Kutoa shaka zote kuwa mimba yako ina tatizo na kuwa mtoto anakua ipasavyo na ana afya kwenye uterasi, ni muhimu kwa mama kufahamu ishara za mimba yenye afya na isiyo na afya.
Ishara za mimba yenye afya

Mwendo wa fetusi
Mama anapofikisha miezi tano ya ujauzito, fetusi huanza kuwa na mwendo kwenye uterasi. Mwendo wa mtoto huongezeka kunapokuwa na mwangaza. Katika mwezi wa saba, mwendo wa mtoto huathiriwa na sauti, mwangaza na uchungu. Mama anapofikisha mwezi wa nane, mwendo wa mtoto huongezeka na kupunguka katika mwezi wa tisa kufuatia kukosa nafasi tosha tumboni.
Kuongeza uzito katika mimba
Kwa kawaida, mama mwenye mimba huongeza kati ya kilo 10 hadi 15 za uzani anapokuwa na mimba. Kila anapoenda kliniki, uzito wake hupimwa kudhibitisha iwapo mtoto anakua ipasavyo. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote, ni vyema kwa mama kuwasiliana na daktari wake.
Ukuaji wa kawaida
Fetusi hukua kwa inchi mbili kila mwezi. Katika mwezi wa saba, fetusi huwa inchi 14. Mama anapokaribia kujifungua katika mwezi wa tisa, fetusi inapaswa kuwa kati ya inchi 18 hadi 20 za urefy na kilo kati ya 2.5 na 3. Kipimo cha ultrasound hufanyika kudhibitisha iwapo mtoto anakua kwa njia ipasayo na iwapo ana changamoto zozote za kifizikia.
Mpigo wa moyo
Moyo wa mtoto aliye kwenye uterasi huanza kupiga katika wiki ya tano ya ujauzito. Kuna kipimo kinachofanyika kudhibitisha mpigo wa moyo wa mtoto. Unapaswa kuwa kati ya 110 na 160 kwa kila dakika.
Nafasi ya mtoto katika kipindi cha uchungu wa uzazi
Katika mwezi wa tisa, fetusi huwa imekua na kuchukua nafasi nyingi kwenye uterasi, na hivyo basi kupunguza mwendo wa fetusi tumboni. Mtoto mwenye afya huwa na kichwa chini katika uchungu wa uzazi ili kichwa kianza kutoka mama anapojifungua.
Ishara za fetusi isiyo na afya

Urefu usio wa kawaida
Kipimo cha kudhibitisha ukuaji wa mtoto hufanyika ili daktari aweze kufahamu iwapo mtoto anakua apasavyo kadri mimba inavyozidi kukua.
Fetusi kukosa mpigo wa moyo
Moyo wa fetusi huanza kupiga katika wiki ya tano, hata hivyo, udhibiti bayana hufanyika katika wiki ya 10. Kuna kifaa cha kieletroniki kinachotumika kudbitisha mpigo wa moyo wa fetusi. Mtoto asipofikisha mpigo unaohitajika, wanafahamu kuwa kuna tatizo.
Kuumwa na tumbo zaidi katika mimba
Ujauzito ni kipindi cha kusisimua pamoja na kuhisi uchungu na uchovu. Maumivu mepesi ya tumbo muda kwa muda huwa sawa. Ila, maumivu haya yanapozidi, ni ishara kuwa kuna kasoro na mama anapaswa kuwasiliana na daktari.
Kutokwa na damu katika ujauzito
Kuna baadhi ya wanawake wanaoshuhudia kutokwa na damu wanapokuwa na mimba. Hata hivyo, damu hii huwa kiasi kidogo. Kutokwa na kiasi kikubwa cha damu ni ishara ya hatari na huenda ikadhihirisha kuwa mama anapoteza mimba.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vidokezo 5 Vya Kuwa Na Ujauzito Salama Na Wenye Afya