Je, unatarajia mtoto wa kiume ama wa kike? Kugundua jinsia ya mtoto anaye kua tumboni mwako huwa mojawapo ya mambo ya kufurahisha zaidi katika ujauzito. Huenda ukawa na hamu nyingi ya kujua jinsia ya mtoto wako kiasi kwamba hauna uvumilivu wa kungoja hadi utakapo fanya ultrasound. Je, kuna njia zingine za kufahamu jinsia ya mtoto unaye tarajia? Tazama, ishara za mtoto wa kike.
Ishara za mtoto wa kike
- Mimba iliyo juu
Wanawake wa hapo kale waliamini kuwa ikiwa mimba yako ilikuwa juu, una tarajia mtoto wa kike. Ila ni vyema kukumbuka kuwa hii ni imani tu. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza mfanya mama kuwa na mimba iliyo juu. Ikiwa hii ni mimba yako ya kwanza, uko kwa shepu nzuri na misuli ya tumbo na umbo la mwili wako yata athiri jinsi utakavyo beba mimba yako.
Kwa hivyo jinsia haichangii katika mahali ambapo mimba yako itakuwa. Baada ya kubeba mimba kadhaa, utakavyo beba mimba yako pia itabadilika.
2. Kuongeza uzito mwingi karibu na katikati
Kuna imani kuwa mahali utakapo ongeza uzito mwingi pana lingana na jinsia ya mtoto unaye mtarajia. Ukigundua kuwa sehemu ya katikati imeongezeka sana, ni kwa sababu una tarajia mtoto wa kike. Kumbuka kuwa, jambo hili lina athiriwa na aina ya mwili wako na sababu zingine za kifizikia.
3. Mpigo wa moyo
Unapo enda hospitalini, hakikisha kuwa unasikiliza kwa makini daktari wako anapo sikiza mpigo wa moyo wa mtoto wako. Watu wana amini kuwa mpigo wa kasi wa 140 kwa kila dakika kuna maanisha kuwa una tarajia mtoto wa kike. Mpigo wa moyo wa msichana huwa wa kasi zaidi ikilinganishwa na wa kijana.
4. Kutamani vitu vitamu tamu

Kuwa na hamu ya kula vitu vitamu unapokuwa na mimba kuna husishwa na mtoto wa kike anaye kua tumboni mwako. Ikiwa una tamani kula vitu chachu na vyenye chumvi, una tarajia mtoto wa kiume.
5. Chunusi usoni
Ikiwa uso wako umegeuka kuwa wenye mafuta mafuta na wenye chunusi ama upele, una tarajia mtoto wa kike anaye jaribu kuchukua urembo wako. Ukweli ni kuwa, mabadiliko haya yana sababishwa na homoni mwilini katika safari hii.
6. Ugonjwa mwingi wa asubuhi
Unapo shuhudia ugonjwa wa asubuhi ulio zidi, una tarajia mtoto wa kike.
7. Mhemko wa hisia ama mudi
Unapo gundua kuwa una mhemko wa hisia usio tarajiwa, huenda ikawa ni kwa sababu una tarajia mtoto wa kike.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Dalili Za Mimba Ya Kiume: Jinsi Ya Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Unaye Mtarajia