Mtoto Kukosa Hewa Anapobadilishwa Diaper Kwa Sababisha Kifo Chake

Mtoto Kukosa Hewa Anapobadilishwa Diaper Kwa Sababisha Kifo Chake

A 26-year-old mum just left the room to get her baby a bottle, not knowing her little one was suffocating on the changing table...

Je, ni rahisi mtotokukosa hewa? Kina mama na baba, mwaweza kuwa mnajua madhara yaliyopo mnapomwacha mtotokwenye kihero ama kitanda cha watu wazima.  Lakini hata yale maeneo yanayokaa salama yanaweza kuwa ya kuhatarisha.  Tukio moja la kuogopesha lililotokea kwa mama mmoja, linatuelimisha kuhusu ishara za ukosefu wa hewa kwa watoto.  Na madhara ya kumwacha mtotobila kuangaliwa ata kwenye meza ya kumbadilisha diaper.

Ishara za ukosefu wa hewa kwa watoto ambazo tunafaa kujua kupitia kwa tukio la kuogopesha lililompata mama

Kulingana na chumba cha habari KCCI 8 Des Monies, Laci Lynn mwenye miaka 26, mama ya mtotoaliyekuwa wa miezi mitatu ameshtakiwa kwa kuhatarisha kuliko sababisha kifo.

Ripoti zinasema kuwa mama huyo wa watoto wawili alimwacha mtotowake wa kike bila kuangaliwa juu ya meza ya kumbadili diaper. Baada yake kutoka kwa chumba, mtotoakajipinda na kulala kwa tumbo lake hivyo shingo yake ikifinywa kwenye ukingo wa meza. Matokeo yake nikuwa mifumo ya mtotoya kupitisha hewa ilifungika na mtotoakafa kwa Kukosa hewa.

Wenye mamlaka wanasema kuwa linalofanya hili kuwa hatia ni kuwa mama alimwacha mtotokwa muda mrefu bila kumwangalia.  Cha zaidi, ni kuwa mama alijua vizuri kuwa mtotoalikuwa anaweza kuijpinda.

ishara za mtotokukosa hewa

This tragic case highlights baby suffocation signs and risks parents should know about. | Screenshot: KCCI 8 News video

Licha ya haya, babake mtotoanasema kuwa hamlaumu bibi yake kwa lililotokea.

“Sina chochote ndani yangu kinachomtilia lawama mke wangu,” akasema baba mtotoDon Taylor akiongeza kuwa ni ajali mbaya inayoweza kumpata mzazi yeyote. Anakumbuka jinsi bibi yake alitoka kwa chumba ili kuchukua chupa ya mtoto.

“Hakuna siku ata moja ambayo sote wawili hatumfikirii huyo mtoto, na matukio ya hio siku yangali akilini mwetu,” Taylor akakiambia kituo cha habari.

Nyoyo zetu zinaiendea familia ya mtotohuyu mchanga. Twawaombea wapate nguvu na faraja katika siku hizi ngumu zifuatazo.

Kina mama na baba, jitahadhari na ishara hizi za ukosefu wa hewa kwenye watoto

Kilichomtendekea huyu mtotoni cha kuvunja moyo.  Ata cha kuogofya zaidi, ni kuwa inaweza mfanyikia mzazi yeyote. Unafanya juu chini kumkinga mtotowako kutokana na kihero na kitanda cha mtotolakini maeneo yoyote yanaweza kuwa yenye hatari.

Ingawa kupinda kwa tumbo ni awamu kuu katika kukua kwa mtoto, inaweza kuwa chanzo cha ukosefu wa hewa kwa mtotokama tukio hili linavyoonyesha.

