni nawe
Katika uhusiano ambao wapenzi wana uhakika nao, mada ya maisha yenu ya usoni pamoja kama kujenga nyumba, kupata watoto, kufunga ndoa hutokea mara nyingi. Kupanga kuzuru kwa pamoja, kufanya mambo yanayowafurahisha pamoja. Ikiwa mpenzi wako hapendelei mazungumzo kama haya, ana tatizo la kujitolea katika uhusiano, ama haoni maisha marefu nawe.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Je, Kuna Madhara Ya Kufanya Mapenzi Kwa Mjamzito?