Jinsi Ya Kufahamu Iwapo Mtoto Anaye Nyonya Ameshiba

Jinsi Ya Kufahamu Iwapo Mtoto Anaye Nyonya Ameshiba

Mama anapo nyonyesha mtoto ana himizwa kuwa makini kuangalia anavyo nyonya na wala sio kuangalia wakati anao chukua kunyonya ili kubaini iwapo ameshiba ama la. Sio vyema kumwanzia mtoto ratiba ya kunyonya hasa katika miezi ya kwanza michache. Mwache mtoto anyonye kadri awezavyo hadi atakapo shiba na wakati anapo hisi njaa. Hakikisha kuwa amemaliza kunyonya kutoka chuchu moja unapo mbadilisha upande. Ishara za mtoto kushiba anapo nyonya ni kama zipi?

Ishara Za Mtoto Anaye Nyonya Kushiba

ishara za mtoto kushiba

  1. Unambadili mtoto wako nepi iliyo jaa kila siku
  2. Unambadili nepi mara 5-6 kwa siku baada ya siku ya nne
  3. Kinyesi chake kinaanza kubadili rangi kutoka nyeusi hadi kuwa kijani na kisha manjano
  4. Uzito wa mtoto kuongezeka

Ishara hizi zinamjuza mama kuwa mwanawe ana nyonya vyema na ifaavyo. Usiwe na shaka unapo gundua kuwa kuna baadhi ya siku ambazo mtoto wako hanyonyi vizuri na ana sumbua sana. Huku siku zingine akinyonya vyema. Yote haya ni kawaida. Hakikisha kuwa anachukua muda kwa chuchu moja na kumaliza kisha umbadilishe upande. Kuwa makini na unavyo mshika anapo nyonya. Kwani unavyo mshika pia kunachangia katika jinsi atakavyo nyonya.

Ikiwa una tatizika kutoa maziwa ya mama, ni vyema kuwasiliana na daktari wako ili akushauri utakavyo fanya ili kuboresha utoaji wa maziwa ya mama. Kwa mama anaye mkamulia mtoto maziwa, hakikisha kuwa umemkamulia maziwa ya kutosha.

Kinacho dhibiti utoaji wa maziwa

ishara za mtoto kushiba

Utoaji wa maziwa unadhibitiwa na homoni ya prolaktin. Kadri mama anavyo nyonyesha sana ndivyo kiwango cha homoni hii kinavyo zidi kuwa kingi na maziwa kutolewa kwa wingi. Mama anapo toa maziwa ya kutosha, ana uhakika kuwa mtoto ata shiba.

Ikiwa mama hanyonyeshi sana, kiwango cha homoni ya prolaktin inayo athiri utoajo wa maziwa ya mama kitashuka. Na idadi ya maziwa ya mama yanayo tolewa yatapungua. Na kumfanya mtoto akose maziwa tosha ya kukimu mahitaji yake ya kilishe. Mama anapaswa kuhakikisha kuwa anam nyonyesha mtoto wake angalau mara 8 hadi kumi kila siku.

Soma pia:Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

Written by

Risper Nyakio