Kama ilivyotajwa awali, mtotoalijipinda kwa tumbo lake na akosa hewa alipofinywa kwenye ukingo wa meza. Kwa hivyo ni vizuri kujua kuwa maeneo yoyote nyumbani yanaweza kuwa ya hatari.

mtoto

Ishara za ukosefu wa hewa kwenye watoto za kuzingatia

Ukosefu wa hewa kutokana na kufungika kwa mifumo ya kupitisha hewa kwa kusonga kabisa na malazi, mifuko ya plastiki husimamia asilimia 80% ya vifo kutokana na ajali kwa watoto wachanga U.S pekee.

Mtoto aliye na ukosefu wa hewa, anaweza onyesha dalili za kushindwa kupumua na kugeuka rangi kuwa bluu; petechiae (madoa ya rangi nyekundu) yanaweza kutokea kwenye uso na macho pia

Hili linapotendeka hakikisha kuondoa pingamizi kwa mifumo ya mtotoya kupitisha hewa. Kama kuna chombo kinachoifunga kitoe ama umfanyie heimlich ya watoto kama inavyotakikana.  Iwapo haufahamu jinsi ya kuendelea, mkimbize mtotokwenye hospitali iliyoko karibu nawe ama wapigie simu wahudumu wa matibabu ya dharura bila kusita.

Hizi ndizo njia za kujikinga mtotokutokana na ajali nyumbani

Cha muhimu kuchukua kutoka kwa makala haya ni kutomwacha mtotobila uangalizi ata kama ni kwa dakika chache. Mengi yanaweza kutendeka ata kama ni kwa dakika chache.

Hizi ni tahadhari zaidi za kujikinga kutokana na ajali nyumbani za mtotokukosa hewa.

hatari za kumwacha mtotobila kumchunga

Katika beseni la kuogea:

 1. Hakikisha kuangalia kiwango cha joto kwenye maji na kikwe cha mkono wako kabla ya kumweka mtotondani ya beseni.
 2. Weka vifuniko vya usalama kwenye mifereji ama bomba.
 3. Weka mikeka isiyo ya kuteleza kwenye chumba cha kuogea – ndani na nje ya beseni la kuogea.
 4. Hakikisha vikalio za choo zina lock za watoto za kukinga kutokana na ajali.

Kwenye chumba cha mtoto:

 1. Ondoa zagaazagaa ama vichezeo vyenye hatari kwenye kihero cha mtoto.
 2. Usiweke virembesho kama mito laini, vichezeo, vitandiko kwenye kihero na blanketi kukinga kutokana na kunyongwa na ukosefu wa hewa.
 3. Weka monita isiyo na kamba kuhakikisha usalama wa mtotowako.

Kwenye gari:

 1. Tumia kiti cha mtotokinachoangalia nyuma mpaka awe zaidi ya miaka miwili ama mpaka apitishe urefu na uzito wa kiti unaohitajika.
 2. Hakikisha kuwa kiti cha gari kimefungika vizuri mahali pake, katikati ya kiti cha nyuma.
 3. Weka kanda za mabega kwenye au chini ya mabega ya mtotowako kukinga kutokana na ukosefu wa hewa.
 4. Usiweke kwa hali yoyote ile blanketi chini ya kanda za kiti cha mtoto.

Nyumbani:

 1. Je, una ngazi nyumbani mwako? Hakikisha kuweka lango la usalama kwa mtotowako.
 2. Iweke runinga yako mahali palipo juu ili watoto wasije kuifikia. Hakikisha kuwa nyaya ziko dhabiti.
 3. Tumia pazia sizizo na kanda kukinga kutokana na kujinyonga.
 4. Hakiki kuweka vifuniko vya usalama kwenye kingo kali za rafu za chini, meza na kadhalika.

Kuwa mwangalifu kutokana na ajali zisizotarajiwa za nyumbani kunaweza okoa maisha ya mtotowako.

 

Source: USA Today, American SIDS Institute, National Safety Council

ALSO READ: Mum warns others after her baby suffers brain damage from a fall

This article was published with permission of theAsianparent Singapore

 

Written by

Risper Nyakio